🚨 𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆:
Bernard Morrison will leave Yanga SC and won’t be part of the squad next season.
Morrison’s contract ended and won’t be extended.
He is a free agent now. 🇬🇭
#Transfers#TimuYaWananchi
Ni vibe la hela yote, ni shangwe za volume yote, ni cheers za glasi zote kwa Mashabiki, Wafuasi na Wa-Cloudsnia wote ndani na nje ya Tanzania leo baada ya Mfalme wa show za mchana Mtangazaji Hamisi Mandi maarufu kama B Dozen, B12, B Twangala kutangaza kurejea rasmi Clouds Media Group baada ya kuwa nje kwa miaka mitatu.
Clouds Media Group imethibitisha taarifa za kurejea kwa kiungo huyu muhimu na Mkongwe ambaye kipaji chake, ubunifu wake na umahiri wake vina mchango mkubwa sana kwenye media hii na sasa ni rasmi anarudi kuanzia alipoishia kwenye show yake ya siku zote ya XXL kuanzia Jumatatu May 26 2023.
Mkali huyu ambaye mwezi huu wa June anatimiza miaka 20 toka aanze kufanya kazi ya utangazaji kwenye Radio, aliondoka Clouds FM tarehe 31 May 2020 na kujiunga na EFM kabla ya kurejea rasmi hii leo ikiwa ni miaka mitatu baadaye.
B Twangala alianzia kutangaza Redioni CloudFM Arusha mwaka 2003 akiwa Mwanafunzi wa Sekondari Arusha Sec. huku akifanya kipindi cha DR. BEAT ( saa nane mchana hadi saa kumi) na ni miongoni mwa Waasisi wa show ya XXL ambayo ilianzishwa mwaka 2007 (saa 7 hadi 10 jioni).
Umahiri wa @BDozen haupo tu kwenye Radio bali hata nje ya Radio ambako ameshiriki ku-host Matamasha mbalimbali ya FIESTA ambako Mastaa wa muziki duniani kama Jay Z, Busta Rymes, Fat Joe, 50 Cent, Ja Rule, Eve, Ludacris na wengine wali-perform. #MillardAyoUPDATES #IkumbatieCLOUDS