“Bawacha tunaitaka Mamlaka ya Dola kuhakikisha wanawake wote wanaoshikiliwa wanapatiwa haki ya kiwaona ndugu zao, Mawakili na kupatiwa huda za msingi za kibinadamu.” Mhe. Sharifa Suleiman, Mwenyekiti Bawacha Taifa
Jana nilipoona taarifa ya kufariki kwa Lucas Masawe niliumia sana.
Sijamfahamu Lucas kwa muda mrefu, na tulijuana humu humu X kwenye mijadala mbali mbali ambayo tulikuwa tunashiriki.
Siku pekee iliyonifanya nikamkubali zaidi ni ile siku ambayo alinitafuta DM "INSTAGRAM" kunishauri niongeze uchangamfu kwenye content zangu.
Hii ilikuwa January mwaka huu, yeye ni miongoni mwa watu wachache walioamini kwenye ninachofanya na akawa mtu wa kushauri ili niboreshe mbeleni nije kuwa mtu bora zaidi.
Mimi sio mtu wa kujibu na kusoma DM za watu wanaonitafuta, ila ya LUCAS nilifungua na tulichat kwenye maoni ambayo alitamani niyafanyie kazi.
Baada ya pale nilianza kubadilika na naamini nilivyokuwa nayafanya baadae pale instagram, facebook & tiktok huenda yeye mwenyewe ni shahidi kuwa NILIFANYIA KAZI ushauri wake kwa asilimia 200%.
Tunakuja duniani kuja kuacha IMPACT KWENYE MAISHA YA WATU WENGINE. Mimi kwenye maisha yangu Lucas kaacha hiyo impact itakayoishi miaka na miaka.
Pumzika kwa amani Lucas Masawe, kama kuna kesho nyingine kama tunavyoahidiwa kwenye Biblia basi naamini tutaonana tena sote njia ni moja wewe umetangulia tuu.
Familia yake pia Poleni, najua mnapitia kipindi kigumu kwa kijana kama Lucass kuondoka akiwa bado ana umri mdogo sana.
R.I.P BROTHER🕊
‼️JAJI NDUGURU HAKUAZIMISHWA, ALISHIRIKI KWA HIARI KUANDIKA HUKUMU‼️
Taarifa niliyopata ni kuwa Jaji Ndunguru alizunguka kuulizauliza kuhusu cognate offense (yaani kosa dogo) la uhaini. Aling’ang’ania kuwa South Africa treason yaani uhaini Ina makosa madogo. Kwa SA ni kweli kosa linaendana na sedition na incitement lakini aliambiwa na kila aliyemwuliza kuwa kwa Tanzania hakuna kitu kama hiki. Akagoma kusikiliza sasa KAUMBUKA! 🙄
Sasa shida yeye ni mwenyekiti wa jopo na shida kubwa kwa sasa Tanzania hamna dissenting opinion, la sivyo hivyo kuna jaji au majaji wangeweka hukumu tofauti. Na ndiyo maana hukumu zilikuwa mbili. Ile inayomwonyesha Ndunguru peke yake ilivuja kabla ya kupandishwa Tanzilii, ilikuwa ni ya mfumo wa ndani wa mahakama. Hiyo ndo ilikuwa nakala yake aliyotii maelekezo ya Abdul!
Ila uzuri Haki itashinda na washiriki wote wa dhulma watajulikana na kuwajibishwa!
#FreeTunduLissu
Kuna ajenda wanaleta CHAWA kuhusu yaliyotokea #MO29 wanadai waliochochea wananchi wanatakiwa kuchukuliwa hatua.
Kwa uelewa wangu mimi, waliowachochea wananchi ni hawa wafuatao;
1. Waliosema HAKUTAKUWA na Nywi nywi.
2. Waliosema WATATIKI huku wananchi wakidai TUME HURU YA KWELI YA UCHAGUZI.
3. Walioteka watu wote waliopinga UCHAGUZI kwa kudai uchaguzi sio huru na haki.
4. Waliofunga makanisa ya wachungaji wote waliohubiri HAKI ni bora kuliko AMANI.
5. Waliomfunga Jela LISSU wakijua wazi alichokuwa anadai LISSU ndio matakwa ya wananchi.
Ongeza mengine.
DPP Mwakitalu na mahakama ya Tanzania chini ya Jaji mkuu Masaju.
Mnafuta mfumo wa vyama vingi vya kisiasa Tanzania, kwa kutumia ofisi ya DPP na mahakama za Tanzania.
Mnawafungulia wapinzani wa kweli wa ccm na Samia, kesi za uongo za Ugaidi na uhaini na kuwafunga kwa hila.
Ni wajibu wetu Watanzania kukataa kurudishwa kwenye mfumo wa zidumu fikra za Mwenyekiti wa ccm.
Kikubwa zaidi historia itakuandika Mwakitalu na Masaju mnavyopaswa kuandikwa.
"Wanaokemea watu kuuawa wanawekwa ndani kama Lissu alivyowekwa ndani kwa uongo, mahakama ipo kwa sababu watu wanaamini kuna haki, siku watu wakiona hamna haki hakutakuwa na sababu ya kusoma sheria kwa sababu unakwenda wapi." Mhe. @HecheJohn
Tundu Lissu amepewa namba ya mfungwa ambayo ni 623.
