Kesho tarehe 16 Desemba 2024 Katibu Mkuu wa Chama Mhe. @jjmnyika atazungumza na watanzania kupitia mkutano na Waandishi wa Habari utakaofanyika saa tano asubuhi Makao Makuu ya Chama Mikocheni Dar Es Salaam.
Waandishi wote wa habari mnakaribishwa.
Mwenyekiti wa CHADEMA @freemanmbowetz na Makamu Mwenyekiti @TunduALissu wakisalimiana leo kabla ya kuanza kwa kikao chama Kamati Kuu ya CHADEMA ambayo pamoja masuala mengine, itaketi na kusaili wagombea wa nafasi mbalimbali katika Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Kati.
Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. @TunduALissu atazungumza na watanzania kupitia mkutano na waandishi wa habari leo Jumatano tarehe 25 Septemba 2024, saa kumi na nusu jioni, Makao Makuu ya Chadema, Mikocheni Dar es salaam. Vyombo vyote vya habari vinakaribishwa.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesema maandamano waliyopanga kufanya kesho Septemba 23, 2024 yatakuwepo kama ilivyopangwa huku ikisisitiza kuwa yatakuwa ya amani na maombolezo ya viongozi wao waliotoweka na kuuawa.
Vijana wa kike na kinamama wajitokeza kwa wingi katika mkutano wa Mlola, Tanga, ambapo mkutano huo ulihutubiwa na mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. @freemanmbowetz na Mwenyekiti wa Kanda Mhe. @godbless_lema.
#UshindiUnakuja
Kamanda @HecheJohn mjumbe wa kamati kuu ya @ChademaTz Akiendelea na ziara yake kanda ya serengeti Jimbo la tarime vijijini kijiji cha Borega kata ya Ganyange.