Chaos inside the Senegalese parliament after the controversial constitutional reform bill was voted in and contested by the supporters of President Bassirou Diomaye Faye in the assembly.
The reform bill reduces president's powers and strengthen parliamentary control over national budget and improve accountability.
The most fascinating part of the bill is that now Senegalese senior officials including the president have to declare their assets before taking the office and after leaving the office.
Guess who is behind the architect? The former prime minister Ousmane Sonko who is now the president of national assembly/parliament.
Kanisa Katoliki Nchini Kenya walipopewa Mamilioni ya fedha na Raisi Ruto Maaskofu walihoji fedha hizo amezitoa wapi na alivyoshindwa kuelezea alipozitoa Maaskofu waliamuru arudishiwe fedha zake wakaziita kuwa ni fedha chafu za wizi na jasho la Wakenya.
KKKT chini ya Askofu Malasusa wamekubali kuwa jukwaa la siasa chafu za Samia kwa kuhongwa Mamilioni ya fedha zisizojulikana zimetoka kwenye bajeti ipi. Waumini wa KKKT mnawajibu wa kuhoji na kupinga kanisa lenu kutumika na hawa wanasiasa.
Kataeni fedha za hizi, Ni fedha chafu, Ni fedha zilizolowa damu za Watoto wa Tanganyika zilizomwaga Oktoba 29.
TUNDU LISSU KUMUHOJI MKUU WA GEREZA LA UKONGA NA KAMISHNA MKUU WA MAGEREZA KATIKA SHAURI LA KIKATIBA NAMBA 7300/2026
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Mhe. Tundu Lissu, atawahoji kwa maswali ya dodoso Kamishna Mkuu wa Magereza pamoja na Mkuu wa Gereza la Ukonga tarehe 1 hadi 3 Julai 2026 katika Shauri la Kikatiba Na. 7300 la Mwaka 2026 mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma.
Shauri hilo lilifunguliwa na Mawakili Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu na Paul Kisabo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Mkuu wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ukonga.
Katika shauri hilo, Mahakama inaombwa kuamua kuhusu masuala mbalimbali ya kikatiba yanayohusu vikwazo vya Jeshi la Magereza dhidi ya Mhe. Tundu Lissu, mawakili wake, ndugu, viongozi na wanachama wanaomtembelea gerezani.
Miongoni mwa masuala yanayolalamikiwa ni pamoja na kuzuiwa kwa viongozi na wanachama kumuona Mhe. Lissu gerezani, pamoja na vitendo vya askari wa magereza vya kusikiliza mazungumzo kati ya Mhe. Lissu na mawakili wake wanapofanya mashauriano ya kisheria, jambo ambalo linakiuka haki ya faragha na haki ya mawakili kufanya kazi yao kwa mujibu wa Katiba na Sheria.
Katika shauri hilo, Mhe. Tundu Lissu ni miongoni mwa wajibu maombi (Respondents, huku Chama cha Wanasheria Tanganyika kitashiriki kama mdau mwenye maslahi katika shauri (Interested Party) baada ya Mahakama kukubali maombi yake.
Aidha, kutokana na uzoefu wao wa kukumbana na changamoto hizo wanapomtembelea Mhe. Lissu gerezani kwa ajili ya mashauriano ya kisheria, Mhe. Lissu anatarajiwa pia kuwahoji mawakili waliofungua shauri hilo ili waweze kuieleza Mahakama kuhusu mazingira halisi wanayokumbana nayo wanapotekeleza wajibu wao wa kitaaluma.
Shauri hilo litasikilizwa kwa njia ya Mtandao mbele ya Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu; Mhe. Jaji Mruma, Mhe. Jaji Dkt. Rumisha na Mhe. Jaji Dkt. Longopa.
Shauri hili ni miongoni mwa mashauri muhimu ya kikatiba yanayoweza kuweka mwelekeo wa kisheria kuhusu haki ya mawakili kufanya mashauriano ya faragha na wateja wao waliopo mahabusu au gerezani, pamoja na kulinda misingi ya haki ya kupata msaada wa kisheria na usiri wa mawasiliano kati ya wakili na mteja.