Ukisoma Luka 6:23 inasema “Furahini siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.”
Kila kitu kinachotokea kwenye maisha ya Tundu Lissu ni kusudi la MUNGU tusihuzunike sana.
USHINDI UNAKUJA NA HAUPO MBALI.
GOOD MORNING.
REPOST 200
#FreeTunduLissu
Kutoka UKTANZANIA 🙏
Tuna wasiwasi mkubwa kufuatia kutiwa hatiani kwa kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Bw. Tundu Lissu, kwa mashtaka ya uchochezi.
Tunakumbusha matokeo ya Kikundi Kazi cha Umoja wa Mataifa kuhusu Kuzuiliwa kwa Watu Kiholela (maoni namba 74/2025), ambacho kilihitimisha kuwa kuzuiliwa kwa Bw. Lissu kulifanyika kiholela, hakukuwa na msingi wa kutosha wa kisheria, kuliambatana na wasiwasi mkubwa kuhusu haki ya kupata kesi ya haki, na kulikiuka ulinzi uliowekwa katika Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu pamoja na wajibu chini ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa, ambao Tanzania ni mwanachama wake.
Aidha, tunakumbusha wajibu wa Tanzania chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu, ikiwemo kulinda haki ya kupata kesi ya haki, uhuru wa kujieleza, ushiriki wa kisiasa, na kutendewa kwa usawa mbele ya sheria.
Tunaunga mkono mtazamo wa Tume ya Rais ya Uchunguzi kwamba maridhiano ya kisiasa ni hatua muhimu katika kuponya majeraha yaliyosababishwa na vurugu zilizotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, na katika kurejesha amani, kuaminiana, na mshikamano.
Tunatoa wito kwa mamlaka nchini Tanzania kuzingatia ahadi hii muhimu ya maridhiano, demokrasia ya vyama vingi, pamoja na kanuni za kesi ya haki, taratibu sahihi za kisheria, na utawala wa sheria.
KIRSTY MCNEILL
WAZIRI WA AFRIKA NA MAENDELEO YA KIMATAIFA.
Please see the Original in English.
👇👇👇
ZIARA YANGU LEO GEREZANI SEGEREA :
Nimepata nafasi leo ya kuwatembelea wateja wangu wanaoshikiliwa Gereza la Mahabusu Segerea kwa makosa ya Uhaini na Ugaidi. Wako salama na afya zao ni njema . Wateja hao ni viongozi na wanachama wa CHADEMA ambao walikamatwa maeneo mbalimbali na kuishia kushitakiwa kwa makosa hayo, orodha ya watuhumiwa ni kama ifuatavyo:
Mosi, Mwalimu John Justine Pambalu, Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mafunzo CHADEMA aliyekamatwa Arusha na kusafirishwa hadi Dar, na baada ya siku kadhaa akashirakiwa Mahakamani kwa kosa la Uhaini.
Pili, Coletha Clavery Ntidyicha, mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Kigoma, ambaye alikamatwa kwa Azizi Ali Dsm , akashikiliwa kwa week kadhaa na akaletwa mahakamani baada ya amri ya Mahakama, yeye akashitakiwa kwa kosa la Ugaidi.
Tatu, ni Athumani Abdallah Mganda, huyu ni mjumbe wa kamati Tendaji ya Jimbo la Urambo, tangu mwezi wa 7 leo amefikisha siku 104 Gerezani tangu kukamatwa kwao.
Nne, Hamad Athuman Hassan aliyekamatwa tarehe 8/7/2026 kazini kwake, akashikiliwa kituo cha Polisi Msimbazi na baadaye central kabla ya kupewa dhamana na kushikiliwa tena kisha kupewa kosa la Ugaidi.
Tano, Ally Abdallah Mrisho, yeye alikamatwa tarehe 08/06/2026 kosa lake lilikuwa kusambaza kipeperushi chenye maneno ya katiba mpya , alishikiliwa kwa week mbili kabla ya kuachiwa na kushikiliwa tena kwa week mbili na baadaye kushitakiwa kwa kosa la ugaidi pale Kinondoni.
Sita; Jenifrida Petro Mtuka - huyu alikamatwa tangu mwezi wa saba na ameshitakiwa kwa muda mrefu sana. Anashitakiwa kwa kosa la ugaidi pia.
Saba, Upendo kileo - huyu naye alikamatwa mapema zaidi naye anasiku takribani siku 100+,
Pamoja na hawa watu 7 kuna watu wengine 2 wako mahabusu ambao walishitakiwa kwa makosa ya ugaidi nao ni Dastan Mhiku huyu nimeambiwa ni mwandishi wa habari na Mashaka Nestory Mkindikwa ambaye anashitakiwa Kibaha.
Tumeonewa na kufanyiwa ukatili mkubwa na viongozi wa CCM na serikali ya CCM kwa muda mrefu sana……..
It’s time for a new Tanzania to be born……..
Tupambane…..:::