MREJESHO WA UFUATILIAJI:
Salaam. Nimefuatilia na kuwasiliana na mtoa taarifa kisha uongozi wa mkoa wa Dodoma na Morogoro ambao, wote wameshirikiana vema na kusimamisha gari hilo Gairo na kumbaini Binti huyo kama ilivyoripotiwa. Aidha, msichana huyu yuko na ndugu yake na wanaelekea morogoro kwenye matibabu. Taarifa zaidi zitatolewa na mamlaka ya morogoro muda si mrefu. Ahsanteni Sana kwa ushirikiano wenu. 🙏🏽
@TimesMajira Waziri hajawahi kukoshwa na matamasha ya Utamaduni. Sijawahi sikia mfano akikoshwa na Tamasha la #SanjoYaBusiya ambalo mwaka huu limefanyika kwa mara ya 14 na wananchi zaidi ya 50,000 kuzuru tukio hili ambalo huanza tarehe 1-7 Julai kila mwaka.
Katika kudumisha ujirani mwema na Shule ya Msingi, Ibeshi iliyoko Gedeli, Mkurugenzi wa @adlgtz Ndugu @kazikwanza amekabidhi ngoma zitakazitumika kwenye bendi na shughuli za sanaa hapo shuleni.
Karibuni tena majirani zetu.
Kwa anayevutiwa, anaweza kufika kwenye Uwanja wenye ngome hapa Bujora na kushuhudia sherehe hizi za #Bulabo zinazoendelea wiki nzima ambapo siku ya kilele Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh @SuluhuSamia
Tokwile Basiya!
Busiya katika Ushiriki wetu kwenye #Bulabo tumepeleka ngoma tatu:
Beni, Badimi na Bazoli.
Wameambatana pia Kinamama nane watakaofanya maonyesho ya Vyakula asili; na Mganga wa tiba asili.
Katika Tamasha la Bulabo linalofanyika hapa #Bujora Mwanza kila
mwaka, Serikali kwa mwaka huu imeshiriki maandalizi na kutualika Utemi wa Busiya kama ilivyo kwa temi zingine ndani ya Kanda ya Ziwa Victoria. #Bulabo cc @nickluhende
Asante Mh. Mndeme kwa kutambua umuhimu wa mila na desturi zetu na hata kushiriki Tamasha letu la #SanjoYaBusiya#77Fest mwaka jana 2023.
Tunakutakia kila la kheri na karibu tena katika Tamasha letu la kila mwaka.
Kabla ya Ukoloni,
Kabla ya mgawanyo wa kiserikali, waafrika tulikuwa na maeneo na mipaka yetu kwa kuzingatia uongozi wa jadi uliokuwepo.
Temi (falme) za kisukuma zilikuwepo zaidi ya 50. Ingia hapa upate dondoo.
https://t.co/FJnsrs7cPv