Imetolewa na:
Wakili Paul Kisabo
Dar es Salaam
30 Juni 2026
Hi guys, I need a huge favor. Naomba msaada wenu mkubwa.
Hili tangazo ni la maana sana, siwezi kuelezea kwa kina sasa hivi ila baadae nitawaelezea. Ila ni process ya kupata account zangu za meta (instagram na Facebook)
Naomba mnitumie posti yoyote ile ya Mmarekani yoyote yule, mweusi au Mzungu ambae kawahi kuandika posti yoyote ile akiikosoa serikali ya Tanzania na posti hiyo haikufutwa au kuchukuliwa hatua na meta, posti lazma iwe kwenye mitandao ya instagram au facebook sio humu X.
Sio lazma awe Mmarekani au mzungu, hata awe mweusi ila sio Mtanzania ila awe anaishi hapa Marekani au hata nje ya Marekani.
Yani kwa kifupi posti za foreigners haswa wazungu wakiikosoa serikali ya Tanzania.
Naomba mnitumie kupitia whatsapp +1 424-537-3057
Tarehe 29 sio tarehe ya kawaida tena.
Tutawakumbuka daima mashujaa wote waliouwawa wakidai haki.
Na maelfu waliopigwa risasi wakauwawa wakati Samia akijilazimisha kuwa rais wa Tanzania.
Damu zenu zisinyamaze kamwe hadi haki ipatikane.
Rest in power, comrades! #MO29#Saba7
Baba Askofu nakusalimu. Hili jambo huwa linanitafakarisha sana. Kanisa linapomchagua mwanasiasa kuwa mgeni rasmi kwa kuamini kwamba kupitia kwake litapata fedha nyingi.
Msingi huu wa fikra unawajengea wanasiasa dhana kwamba ili wakubalike na kuheshimiwa, ni lazima wawe na uwezo wa kutoa fedha, haijalishi zimepatikanaje. Kwa namna hiyo, tunachangia kulea utamaduni wa ubadhirifu na ufisadi katika uongozi.
Cha kusikitisha zaidi ni kwamba, bila kukusudia, Kanisa linaweza kujikuta likihalalisha mfumo unaodhoofisha uadilifu. Nafikiri waumini wanahitaji fikra mpya zitakazotanguliza maadili kuliko fedha.
KATAMBI, acha kutufokea. Tupatie uthibitisho wa kisheria. Tuonyeshe ni ibara gani ya Katiba au sheria gani inayokupa mamlaka ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Kama katazo lenu ni halali, thibitisheni hilo kwa kutaja vifungu vya sheria. Taifa hili linatakiwa kuongozwa kwa misingi ya sheria na Katiba, na si kwa mabavu au utawala wa kiimla.
DOLA NI NINI? TOFAUTI KATI YA DOLA, SERIKALI, BUNGE NA MAHAKAMA
Na Rev Peter Simon Msigwa
Kumekuwa na mkanganyiko mkubwa katika mijadala ya kisiasa kuhusu maana ya dola na nafasi ya serikali ndani ya dola. Wakati mwingine serikali huonekana kana kwamba ndiyo dola yenyewe. Hata hivyo, kwa mujibu wa nadharia ya dola na misingi ya Katiba, hayo ni mambo mawili tofauti.
Dola ni mfumo mzima wa mamlaka ya umma unaoundwa na wananchi kupitia Katiba ili kulinda usalama, haki, amani na ustawi wa taifa. Dola ndiyo taasisi ya kudumu ya taifa; haibadiliki kila baada ya uchaguzi. Serikali zinaweza kubadilika, lakini dola hubaki.
Ndani ya dola kuna mihimili mikuu mitatu: Bunge, Serikali (Mtendaji) na Mahakama. Kila mhimili una mamlaka na wajibu wake, lakini yote yanatokana na Katiba.
Bunge ni sehemu ya dola, si sehemu ya serikali. Jukumu lake ni kutunga sheria, kuidhinisha matumizi ya fedha za umma na kuisimamia serikali. Serikali inapowajibika mbele ya Bunge, maana yake si kwamba Bunge ni sehemu ya serikali, bali ni kwamba Bunge lina mamlaka ya kuhakikisha serikali inatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba na sheria.
