Upumbavu ni kushughulika na umbea na kuacha mambo ya msingi ya kujenga nchi.
Huku ni kukosa hoja. Haiwezekani kiongozi mwenye hoja kutishwa na agenda za mitaani.
Hana mwaka kazini anaanza kuwaza URAIS.
Tundu Antipas Mugwai Lissu, you can't go toe to toe with this Man broh 🙌.
Yani anaelezea jambo kwa hoja zinazomake sense hata mwendawazimu anaweza elewa
Richard Rugemalira Balile upeo wake ni mkubwa na maswali yake yalikuwa magumu sana, kama unataka kujua kwamba maswali yake yalikuwa magumu fikiria ungekuwa unaulizwa wewe ungeyapatia majibu? Tatizo ni kakutana na mtu mwenye upeo mkubwa zaidi sana kwenye mambo hayo akafichwa vibaya mno.
NJIA RAHISI YA KUIFUTA CHADEMA: AANDIKA ASKOFU BAGONZA
Watu wengi uraiani, vijiweni na serikalini wameniuliza nitoe maoni juu ya hatua ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kuiandikia barua Chadema. Barua hiyo inatafsriwa kuwa ina lengo la kuifuta CDM au kuifungia. Maoni yangu yanapendekeza njia rahisi na SALAMA ya kuifungia au hata kuifuta Chadema.
1. Niliwahi kusema kuwa “uchaguzi mkuu bila CDM ni sawa na kufikiria uchaguzi bila CCM”. Tumekuwa na uchaguzi bila CDM. Kila mtu anauhoji. Asiye mtu ndiye anaona ni kawaida.
Je twaweza kujaribu uchaguzi bila CCM? Nashauri tusionje sumu.
2. Wazo la kuifuta Chadema lipo. Nashauri twende njia ile ile ya uchaguzi lakini tubadili formula au mpangilio. Tuifute CCM na kubakiza CDM. Halafu tuishauri CCM kwa siri ili iombe radhi. CCM isamehewe na kurudi uwanjani.
3. Halafu tuifute CDM. Kwa “kiburi” chao watakataa kuomba radhi. Ifutwe moja kwa moja. Kwa njia hiyo CDM watakula jeuri yao na CCM watavuna matunda ya unyenyekevu wao.
4. Mpangilio huu unazingatia ukweli kwamba, CCM na CDM wote ni wababe. Mmoja ana bunduki na risasi, mwingine ana manati na mawe. Na hatuna utawala wa sheria ulio na miwani ya kuona madhambi ya CCM. Chadema inasaidiwa na dola ijione kuwa inaonewa. Ofisi ya Msajili-kipofu inahujumu maridhiano na amani ya nchi kwa kudhani inaikomoa CDM.
5. Tuliwahi kuvifuta TANU na ASP na kuzalisha CCM. TANU haikuwa na historia ya kumwaga damu lakini ikaungana ASP iliyokuwa na damu mikononi mwake. Mtoto CCM aliyezaliwa ana nini? Tukiifuta CDM itazaliwa ipi?
6. Mnaonaje tuifute TEC tubakize CCT!? Au tuifute BAKWATA tubakize Shura ya Maimamu au Answar Sunna?! Nayasema haya kwa sababu tumefeli kuishi kwa amani na tofauti zetu. Narudia kushauri WASAJILI WETU wafanye kazi ya kusajili siyo kuendesha taasisi wanazozisajili.
7. Tatizo siyo CCM, Wala CDM. Na tatizo siyo Rais SSH. Anaweza kuwa anaonewa na kuhujumiwa. Atazungumzaje maridhiano wakati watu wake wanakazana kufungia, kuteka, kukata vichwa, kuzuia mijadala nk? Tutagundua tumechelewa.
8. Tuna matatizo makubwa mawili: Fedha na hofu ya ukweli. Kwamba fedha zinunue utu, uhai, haki, teuzi, heshima, ukweli, chaguzi, na ajira. Halafu, kila mtu aogope kuonana wala kusikilizana na Ndugu UKWELI. Kuogopa ukweli kunatibiwa na kukubali ukweli.
9. Fedha/Rushwa imeingizwa katika vyombo vitakatifu mpaka mahekaluni. Ni tamu. Utamu huu unavifanya vyombo hivyo vitamani madaraka ili vilinde rushwa. Nashauri tuchore msitari, tuache rushwa. Tusipoacha, atainuka mtu anayekula rushwa lakini ameichukia. Atatutapisha hiyo rushwa. Mbona mnasahau upesi?!
10. Namba 1 mpaka 9 hapo juu yaweza kusababisha walio madarakani waogope kuondoka kwa kuhofia kulipwa kisasi. Wanaotafuta madaraka wanaweza kuwa wanapania wakiingia walipe kisasi. Hakuna mwisho bila kuweka msitari. Kisasi kina risasi.
Wajomba wa Kijaluo wana hekima isemayo, “Mwanamme mkalimu kupita kiasi husababisha watoto wa majirani wazaliwe wakimfanana”.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Mzee Warioba alipoongea juzi kuwa October 29 tume ndio ilipiga kura hakukosea na ushahidi huu hapa.
Nilishaposti hizi video instagram baada ya mauaji ya October 29.
Embu cheki, kipindi nchi nzima iko kwenye darkness Tume ya uchaguzi na CCM ndio walikuwa wanafanya kazi hii.
