@MsigwaGerson Hivi hizi pesa zinazotolewa na Mtukufu Raisi bila kupitishwa kwenye bajeti ya na kuidhinishwa na Bunge ,Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali anapata nafasi ya kuzikagua kweli?? kama tuliweka sheria kwanini hatuzifuati??
Ukimsikiliza JPM na vijembe vyake juu ya waraka wa Maaskofu unajiuliza hivi kweli hawa ndio viongozi tulionao? Maswali magumuu halafu majibu mepesi kabisa tunasafari ndefu sana .
Dhamira inaweza kuwa njema sana,lakini dhamira bila mipango madhubuti ni ujinga tu! Sidhani kama kipaumbele cha kwanza cha watanzania ni kununua ndege na kujenda reli, tukiwakosoa msituweke kwenye viloba mkatutupa cocobeach kaeni mtafakari.
@BMatungwa @MagufuliJP@MbarawaM Kama umeme uliopo hauwezi hata kuwasha friji leo nisiku takribani nne kwa baadhi ya maeneo hapa Dar es salaam,basi labda hiyo treni itatumia power bank, vinginevyo hizi ni plan zisizo na maono na mwisho wasiku tutauita ukurupukaji bila mipango.
@UpdaterTanzania @RemigiorC @UNHumanRights@humanrightstz@MariaSTsehai Ikiwa unajua unamatatizo ya akili ni vizuri ukameza dawa zako kabla ya kuongea na media in public vinginevyo utaonekana kichaa huna akili na utapuuzwa tu.
@salim_alkhasas@hancymachemba Najiuliza tu Askari wetu hasa wanajeshi walioishia kidato cha nne wanaotaka kujiendeleza na elimu ya kidato cha tano na sita kisha chuo kwa utaratibu huu itakuaje? hiki ni kipimo kingine cha ukurupukaji wa Serikali ya awamu ya tano.
Kwakweli Baraza la Maaskofu mmeitendea haki taasisi yenu ya kitume katika nchi yenu, Mungu awabariki sana, hatutashangaa sana mkiitwa wachochezi lakini Mungu wetu atasimama upande wenu natunazidi kuwaombea pia.
Ukisikiliza kauli ya Mkuu wa jeshi la Polisi Dodoma, RPC Muroto kuwa watakao andamana watageuka vilema unapata jibu kuwa ni jeshi la Polisi lilimuua Aqwilina na nijeshi hilohilo ndio liliwavunja miguu kwa risasi wafuasi wa CHADEMA tarehe 15.
Hutuwezi kuishi katika jamii ya kutishiana maisha kila siku,Jeshi la polisi jirekebisheni kazi ya kutishia raia sio yenu kazi yenu nikulinda usalama wa raia toeni huduma kwa raia acheni ubabe usionatija, sasa mnajitofautishaje na majambazi. ??
Ubabe unaofanyiwa kijana Abdul Nondo,juhudi za ubabe huo zingefanywa katika mambo ya msingi tungekuwa mbali sana,Serikali inaelekeza nguvu kubwa sana katika mambo yasio na msingi hata kidigo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Serikali inapaswa kujitathmini katika,Sera ya elimu bure vinginevyo taifa litaendelea kuzalisha vijana wasioweza kushiundana katika soko la ajira, kila kukicha elimu yetu inazidi kudorora kwa kasi kubwa sana.