Mahakama nayo ni taasisi ya dola, si ya serikali. Jukumu lake ni kutafsiri Katiba na sheria, kutoa haki na kulinda haki za wananchi. Mahakama inapaswa kuwa huru ili iweze hata kuitangaza serikali kuwa imekiuka sheria au Katiba pale inapobidi. Ikiwa mahakama ingekuwa sehemu ya serikali, isingeweza kutenda haki kwa uhuru.
Kwa hiyo, serikali ni mhimili mmoja tu wa dola. Serikali ndiyo yenye jukumu la kutekeleza sheria na kuendesha shughuli za kila siku za nchi, lakini si mmiliki wa dola. Serikali hupewa dhamana ya kuongoza kwa kipindi maalumu na mamlaka yake yana mipaka iliyowekwa na Katiba.
Mipaka hiyo ni pamoja na kwamba serikali haiwezi kuwa juu ya Katiba; haiwezi kuingilia uhuru wa Mahakama; haiwezi kulinyima Bunge mamlaka yake ya usimamizi; wala haiwezi kutumia taasisi za dola kwa maslahi ya chama cha siasa au ya viongozi binafsi. Taasisi za dola zinapaswa kulitumikia taifa na wananchi wote bila upendeleo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaweka wazi mgawanyo wa madaraka kati ya Bunge, Serikali na Mahakama. Mgawanyo huo ndiyo msingi wa utawala wa sheria na unazuia mamlaka yote kujikusanya mikononi mwa chombo kimoja.
Pale serikali inapoanza kujiona kuwa ndiyo dola, au pale taasisi za dola zinapoonekana kutumikia serikali au chama tawala badala ya Katiba na wananchi, misingi ya utawala wa sheria huanza kudhoofika. Demokrasia haiimariki kwa kuwa na serikali yenye nguvu kuliko taasisi nyingine; huimarika kwa kuwa na taasisi huru zinazowajibishana na kila mmoja kuheshimu mipaka ya mamlaka yake.
Kwa hiyo, ni muhimu kutambua ukweli huu: Dola ni ya wananchi. Serikali ni msimamizi wa muda wa mamlaka ya dola. Bunge hutunga sheria. Mahakama hutafsiri sheria na kutoa haki. Serikali hutekeleza sheria. Hakuna mhimili unaopaswa kujiona kuwa juu ya mwingine, kwa sababu wote wanawajibika kwa Katiba na kwa wananchi.
Kaka @zittokabwe habari yako!
Umekuwa mkali baada ya Mkuu wa Majeshi Uganda, Dikteta Muhoozi Kainerugaba kutoa agizo la kufunga vituo vya NTV na gazeti la Daily Monitor, ukisema ni shambulio dhidi ya uwekezaji wa Kitanzania.
Nyumbani kwetu hapa, kituo cha JAMBO TV (kinachomilikiwa na rafiki yako, John Marwa) kimefungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa siku 90 kwa kukiuka kanuni zao.
JAMII FORUMS, ilifungiwa kwa siku 90 na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Septemba 2025 kwa tuhuma za kuchapisha maudhui ya kupotosha na kudhalilisha serikali. Hukupaza sauti kabisa.
Walistahili kupiganiwa ipasavyo kwa wewe kupaza sauti. Unatetea maslahi ya matajiri (tycoons) wa kisiasa waliowekeza nje ya nchi wakati huo ukipuuza ukandamizaji wa vyombo vya habari ndani.
Unakaa kimya wakati JAMBO TV inafungiwa hatua inayoumiza waandishi wa habari wa Kitanzania moja kwa moja, unasimama kutetea maslahi ya kampuni ya Mauritius inayofanya biashara Uganda.
Kwamba kufungwa kwa vyombo hivyo Uganda ni pigo kwa uwekezaji wa Watanzania? Muundo wa kampumi ya TAARIFA LIMITED unapingana na hoja yako ya msingi. Huo siyo uwekezaji wa Kitanzania.
TAARIFA LIMITED ni kampuni ya uwekezaji (investment holding company), ilichaguliwa kama muundo wa kisheria kwa ununuzi wa hisa kubwa katika kampuni ya Nation Media Group (NMG)
Ilitumika katika ununuzi wa hisa (54%) katika kampuni ya Nation Media Group (NMG), kupitia kununua NPRT Holdings Africa LTD kutoka Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED).