Uchaguzi wa Octover 29 2025 ni null and void. Hatuutambui.
I think wanasiasa wote wa upinzani, wanaharakati wote na yoyote Tz ambae hana uhakika na usalama wake ni lazma watumie hii app inaitwa life360.
Niliijua hii app kupitia crime show inaitwa 2020. Polisi hapa Marekani walimpata mtu aliemteka na kumuua msichana mdogo wa miaka 16 kwa kutumia hii app. Huyo msichana na rafiki zake close walijiunga na hii app wakawa wana trackiana, alipopotea wenzie wakawapa polisi data zake za kwenye hii app. Polisi wanatumia app kujua the exact moment and location aliyopotea.
Mimi naitumia kuwa track watoto wangu 24/7. Kenzo haipendi hii app ila hana choice. Na pia naitumia kwa shemeji yenu kuni track.
Hii app inatrack kila kona mtu anapoenda na it’s tuma allert kwa watu waliopo kwenye circle yako. Yani ukitekwa na simu kuzima inaonyesha kabisa ulitekewa eneo gani na simu ilizimiwa wapi na saa ngapi. Na simu ikitupwa pia inaonyesha iliyopita wapi na saa ngapi.
Yani kwa kifupi ina track kila sehemu ulipokuwa simu nzima, kila barabara uliyopita, kila sehemu uliposimama mpaka dakika unatekwa inatuma alert kwa watu kwenye circle yako. Hata kama ulikuwa unatembea kwa miguu then ukapandishwa kwenye gari inaonyesha mpaka speed ya gari na mwelekeo wa gari inaonyesha.
I wish Polepole au Mzee Kibao wangekuwa na hii app kwenye simu zao, tungejua kwa ushahidi usiopingika walichukulia saa ngapi na exact location waliyochukuliwa na mwelekeo walipoenda. Yani ikiwashwa tu inatuma alert. So muda ule wanakufosi utoe password hii app inaonyesha watu wako mahali ulipo na hata wakiifuta app kwenye simu yako ila tayari alert zimetumwa kwa watu wa circle yako.
Hata ukipata ajali ya gari inatuma message kwa watu wako kuwa umepata ajali na eneo ulilopatia ajali.
Narudia tena wanasiasa wooote wa upinzani na wanaharakati lazma uwe na hii app kwenye simu then add mtu mmoja au wawili unaowaamini ili lolote likikupata tunajua pa kuanzia.
Kwa wazazi, kama unamtoto kaanza ku drive hii app inakwambia mtot anaendesha gari kwa speed gani na hata akigusa simu huku anaendesha inakutumia ujumbe.
Jamani naomba tusisikie tena mtu katekwa Tanzania alafu hakuna mtu wake wa karibu wa kutupa hii tracking. Hii app ina save tracking record ya siku 30.
Izi ni damu zilizomwagwa na Samia suluhu za vijana wasio na hatia wa Taifa hili na hakuna namna izi damu zitamuacha salama wakati wako uko karibu sana damu yako, ya kizazi chako na ya serikali yako itamwagika kama ulivyomwaga damu ya ndugu zetu.
Huu mtambo tulioweka ikulu leo unaweza kueleza chochote kweli?🤔🤔🤔
Tuliwezaje kuporomoka kutoka kuongozwa na watu kama Nyerere na Sokoine mpaka kuwa na Samia na Mwigulu??🤔🤔
Kumbe ile kauli ya Jaji Chande kusema kwamba kuna wanaccm walichochea Maandamano kwasababu walikatwa majina ni taarifa ambayo aliipata kutoka kwa msaidizi wa Mafwele, George Bagyemu.
Hawa watu wanaroho za kikatili sana, maisha yao yamejaa hila kila siku wakilala, wakiamka wanawaza kubambika watu kesi za uwongo.
Huyu Bagyemu na wenzake ndo waliotumika kumbambika Mhe. Lissu kesi ya mchongo ya uhaini.
Warioba amefanya interview nzuri sana, anasema kwa maoni yake uchaguzi 29 October 2026 ni Tume ya Uchaguzi ndio ilipiga kura
Sio rahisi kupata hizo asilimia 97% kwa hali ile ya uchaguzi,
Namna pekee ni kwamba Tume ya Uchaguzi ilitengeneza yale matokeo
Sasa Mafwele ,Abdul, Makonda na Iddi Amini Mama tusikie huyu mzee amepata changamoto halafu mtuambiwa mambo ya yalipangwa, yakafadhiliwa na kutekelezwa
Ameshauri vizuri fanyieni kazi maoni yake.
Na kwa nini mnampa amri Mzee Warioba kuzima simu? makafundia Gazeti la Jamhuri kutokana na Mahojiano aliyofanya nao
Mkazuia TDC na UDASA kufanya event aliyoharikwa kuzungumzia hii Tume ya Chande !!! Kwa hali ya sasa lazima mtuue nchi nzima hakuna anayewaelewa kabisa
Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu aliyasema hayo katika mahojiano yaliyoruka Mei 9, 2026 na Jenerali Ulimwengu pamoja na Khalifa Said wa The Chanzo kuhusu Ripoti ya Kuchunguza Matukio ya Wakati na Baada ya Oktoba 29, 2025.
Fuatilia zaidi https://t.co/mvMyrA4S9a
#JamiiForums #Uwajibikaji