“Baada ya Magufuli kufariki na Samia kuingia madarakani, nilikuwa uhamishoni. Nikaja kukoswa koswa hapa nikakimbilia ubalozi wa Uneeumani, ikabidi niondoke, nikimbie kidogo. 17 Februari 2022 Rais Samia alifanya ziara Ulaya. Kulikuwa na mkutano wa AU - EU SUMMIT. Akanitumia ujumbe kupitia watu wake. Watu wanasema niliomba, hapana, sikuomba tuonane. Yeye ndiye aliomba tuonane. Wakati huo mwenyekiti Freeman Mbowe yupo gerezani miezi 7. Nikawapigia simu viongozi wenzangu tukashauriana na nikaona ni jambo zuri. Tukaenda tukaonana na akasema anataka amalize matatizo aliyoanzisha mtangulizi wake. Nikamwambia anza na Mlmwenyekiti wetu ambaye yupo gerezani kwanza kwa kesi za uongo za akina Kingai. Pia tuzungumze habari ya katiba mpya na ya tume huru ya uchaguzi. Mwisho nikamwambia kuwa mimi na Lema na Wenje tumekimbia nchi kwa usalama wetu. Naomba utangaze kama tutakuwa salama tukirejea. Akatangaza Hamad Masauni bungeni. Tukarejea. Baadae akamuachilia mwenyekiyi Freeman Mbowe ndiyo tukapata faraja mimi na wenzangu kurudi” - Tundu A.M Lissu, Mahakama Kuu, 26.08.2026
Mahakama ya Uganda imetumika kuwatesa wapinzani wa dikteta Museven kwa kuwanyima dhamana, matibabu, na fair trial. Samia ameomba Jaji kutoka mahakama hiyo aje amchunguze kwa mauwaji aliyofanya Oktoba 29. Kwanini Samia anadhani Watanzania wote wana elimu kadha wa kadha kama yeye?
Mnatesa watu wengine kwa kuwaweka gerezani kwa mashtaka ya uongo na kughushi, kuwateka na kuwapoteza. Mnatembea VX.R V8 full kipupwe, lakini mkishtuka moyo kidogo tu, mnadedi papo kwa papo kama mshumaa. Hivi ninyi mngeliweza kuishi gerezani siku 350 kwa kusingiziwa? Takbīr.
Wewe ni rais. Unakerwa na mtoto wa miaka 20, Shadrack Chaula, aliyechora picha inayofanana na sura yako akaichoma. Unaagiza atekwe, ateswe, auwawe.
What kind of a dubious human are you?
Enough is enough!!
CHADEMA kanda ya Pwani yaadhimisha miaka 33 ya kuzaliwa CHADEMA kwa kujenga ofisi na kugawa samani za ofisi (furniture).
Ofisi ya CHADEMA Kanda ya Pwani, kuelekea kilele cha wiki ya maadhimisho ya miaka 33 ya kuanzishwa kwa chama, Januari 19, 2025 Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani, Mh. Boniface Jacob pamoja na Viongozi wengine wa Kanda wamefanya ziara ya kutembelea ujenzi wa ofisi za chama kwa ngazi ya mikoa na wilaya.
Mh. Boniface Jacob amekabidhi vifaa ya ujenzi vyenye samani ya kiasi cha Tsh. 1,000,000/- kwa ajili ya kukamilisha kiasi cha Tsh. 10,000,000/- ambayo ametumia hadi sasa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ofisi za chama, mkoa wa Pwani kwa awamu ya kwanza.
Aidha, Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Pwani, Mh. Boniface Jacob amekabidhi samani za ofisi (furniture) katika ofisi za CHADEMA wilaya ya Ubungo ambazo thamani yake ni kiasi cha fedha Tsh. 3 Milioni.
Hatua hii ni sehemu ya uwajibikaji wa viongozi wa chama kanda ya Pwani kuhakikisha kila wilaya inakua na ofisi za kisasa zenye hadhi kama sehemu ya kuenzi na kulinda misingi ya chama iliyoanzishwa na waasisi wetu wa chama.
Imetolewa leo January 20,2025
Ntele Benjamin
Katibu wa Kanda ya Pwani.
Tundu A.M Lissu alichaguliwa na mkutano mkuu wa CHADEMA. Hakuna kiumbe mwingine yeyote anaweza kumuondoa zaidi ya mkutano mkuu wa chama Taifa ambao ulimchagua. Hizo porojo nyingine za mazombi ya mbogamboga ni za wapumbavu waliolewa visungura tu na hawaelewi katiba ya CHADEMA.