TAARIFA LIMITED, ambayo ilichukua 54% ya hisa zilizokuwa za Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED) ndani ya Nation Media Group (NMG) imesajiliwa MAURITIUS siyo Tanzania
Kisheria na kiuchumi, uwekezaji uliosajiliwa katika maeneo yenye nafuu ya kodi (tax havens) kama MAURITIUS haunufaishi uchumi wa Tanzania moja kwa moja. Siyo ‘Tanzanian-owned businesses’
Hakuna namna fedha zinazozalishwa na vyombo hivyo nchini Uganda zitakavyoingia kwenye mfumo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuongeza akiba yetu ya fedha za kigeni (foreign reserves). HAIPO
Zinaishia akaunti za mabenki ya kigeni Mauritius au kwingineko. Mauritius inajulikana kwa kuwa na mikataba ya kuzuia utozaji kodi mara mbili (Double Taxation Avoidance Agreements - DTAAs)
Inapotokea kampuni imeuza hisa zake au inapata faida, kodi ya faida inalipwa MAURITIUS (ambako viwango ni vidogo au ni sifuri) badala ya Tanzania au nchi ambako biashara halisi inafanyika.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) haiwezi kudai kodi ya mapato (income tax) ya moja kwa moja kwenye miamala inayofanyika chini ya mwavuli wa kampuni iliyosajiliwa katika nchi ya Mauritius.
Kampuni ikisajiliwa Mauritius, iko chini ya sheria za makampuni Mauritius. Tanzania haina mamlaka ya kisheria (jurisdiction) kuhoji muundo wa utawala, akaunti za benki, uwazi wake wa kifedha.
Kodi, faida, na miamala ya kimkakati ya kampuni hiyo haiingii katika mfumo wa mapato ya ndani wa Tanzania. Huo siyo ‘uwekezaji wa Kitanzania’. Labda utafute jina lingine la kuita huo uwekezaji.
Faida inayopatikana kupitia mianya hii ya tax havens hairudi kama kodi ya kujenga shule, hospitali au barabara, ni pesa za mifukoni za wafanyabiashara wakubwa wa kisiasa na makada wa CCM.
Fedha hizi ndizo zinazotumika kufadhili harakati za kisiasa za ndani, ikiwemo kampeni za uchaguzi na matukio ya ukandamizaji wa kisiasa kama yale yaliyoshuhudiwa nchini mnamo Oktoba 29.
Badala ya kuhoji ni kwa namna gani uwekezaji huo wa Taarifa Limited katika vyombo vya habari vya Uganda unamsaidia mwananchi wa kawaida wa Tanzania, unakuwa mtetezi wa biashara za MaCCM.
Unapigania maslahi ya matajiri ambao wanatumia faida zao kudhoofisha demokrasia. Unasikitikia uwekezaji uliosajiliwa Mauritius usiokuwa na tija ya kodi au ajira ya moja kwa moja kwa Mtanzania.
MMM, Martin Maranja Masese, Masese
Nina swali, wale wapuuzi waliokuwa wanapush maridhiano kati ya Watanzania na wauwaji wa CCM wana la kusema kwa sasa????
Wanaharakati tulipokuwa tunayakataa maridhiano tulijua wauwaji hawako tayari kwa maridhiano ya kweli, wanachotaka kwenye maridhiano ni legitimacy na uwezo wa kuwazodoa international community kwa kuwaambia, msituingilie sisi tumeshafanya Maridhiano na tume heal.
About 10 minutes ago, two people, a man and a woman, showed up at my house. They knocked for several minutes. At first, I didn’t answer, hoping they would eventually leave. Instead, they kept knocking louder and louder.
Because I know my life is in danger and I’m home alone right now, I decided not to even go near the door or look through the peephole. My husband has always told me not to do that. He said if someone came to kill me, they could shoot me through the door if they knew I was standing there.
So I stayed well away from the door and asked what they wanted. They said they were looking for someone named Louis. I told them no one by that name lives here. They then asked me to open the door because they couldn’t hear me properly. I refused and told them they could speak from where they were.
The moment I said that, they started walking away. I immediately ran upstairs and recorded them from my balcony.
