Uhusiano wa kudumu haujengwi na mvuto wa mapenzi na tamaa ya ngono. Mvuto wa mapenzi, pamoja na utamu wake, haudumu. Ukitegemea mvuto wa mapenzi kushikilia uhusiano, hutofika mbali na mtu —maana nguzo kuu ya uhusiano ni ile imani kuwa unamfahamu vizuri uliyenaye, unamuamini, na kwamba uko tayari kuwekeza kwenye uhusiano huo. Hivi viwili vina gharama na vinahitaji muda.
Ukiweza kudhibiti kidogo ‘hisia’ za pale mwanzo mapenzi yanapoanza, ukajipa kidogo muda wa kumfahamu mtu (intimacy), kujua anaamini nini, anayatazamaje maisha, unapunguza uwezekano maumivu mengi ya kushtukiza na kwa kufanya hivyo, unaongeza uwezekano wa uhusiano wenu kudumu (commitment).
Ukiangalia mchoro huu wa nadharia ya mapenzi ya mshunuzi Steinberg unaona hatari ya kuwekeza kwenye mvuto wa mapenzi usioenda sambamba na kufahamiana. Ghafla, Steinberg anasema, haidumu. Utajifunza staili zote za ngono lakini bila kuwekeza kwenye kuunganisha fikra na mtazamo wenu, ni suala la muda tu ‘grafu’ itawarudusha panapostahili.
Come and visit London’s Home of Trophies. 🏆
Book your Stadium Tour at Stamford Bridge now. ⭐️⭐Come and visit London’s Home of Trophies. 🏆
Book your Stadium Tour at Stamford Bridge now. ⭐️⭐Come and visit London’s Home of Trophies. 🏆
Book your Stadium Tour at Stamford Bridge now. ⭐️⭐Come and visit London’s Home of Trophies. 🏆
Book your Stadium Tour at Stamford Bridge now. ⭐️⭐Come and visit London’s Home of Trophies. 🏆
Book your Stadium Tour at Stamford Bridge now. ⭐️⭐Come and visit London’s Home of Trophies. 🏆
Book your Stadium Tour at Stamford Bridge now. ⭐️⭐️
Umewahi kuwaza uweza kuongea na mtu msiyewasiliana kabisa? Kwamba unaongea na mtu na anamua kukuacha umalize akaendelee na shughuli zake? Wengine, kwa tabia zako, huacha kabisa kujadiliana lolote na wewe.
Mawasiliano ni zaidi ya maneno. Kisichosemwa kinachukua kati ya asimilia 70 - 80 ya mawasiliano pekee. Hata kwa yale tunayoyasema, asilimia kubwa inabaki kwenye namna tunavyosema kuliko tunachosema. Katika hiyo ‘namna unavyosema’ pana kitu kinaitwa heshima kwa utu wa mtu. Huwezi kuwasiliana na mtu usiyeamini anastahili heshima.
Ukishaamini mtu hajui kama wewe, hana uelewa wala uzoefu kama wewe, tayari unajenga ukuta unaoharibu mawasiliano na inakuwa vigumu kuelewana. Hapa nakuletea baadhi ya tabia zinazoharibu mawasiliano:
1️⃣ Kukosa usikivu
Unazungumza na mtu na huonekani kuwa naye kiakili na kihisia. Upo lakini haupo hata kama husemi. Unapapasa simu, unapepesa macho kuwaangalia wanaopita au kuendelea na shughuli nyingine. Watu hujua huwasikilizi hata kama hawana ujasiri wa kukuambia.
2️⃣ Kujikweza
Mwenzako anakusimulia jambo lake, lakini kwa kufikiri una uzoefu zaidi na ‘uelewa mpana’, unaleta simulizi lako linalowaondoa kwenye jambo lake. “Hilo mbona dogo sana? Sikiliza kilichonitokea mimi uone.” Watu huwa wanajua ukifikiri chako ndicho kinachostahili muda zaidi.
3️⃣ Kushauri
Saa nyingine hata hujaombwa maoni, unadakia juu juu jambo la mtu na maelezo ya nini kifanyike au swali lenye ushauri, “Nadhani hapa ukafanye…” “Kwa nini hukufanya…” “Ulikuwa unafikiri nini kufanya hiki ulichofanya…”
Ushauri unakera ukitokewa bila kusikiliza.
4️⃣ Kufariji kwa kupuuza hisia
Mtu tayari ana hisia hata ukimwelekeza kuzipuuza bado anazo. Mwenzio amekuambia anaogopa, Unakuja na faraja, “Usiogope. Usijisikie vibaya. Jikaze kiume.” Tunahitaji faraja lakini zisizopuuza hisia za mtu. Faraja unayopuuza hisia hubeba ujumbe hasi.
5️⃣ Huruma inayotia unyonge
Huruma sawa lakini ndio umhurumie mtu mpaka ajione anakaribia kufa? “Masikini pole jamani. Dunia kweli haina huruma kweli. Keshakuharibia maisha hapo.”
