Wanangu si tulikubaliana ni swala la muda, sasa papara zinatokea wapi?
Wanangu, Mtaniumiza sana nikija kufahamu usiku kabla ya kulala stress zenu ni Irene wa Ifm kwanini namba yake inatumika muda wote, atakuwa anaongea na nani?
Wanangu nataka tuwe na mentality ya kitajiri, tuote ghorofa hata kama tumepanga geto, godoro na mkeka..
Wanangu mi nataka tuingie yard tuulizie bei za Laptop na magari, hata kama nauli mfukoni ni mzozo.
Wanangu sitapenda hali zetu za sasa zituzuie kuota ndoto kubwa za KESHO..
Wanangu nataka tuamini sisi ni imara hata kama tutakosa hela.
Sitaki unyonge wanangu, Najua Mnanielewa✊
Kijiweni leo @AziziKasese alikua anatufokea🙌Laptop Kali wacheck hawa @chandolaptop 🙏
BARUA YA LINCOLN KWA MWALIMU WA MTOTO WAKE!🙌
Mwanangu, Atapaswa kujifunza, kwamba binadamu wote hawapendi haki, binadamu wote si wakweli. Ila mfundishe pia kuwa kwa kila mwanasiasa mbabaishaji, kuna kiongozi anayejitoa.
Mfundishe, kwa kila adui kuna rafiki. Mfundishe, dola moja iliyovujiwa jasho ina thamani kuliko dola tano za kuokota.
Mwache ajifunze mapema kuwa waonevu ni rahisi kujikomba.
Shuleni, mfundishe kuwa ni heshima kubwa kufeli kuliko kufanya udanganyifu.
Jaribu kumpa mtoto wangu nguvu asifuate umati, pale kila mtu anapofuata mkumbo.
Mfundishe asikilize watu wote, lakini mfundishe pia kuchuja yote anayosikia.
Mfundishe kuziba masikio kwenye kelele za waombolezaji.
Mfundishe kwa upole, ila usimdekeze, kwa sababu ladha ya moto hukifanya chuma kiwe imara.
Mfundishe, jinsi ya kucheka akiwa na majonzi.
Na awe mwangalifu na utamu uliopitiliza😔
Kijiweni Leo na Mwalimu wa zamu @AziziKasese ✊Laptop bora wacheck @chandolaptop 🙏
Ukiwa mwanamme unatakiwa uishi kwa machale sana.
Asubuhi unaweza kuwa na laki, Jioni ukaingia kulala na madeni.
Mwanaume anahitaji utashi wa ziada,
Haijalishi mpenzi wako ni msomi wa aina gani, ujasiri wako ndio utakaoiongoza familia.
Kuna nyakati rudi nyumbani na vizawadi, kuficha maumivu ya kukosa..
Na usizoeleke sana, Kuna muda kuwa mkali tu, ilihali michongo yote imetiki..
Kuna muda na wewe shangilia tamthilia anayoipenda mke wako, kumsaulisha ulivyomfokea mchana.
Bro, Maisha ni Kama tamthilia ya ISINGO kila siku maisha yana visa vipya✍️ Cc @AziziKasese … Nunua laptop apa @chandolaptop
Wanangu si tulikubaliana ni swala la muda, sasa papara zinatokea wapi?
Mafanikio sio mchakato wa haraka, tusubiri na kwasababu tunapumzi basi tutayapata.
Mtanikwaza sana nikigundua mna hustle ili kummiliki yule slay queen wa mabibo mwisho.
Mtaniumiza sana nikija kufahamu usiku kabla ya kulala stress zenu ni Irene wa Ifm kwanini namba yake inatumika muda wote, atakuwa anaongea na nani?
Wanangu nataka tuwe na mentality ya kitajiri, tuote ghorofa hata kama tumepanga geto, na mkeka..
Wanangu mi nataka tuingie yard tuulizie bei ya magari, hata kama nauli mfukoni ni hatuna.
Bro, ni kheri ujitume kwenye kazi izoizo wanazoziona za Ajabu kuliko KUOMBA OMBA✊
Muhariri @AziziKasese 👊 Chukua laptop yako hapa @chandolaptop
Dada, ukimkataa mwanaume wakati hajajipata.
Fikiria mara mbili kabla haujamkubalia nyakati ambazo ana mafanikio.
Kuna uwezekano, wewe ni sehemu ya kisasi chake..
Kuna wakina sisi, tukiugua na familia inaumwa.
Mungu tuepushe na maradhi yatakayotuzuia tusitoke kutafuta riziki..
Tuepushe na magonjwa yatakayomaliza akiba zetu kiduchu.
Amein..