The woman did all the talking. The man didn’t say a word.
As I have informed you all before, the Tanzanian government has commissioned Mexican cartels to kill me. Today, while I was home alone, two Mexicans showed up at my front door.
Everything is being forwarded to the FBI.
If anything happens to me, this is where the investigation should begin.
I think the time has come for me to put away my fear of guns and buy one. Hopefully this week I find the courage to own one.
KISWAHILI
Takribani dakika 10 zilizopita, watu wawili, mwanamume na mwanamke, walifika nyumbani kwangu. Waligonga mlango kwa dakika kadhaa. Mwanzoni sikuitika, nikitumaini kwamba wangeondoka. Badala yake, waliendelea kugonga kwa nguvu zaidi na zaidi.
Kwa sababu ninajua maisha yangu yako hatarini na kwa sasa niko peke yangu nyumbani, niliamua kutosogea hata karibu na mlango wala kutazama kupitia tundu la mlango. Mume wangu amekuwa akiniambia kila mara nisifanye hivyo. Aliniambia kwamba kama kuna mtu amekuja kuniua, anaweza kunipiga risasi kupitia mlangoni akijua nimesimama nyuma ya mlango.
Kwa hiyo nilibaki mbali na mlango na kuwauliza wanataka nini. Walisema wanamtafuta mtu anayeitwa Louis. Nikawaambia hakuna mtu wa jina hilo anayeishi hapa. Kisha wakaniomba nifungue mlango wakidai hawawezi kunisikia vizuri. Nilikataa na nikawaambia wazungumze wakiwa waliposimama.
Mara tu niliposema hivyo, walianza kuondoka. Nilikimbia haraka ghorofani na kuwarekodi kutoka kwenye roshani yangu.
Mwanamke ndiye aliyekuwa akizungumza muda wote. Mwanamume hakusema hata neno moja.
Kama nilivyowaeleza hapo awali, serikali ya Tanzania imewaajiri makundi ya wahalifu wa Mexico (Mexican cartels) ili kuniua. Leo, nikiwa peke yangu nyumbani, Wamexico wawili walifika kwenye mlango wa nyumba yangu.
Taarifa zote zinawasilishwa kwa FBI.
Ikiwa chochote kitanitokea, uchunguzi unapaswa kuanzia hapa.
Nadhani muda umefika wa mimi kuacha kuogopa silaha na sina budi kununua silaha wiki hii ili mtu akigonga tena mlangoni naenda mlangoni na bunduki.
One day the whole world will understand me
I am a canary in the coalmine and warned about lawafare, enforced disappearances and media shutdown in #Tanzania and I warned that it will spread in the region like a virus!
Until we continue to outsource our power and sovereignity to a group of people there will always be those who take advantage and grab it all!
This is not only a physical or psychological warfare, it is a spiritual warfare as well
#TutaelewanaTu
Ni Wakati Gani Serikali na Chama Tawala Vinakuwa Tishio kwa Usalama wa Taifa?
Rev Peter Simon Msigwa.
Hili ni swali zito, na ukweli ambao si rahisi kuusema ni kwamba serikali na chama tawala kimsingi vimepewa wajibu wa kulinda usalama wa taifa. Hata hivyo, chini ya mazingira fulani, vinaweza kuanza kuwa sehemu ya tatizo na kudhoofisha usalama huo wenyewe.
Mara nyingi tunapozungumzia usalama wa taifa, fikra zetu hukimbilia jeshi, polisi, vyombo vya ulinzi na usalama, mipaka ya nchi au uwezo wa kukabiliana na maadui kutoka nje. Hayo ni muhimu, lakini siyo msingi mkuu wa usalama wa taifa.
Msingi wa usalama wa taifa ni imani ya wananchi kwa dola na taasisi zake.
Serikali huanza kuwa tishio kwa usalama wa taifa pale inapoweka kuendelea kubaki madarakani mbele ya kulinda Katiba, sheria na maslahi ya taifa. Wakati chama tawala kinapoanza kujiona kuwa ndicho taifa, na yeyote anayekikosoa anaonekana kama adui wa nchi, hapo msingi wa taifa huanza kuyumba.
