✅️Hii ni shule ya Sekondari Mkalama One iliopo kata ya Nduguti, Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida.Shule hii ilianzishwa kama sehemu ya juhudi za kuboresha upatikanaji wa elimu ya sekondari katika wilaya hiyo.
✅️Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ilipokea jumla ya Tsh.544,225,626 kwa ajili ya ujenzi wa shule hii. Fedha hizi zilitumika kujenga miundombinu muhimu ikiwa ni pamoja na madarasa ,nyumba za walimu na ofisi za Utawala. Hatahivyo, Halmashauri ilipokea 110,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mpya za walimu.
TUELEZE BILA HIYANA WALA KINYONGO MAHALI ULIPO NA MNANUFAIKA NA NINI WENZETU😁😁😁
@sisiniTanzania@NCHIYANGUT@matokeochanya@AsyaMessos@Mwafricas
#sisinitanzania #nchiyangukwanza #kazinaututunasongambele #mslac
Kwa mara ya kwanza katika historia sherehe za Mei Mosi kitaifa zimefanyika mkoani Singida katika uwanja wa Bombadia. Sherehe hizo zimeongezewa radha na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa asilimia 35.1 ,Singida ni yenye neema na baraka
Zaidi ya bilioni 4 zimetekeleza miradi mbalimbali ya afya na kununua vifaa tiba katika Halmashauri ya Mkalama katika kipindi cha miaka minne ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwaajili ya kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Mkoa wa Singida umepata heshima ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya Mei Mosi. Karibuni Singida zaidi karibuni Mkalama kwenye kuku watamu kushinda wote duniani.
Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama tayari imeshatoa jumla ya shilingi 395,500,000/= kwa vikundi 73 ili kusaidia kuimarisha biashara zao na kunyanyua uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Serikali imeendelea kuboresha makazi ya walimu, kwenye picha ni nyumba ya walimu (2 in 1) yenye thamani ya Shilingi 95,000,000 katika kijiji cha Maziliga, kata ya Nduguti Wilayani Mkalama
Nimeshiriki Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995 Toleo la Mwaka 2023 jijini Dodoma, ambapo mgeni rasmi ni Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hafla ya utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum. Halmashauri imetoa jumla ya shilingi 395,500,000/= kwa vikundi 73
Utoaji wa mikopo hii ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, serikali imeelekezwa kuhakikisha inatoa mikopo kwa wajasiriamali.
Shule ya Sekondari ya Mkalama One. Shule hii ni mpya imejengwa kwa gharama shilingi milioni 555. Awali wanafunzi wote wa kata ya Nduguti walikuwa wakisoma katika Shule ya Sekondari ya Nduguti, kujengwa kwa shule hii kumepunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya Nduguti.
WANANCHI MKALAMA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA (MSLAC)
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wameonyesha furaha na shukrani zao za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuanzisha na kufanikisha Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC). Kampeni hii inalenga kuhakikisha haki za wananchi, hususan wanyonge, zinalindwa na kila mmoja anapata msaada wa kisheria bila ubaguzi.
Wakizungumza katika tukio la uhamasishaji wa msaada wa kisheria lililofanyika hivi karibuni, wananchi wamepongeza jitihada za Rais Samia katika kuleta huduma hiyo karibu na jamii, wakisema kuwa imekuja kwa wakati mwafaka kwani changamoto za kisheria zimekuwa zikikabili wananchi wengi, hasa wale wa kipato cha chini.
Mmoja wa wananchi, Bi. Rehema Juma, alisema, "Kampeni hii ni msaada mkubwa kwetu. Awali tulikuwa tunahangaika sana kufuatilia haki zetu kwa sababu ya ukosefu wa uelewa na gharama kubwa za kisheria. Tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia kwa moyo wa upendo na kuwajali wanyonge."
Kwa upande wake, Bw. Julius Mkomwa, mkazi wa Mkalama, alisisitiza kuwa msaada wa kisheria unasaidia kupunguza migogoro ya kifamilia, migogoro ya ardhi, na hata matatizo mengine yanayohusiana na haki za binadamu. Aliongeza kuwa kampeni hii inatoa nafasi kwa wananchi kujifunza sheria na haki zao ili waweze kujilinda kisheria.
Kwa mujibu wa viongozi wa kampeni, MSLAC inalenga pia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu sheria, haki, na wajibu wao. Kampeni hii imekuwa ikitekelezwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo mawakili wa kujitolea, wanasheria wa serikali, na asasi za kiraia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama alieleza kuwa juhudi za Rais Samia zimekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha amani na utulivu kwa kuwezesha wananchi kupata haki zao kwa wakati na kwa usawa.
Aliongeza kuwa msaada wa kisheria kupitia MSLAC utaendelea kutolewa kwa wananchi wote, huku juhudi za uelimishaji zikiimarishwa zaidi ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Wananchi wa Mkalama wanaahidi kuendelea kumuunga mkono Mhe. Rais Samia katika juhudi zake za kuwaletea maendeleo na kuhakikisha kuwa haki na usawa vinapatikana kwa kila Mtanzania.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) inadhihirisha dhamira ya dhati ya serikali ya awamu ya sita katika kuimarisha mifumo ya kisheria na haki za kijamii kwa maslahi ya wananchi wote.
#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @IkuluMawasiliano
Serikali imeleta mbegu ya mahindi ya ruzuku ikiwa ni jitihada za kusikiliza kilio cha wakulima kutokana na kupanda kwa bei ya mbegu ya mahindi. Mbegu ya mahindi kabla ya ruzuku iliuzwa shilingi 19,000 baada ya ruzuku mbegu inapatikana kwa shilingi 14,000 kwa kilo.