@McinikaWaLamar Jitathimini kila siku, kila wiki, kila mwezi, kila mwaka,
Nini cha maana umefanya/improve
Kama hakuna umekosea wap, ili isijirudie
Note:
Tupunguze muda wakukaa mitandaoni kwa video za vichekesho l, porn, na zisizo na mchango ku improve maisha yako
Nina miaka takribani sita kwenye Ndoa sasa Baba yangu alibariki Uamuzi wangu nikiwa na miaka 22 tu, lakini katika miaka sita (6) hii ya ndoa nimegundua mambo kadhaa.
1- Ndoa yangu huyumba sana kipindi ambacho Mimi huwa nayumba yaani siketi katika mstari sahihi.
2- Ndoa yangu hustawi sana kipindi ambacho Mimi huwa nasimama imara kwenye mstari sahihi.
3- Mimi kama Baba wa Familia napaswa kuwa na mambo mengi lakini hayapaswi kuathiri familia yangu.
4- Naishi kwa kuamini Mimi sio Mkamilifu nina makosa na nakosea, ni sahihi kumwomba radhi Mke wangu napomkosea kwakuwa ni Ubinadamu, ni sahihi kuwaomba radhi Watoto wangu napowakosea kwakuwa ni Uungwana.
5- Hakuna Mwanamke Mkamilifu ila kila mmoja anapambana kufit kwenye Ndoa yake, tumetoka mazingira tofauti na Malezi tofauti hivyo kuelekezana na kustiriana huku tukisonga.
6- Talaka ni hatua ya mwisho sana ambayo sio baraka kwenye dini, sio sifa kwa Mtaliki wala Mtalikiwa na sio hatua njema kwa Wazazi wa pande zote mbili, hakuna kisichorekebishika kikitangulizwa na IBADA.
7- Kwenye sababu za KUOA haipaswi kuwa Makalio, Urembo ama sifa, hatuoi ili kuficha madhaifu bali tunaoa kwasababu tupo tayari kuingia kwenye darasa la furaha na huzuni lakini tutafika salama.
8- Ndoa ikileta baraka ya Watoto mtagundua tunaoana kwasababu ya Familia, kwasababu ya Watoto na hatupaswi kuwarithisha shida zetu sote tuishi na tusonge kwa ajili yao.
9- Ingali nimeoa Kijana najitahidi kutoleta Ujana kwenye Ndoa, Usela wa Masela kuja Maskani kila Wakati HAPANA, mapema kurudi home na kuchelewa kutoa taarifa ni MISINGI.
10- Mwalimu wa ndoa? Hayupo na hatotokea kwasababu kila mmoja ana Mtihani wake wenye maswali tofauti, jitahidi kujibu mtihani wako kwa mazingira yako naamini hivyo.
MWISHO, hakuna Mwalimu wa Mapenzi wala Ndoa, ni kudra za Mwenyezi Mungu katika kila kitu ukiweza hata kuvuka mwaka kwenye Ndoa basi shukuru Mungu, hii ni Ibada ina vita yake.
Mwenyezi Mungu awajalie kheri Wana Ndoa wote๐ Taasisi yetu ya Migogoro hii unalala Kitanda kimoja na Adui yako na anakupikia unakula๐