Shukrani kwa Wanachama na Mashabiki wetu kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wetu wa kariakoo derby jana. Tutarudi tukiwa imara zaidi๐ฐ๐ช๐ฝ
#TimuYaWananchi#DaimaMbeleNyumaMwiko
VIDEO:
Wakili Sweetbert Nkuba ameeleza kuwa kudai Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 si ya haki ni upotoshaji, kwani Katiba hiyo ndiyo msingi mkuu wa sheria zote nchini na imeweka misingi thabiti ya utawala wa sheria na haki za msingi za raia.
Wakili Nkuba ameyasema hayo leo Jumamosi, tarehe 10 Oktoba 2026, wakati akichangia katika mjadala wa Utawala wa Sheria kwenye kipindi cha Medani Kuu kinachorushwa na kituo cha Star TV chini ya mtangazaji Edwin Odemba (Chief Odemba).
Akijibu hoja za wanaodai kuwa Katiba ya sasa haina haki na ni katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wakili Nkuba amebainisha kuwa Ibara ya 13 ya Katiba ndiyo inayotoa msingi wa utawala wa sheria kwa kuhakikisha usawa mbele ya sheria, uhuru wa mtu, na haki ya kutohukumiwa kabla ya mahakama yenye mamlaka kujiridhisha.
Wakili Nkuba amekiri kuwa Katiba hiyo ilitungwa wakati nchi ikiwa chini ya mfumo wa chama kimoja ili kuendana na mazingira ya wakati huo, lakini alisisitiza kuwa hilo halifanyi Katiba hiyo kuitwa ya CCM au kukosa haki. Hata hivyo, amekiri kuwa kuna hoja ya msingi ya kuwa na Katiba mpya kutokana na Katiba ya sasa kudumu kwa muda mrefu.