“Halikuwa kosa lako kabisa. Sema mtu mwenyewe ndio kawa shetani kabisa.” Huruma isipofikiriwa vizuri hutia unyonge.
6️⃣ Kuelimisha
Unataka kuonekana unajua, una uzoefu na mwenye shida hana uelewa: “Mungu anajua kwa nini unapitia hili.” “Mungu amemchukua marehemu kwa wakati wake.” Kujipa kazi ya ualimu kwa tatizo la mtu ni kiburi. Kuna wakati mtu anahitaji kusikilizwa tu sio kupewa elimu.
7️⃣ Maswali mengi
Unauliza maswali yanayochonoa jambo mtu hajawa tayari kukuambia. “Unaendeleaje na masimango ya wakwe?” “Hebu niambie huyu ni mwanaume wa ngapi kukuacha?” “Ulijisikiaje alipokuwa anakulazimisha?” Magonjwa yetu mengi na ugomvi mwingi unaotusumbua ni kilio cha nafsi iliyokosa mtu wa kuisilikiza na kujaribu kuielewa. Ukiweza kumsikiliza mtu, ukajali anachokisema, unatibu mengi yanayowazuia kuzungumza.
✳️ Kufanyia kazi unachojifunza
Kuna vitu tunafanya saa nyingine bila kujua lakini vinaathari pakubwa namna tunavyosikika kwa watu tunaotaka kuwasiliana nao. Mawasiliano huanza na heshima. Ukimheshimu mtu, akili yako ‘inajiset’—unamsikiliza, huingilii anachosema, humalizii sentensi zake, hukimbilii kumwelekeza cha kufanya, unaheshimu hisia zake, humtii unyonge kwa taarifa asizozihitaji wala maswali yanayochokonoa usichoaminiwa kuambiwa.
Ukiwa bado unaogopa mwambie.
Ukiwa bado unaogopa omba.
Ukiwa bado unaogopa sema.
Ukiwa bado unaogopa omba msamaha.
Ukiwa bado unaogopa mkubalie.
Ukiwa bado unaogopa nenda.
Ukiwa bado unaogopa anza.
Ukiwa bado unaogopa andika.
Ukiwa bado unaogopa fanya.
Ukiwa bado unaogopa kamilisha.
Ukisubiri hofu iondoke umeshachelewa.
Ogopa ukiwa unafanya unachoogopa.
Mwaka huu 2026 kutakuwa na kupatwa kwa jua na mwezi kipekee
Itaanza kupatwa kwa jua kwa "mduara wa moto" tarehe Februari 17, 2026, na kufuatiwa na "mwezi wa damu" yaani bliid moon nyingine Machi 3, 2026, na kumalizika na "kupatwa kwa jua ya karne" mnamo Agosti 12, 2026.
Mnaobisha kuwa haya matukio hayana effect kwa binadamu nadhani mmeona blood moon ilichofanya mwaka jana!
Unatumia muda mrefu kutafuta mali. Unaishi maisha ya hila na ulaghai. Unakuwa mtu wa dili muda wote, uhusiano wowote usioambatana na dili unaona ni kupoteza muda. Kwa vile ulivyojaza ufahamu wako na vitu, unaona hata familia na ndugu zako ni wasumbufu. Unaishia kuwa mtu mbinafsi unayetazama maisha kwa mtazamo finyu wa vitu. Huna muda na yeyote asiye na ‘chochote cha ku-offer’. Muda wote anawaza namna kupata zaidi, kuumiza zaidi, hila zaidi, kujishibisha zaidi.
Unawatazama watu kama nyenzo ya kufikia malengo yako. Unawaona watu kama vitu unavyoweza kuvizimisha na vikanyamaza. Unadharau hisia za kila anayekuzunguka. Unaumiza watu wengi wanaonekana kuwa kikwazo cha ukusanyaji wa mali ambazo hata huzihitaji na utukufu unaokutenga na watu. Unaishia kuwa mpweke aliyefanikiwa kuwa na kila kitu. Unakufa na umaarufu usiokupa amani wala utoshelevu.
Mzee Mwinyi alituasa, maisha ni kuacha simulizi jema kwa wengine. Hili haliwezekani ukiyatazama maisha kama mradi wa kujikusanyia vitu, nguvu na utukufu. Maisha ni zaidi ya vitu. Maisha ni zaidi ya madaraka. Maisha ni zaidi ya kujikusanyia mali kwa ajili ya ndugu, jamaa na marafiki. Maisha ni zaidi ya kupambana na hofu zako. Maisha ni zaidi ya kulinda kiburi chako. Maisha ni pamoja na kuwa furaha kwa jirani yako. Maisha ni kuwa jibu la matatizo ya wanyonge wanaokuzunguka. Maisha ni kutumia uwezo wako, vipawa vyako, elimu yako, ushawishi wako kuwa mchango katika ustawi wa jamii katika upana wake.
@bwaya Brother mshunuzi @bwaya .
Leo roho ananieleza nirejee kusoma sana lectures zako za EDU psychology, tafadhal iponye nafsi yangu boss.
Kwa link au files please nitashukuru sana.
#Remainhumble.