Chama cha siasa ni cha muda; taifa ni la milele.
Taasisi za dola zinaposhindwa kutumikia wananchi wote kwa usawa na badala yake kutumiwa kulinda maslahi ya kisiasa ya watawala, imani ya wananchi huanza kupotea. Mahakama zinapoonekana hazitendi haki kwa uhuru, Bunge linaposhindwa kusimamia Serikali, na vyombo vya dola vinapoonekana kutumikia chama badala ya Katiba, changamoto ya usalama wa taifa huanza kutoka ndani ya mfumo wenyewe.
Serikali huwa tishio kwa usalama wa taifa pale ukosoaji unapochukuliwa kuwa uasi badala ya uzalendo. Taifa lolote lenye afya ya kisiasa hukua kwa sababu lina wananchi wanaoweza kusema ukweli hata unapoumiza. Kukandamiza sauti za wananchi hakuondoi matatizo; huyaficha kwa muda mpaka yanapokuwa makubwa zaidi.
Pia serikali huwa tishio pale:
Hofu inapochukua nafasi ya uhuru.
Utii kwa viongozi unapokuwa muhimu kuliko utii kwa sheria.
Uaminifu kwa chama unapewa thamani kuliko uwezo na uadilifu.
Uchaguzi unapopoteza uaminifu wa wananchi.
Vyombo vya ulinzi na usalama vinapoingizwa katika ushindani wa kisiasa badala ya kubaki waaminifu kwa Katiba na taifa.
Historia inatufundisha jambo moja muhimu: mataifa mengi hayajaanguka kwa sababu wananchi walikuwa huru kusema; yameanguka kwa sababu viongozi walikataa kusikiliza waliokuwa wakisema ukweli.
Usalama wa taifa wa kweli haujengwi kwa nguvu za dola pekee. Unajengwa juu ya nguzo tano:
Katiba kuheshimiwa kuliko matakwa ya watawala.
Taasisi zinazojitegemea na kutenda haki bila upendeleo.
Sheria kutumika kwa usawa kwa kila mtu.
Ushindani wa kisiasa ulio huru na wa haki.
Serikali inayowajibika kwa wananchi na kujenga imani yao.
Serikali yenye nguvu si ile inayowaogopa wapinzani wake; ni ile inayojiamini kiasi cha kuvumilia ukosoaji. Taifa lenye nguvu si lile linaloziba midomo ya wakosoaji; ni lile linalojibu hoja kwa hoja na changamoto kwa utendaji bora.
Uzalendo si ukimya mbele ya makosa. Uzalendo ni ujasiri wa kusema ukweli kwa lengo la kulijenga taifa.
Kutetea Katiba si kupinga serikali. Kutetea uhuru wa Mahakama si kuhujumu dola. Kudai uwajibikaji si kuhatarisha usalama wa taifa. Kinyume chake, hayo ndiyo yanayolinda taifa dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka.
Kiongozi mwenye maono haulizi, “Tutabaki madarakani kwa namna gani?” Bali huuliza, “Tutaliachaje taifa letu likiwa imara zaidi kuliko tulivyolikuta?”
Kwa sababu mwisho wa yote, serikali zitapita, vyama vya siasa vitabadilika, viongozi watastaafu, lakini taifa lazima libaki.
Huo ndio wajibu mkuu wa uongozi wa kweli.
What you see in this video is the reason political rallies have now been banned in Tanzania. The opposition’s rallies were growing larger with each passing day. Not only were they drawing massive crowds, but people attending the rallies were also voluntarily donating money to support the opposition.
It was a clear and powerful rebuke of Samia Suluhu’s regime by the people of Tanzania.
@POTUS@SenTedCruz@SenatorShaheen@SenateForeign@SFRCdems
Message za kutisha zinazidi kuja Dm.
@jmkikwete do the needful you greedy evil man. Unaangamiza nchi for personal gain????? Samia has no major power kwenye system ya usalamaTZ, especially bara, wewe ndio una drive nchi kuingia kwenye laana ya machafuka kwa manufaa yako na familia yako.
Watanzania hawajahi kufika sehemu wanawaza vitu kama hivi. Wanachodai ni haki.
Wananchi wasikilizwe kabla nchi haijafika point of no return