Mimi na mshirika wangu Bob Wangwe tumeishitaki Tanzania katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) kufuatia vurugu na dosari ktk ‘uchaguzi’ wa Oktoba 2025.
Tunaamini TZ ilikiuka Makataba wa EAC, na tunaomba EACJ iingilie kati kutoa nafuu tulizoomba, ikiwemo uchaguzi kurudiwa.
Delivering powerful messages that touch on everyday struggles, personal growth, and staying authentic in the face of fame and pressure isn’t for everyone. Kodi yangu asipewe mchezaji, pelekeni hizo pesa zikahudumie wananchi, kuna mashida kibao kwa raia. S/o to my nigga #AdamMchomvu . 👊🏾
HAWA NDUGU ZETU WANAHITAJI MSAADA WETU ILI WAWEZE KUPATA MATIBABU.
Hawa mnaowaona hapa ni Watanzania wenzetu ambao wamepata madhira mbalimbali.
Picha ya Kwanza anaitwa Kuringe Sawere huyu alitekwa na Maofisa wa Polisi Disemba 4, 2025 baada ya wiki mbili kupita kuna msamalia mwema alitujulisha kwamba Kuringe kafichwa kituo cha Polisi Chang’ombe Dar es salaam lakin alikuwa ameteswa sana kiasi kwamba alikuwa anatembelea tumbo maana alipigwa sana maeneo ya kwenye nyayo, magoti na mgongo.
Disemba 22 aliachiwa kwa dhamana ya Polisi lakin hali yake kiafya sio nzuri bado anapata maumivu makali ya miguu na mgogo hivyo anahitaji kufanya vipimo ili aweze kupata tiba.
Picha namba 2 ni Musa Ndile huyu alitekwa November 27, 2025 na maofisa wa Jeshi la Polisi, walimpiga sana na kumuumiza miguu yote miwili, Disemba 17 aliachiwa kwa dhamana lakin bado hawezi kutembea vizuri, anachechemea hivyo anahitaji matibabu zaidi ili aweze kuwa sawa.
Picha no. 3 ni Alex Mutembei yeye alipigwa risasi ya kwenye paja Oktoba 29 lakin mpaka Leo hawezi kunyoosha mguu wake lakin pia mguu huo umeanza kuwa mwembamba hivyo anahitaji matibabu zaidi.
Picha namba 4 anaitwa Martin Elia huyu alipigwa risasi Oktoba 29 hali ya mguu wake inazidi kuwa mbaya kwasababu anajiuguzia nyumbani, anahitaji msaada ili aweze kupelekwa Hospital kwa ajili ya matibabu ili aweze kupona.
Hivyo basi tunaomba mchango wako kiasi chochote ulichojaliwa na Mungu ili tuweze kuokoa maisha ya hawa ndugu zetu
Michango itumwe kwenye namba
Mpesa: 0744719187
Jina: Musa Ndile
Nani anaweza kusema huu ni uongo…
Bunge la hovyo lisiloweza kusimamia serikali..
Tulia na bunge lake waliogopa kujadili hata suala la utekaji, kama hauwezi kujadili jambo hilo la wananchi upo kwaajili ya nani?
Kuna sababu gani ya kuwa na muhimili unaitwa bunge kama hausaidii wananchi?
Bado Tulia na kujipendekeza kote!!!!
Ukimsikiliza Mwigulu na ccm wenzake wanazungumza… utafikiri Nchi hii ni mali yao binafsi na sisi wengine wote ni wapangaji!!
Unawezaje kuiba uchaguzi, ukajitangaza kwa nguvu, ukaua maelfu ya watu na wengine ukawafanya walemavu ili uwe kiongozi usie na ridhaa wala kura za umma.
Alafu unapata ujasiri wa kukemea wale wanaokwambia umeiba, wale wanaotaka uchaguzi uwe huru na haki, wale wanaotaka Mwananchi ndie awe na sauti ya kuweka kiongozi anaemtaka.
Tena unamwambia analeta vurugu na kuchafua Nchi…
Hivi alieiba uchaguzi na kuua watu na yule anaesema utaratibu ufuatwe nani analeta vurugu? Nani anatumika kuchafua Nchi?
Mwigulu Nchi hii sio mali yenu binafsi, wananchi wana haki na mamlaka yote na Nchi yao..
Acheni kutishia wananchi.