ASANTENI WATANZANIA!
TUMEFIKISHA TSH. MILIONI 50 ✌️
Ndani ya saa 96 sawa na siku 4.
Asanteni kwa mwitikio wenu mkubwa. Mpaka sasa, tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 50 katika Marathon ya kufikia TSh. Milioni 334 kwa ajili ya kufanikisha Baraza Kuu la Umma.
Huu ni ushahidi kwamba Watanzania wanaweza. Safari inaendelea. Kila mchango una thamani. Tuendelee kuchangia hadi tufikie lengo letu la TSh. Milioni 334.
✌️ @Sativa255
Huu ni mfano wa kile kinacholikuta lile genge haramu lililokula fedha chafu ili limchafue Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe John Heche!
Ni suala la muda tu watatema bungo!
ASANTENI WATANZANIA! MPAKA JIONI HII TUMEFIKISHA TSH. MILIONI 40 ✌️
Tunawashukuru kwa dhati Watanzania, wanachama, wapenzi na marafiki wa CHADEMA kwa mwitikio wenu mkubwa katika Marathon ya kufikia TSh. Milioni 334.
Mpaka jioni hii, tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 40, hatua muhimu inayotupeleka karibu zaidi na lengo letu la kufanikisha Baraza Kuu la Umma.
Mafanikio haya ni ushahidi kwamba nguvu ya umoja na mshikamano wa Watanzania inaweza kutimiza malengo makubwa. Kila mchango unaotolewa ni sehemu ya kujenga CHADEMA imara na kuwezesha Baraza Kuu la Umma kufanyika kwa mafanikio.
Safari bado inaendelea. Tunaendelea kuwaalika Watanzania wote wenye imani na matumaini makubwa kwa CHADEMA kuendelea kuchangia kwa kadri ya uwezo wao na kuwahamasisha wengine kushiriki.
Asanteni kwa kuendelea kuandika historia pamoja nasi. Tuendelee kuchangia hadi tufikie lengo la TSh. Milioni 334. ✌️
"Chadema Kanda ya Kati ina taarifa na ushahidi wa awali unaojumuisha vielelezo vya picha, Video na mawasiliano ambayo ni sambamba na miamala iliyotumwa kutoka kwa hao wanachama wa Chama cha Kikaragosi kwenda kwa wanachama wa Chadema. Wapo wanachadema wengi ambao wamepokea fedha na ushahidi huo tutauweka hewani lakini kwasasa tumekabidhi vielelezo kwa mwanasheria Mkuu wa Chama ili waweze kupitia kwaajili ya hatua nyingine za kisheria. Tuna mawasiliano ya namba zinazotumima kuwapigia Viongozi wa Majimbo, wengine wamepokea fedha na hawajapokea wito."-Katibu wa Chadema Kanda ya Kati Bi. Ashura Masoud.
ASANTENI WATANZANIA!
MPAKA ASUBUHI YA LEO TUMEFIKISHA TSH. MILIONI 42.5 ✌️
Tunawashukuru kwa dhati Watanzania, wanachama, wapenzi na marafiki wa CHADEMA kwa kuendelea kuitikia wito wa kuchangia Marathon ya kufikia TSh. Milioni 334.
Mpaka asubuhi ya leo, tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 42.5, hatua nyingine muhimu katika safari ya kufanikisha Baraza Kuu la Umma litakalofanyika Septemba 15, 2026.
Kila mchango unaotolewa ni ishara ya imani, mshikamano na dhamira ya kuendelea kuijenga CHADEMA. Tunaendelea kuwahimiza Watanzania wote kuungana nasi kwa kuchangia na kuwahamasisha wengine kufanya hivyo.
Safari bado inaendelea. Zimebaki siku 61 pekee. Kwa pamoja tutafikia lengo la TSh. Milioni 334 na kufanikisha Baraza Kuu la Umma.
@assengajrr Ukisikiliza hotuba zote vizuri bila chembe ya chuki wala hasira utatambua @ChademaTZ2 wana strategy nzuri ya ku-implement hizo action unazozitaka, things don't just pop out of the blue. For starters hata hili linalomfanya msajili atake kukifuta chama ni way forward. Usipanic!
Vita ya mashariki ya kati haiwezi kuwa kisingizio cha mafuta kupanda bei.
Tunajua mmeagizwa na aliewateua kusema vita vita vita.
Kwenye kila lita moja ya mafuta kuna kodi na tozo mbali mbali za serikali zinazofikia 16.
Ukiondoa hizo tozo hata nusu bado mafuta yatabaki sh 2,700 na hii itamsaidia Mwananchi kupumua..
Hizi kodi na tozo zote zinakusanywa na kuibiwa kama vile ni kawaida tu..
Baadae wanasema Mwizi asemwe hadharani ili aone aibu !!! Hakuna hatua za kuchukua!
Kiongozi wa Kijeshi wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traore, amewataka Wananchi wa Taifa hilo la Afrika Magharibi kuacha kabisa kufikiria kuhusu demokrasia na kusisitiza kuwa mfumo huo hauendani na mahitaji ya Nchi yao kwa sasa.
Traore ameitoa kauli hiyo wakati wa mahojiano yaliyorushwa na Televisheni ya Taifa, RTB ambapo alieleza kuwa msingi wa demokrasia haukujengwa kwa ajili ya mazingira ya Burkina Faso na kwamba msimamo wake kwa sasa ni kuwa Taifa hilo linapaswa kuzingatia mbinu mbadala za Uongozi zitakazoweka mbele usalama na utulivu wa Nchi badala ya mifumo ya kisiasa ya Magharibi.
Serikali ya Burkina Faso ambayo ilianza kuongozwa na Kapteni Traore baada ya mapinduzi ya kijeshi baada ya kuipindua Serikali nyingine ya Kijeshi Septemba 2022, mwaka jana 2025 ilitangaza kuvunja Tume ya Uchaguzi huku pia February 2026 Bunge la Nchi hiyo linaloongozwa na Wanajeshi likipiga marufuku Vyama vyote vya siasa.
#MillardAyoUPDATES
( via @DWkiswahili )
Napenda kuchukua nafasi hii, Kumshukuru sana kaka yangu Bwege…. Pamoja na hali yake, hali ya usafiri wa Dar … Amejitoa na kuja mahakamani kusikiliza na kumpa nguvu Mwenyekiti wetu .. Tundu Lissu katika kesi yake uongo ya uhaini..
Mwenyezi Mungu aendelee kukulinda kaka Bwege akupe afya njema na maisha marefu.
Tutashinda.