@Oleshangay Yeah! Once,, The father of this nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, said, we need a leader, who, when he speaks, and you looks into his eyes and meant what he says. This one, if you look at him carefully, you will understand what he says, doesn't match his consciousness.
@TZUnitedNations Why does the United Nations allow a Tanzanian representative to issue a speech, especially when considering the massive killings they committed on Oct 29? And just yesterday they kidnapped Lissu's aide who was seriously injured. UN must rethink on its move to Tanzanian Gvt.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 24, 2026
Last time tuliishia Part 222 so leo tunaendelea na-;
Part 223
Majaji wameingia na Mshitakiwa pia ameingia.
Karani anasoma shauri hapa.
Anasimama Renatus Mkude anasema yupo na Ajuaye, Katuga, Thawabu, Cathbert Mbiringe.
Anasema leo tumekuja kwa ajili ya kupokea ruling na sisi tuko tayari.
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa unasemaje?
Mhe. Lissu: Na mimi niko tayari.
Jaji anaanza kusoma hapa UAMUZI.
Uamuzi huu unatokana na pingamizi lililowekwa na pingamizi la mshitakiwa kutokana na taarifa ya kuongezwa kwa ushahidi.
Taarifa hiyo ililetwa tarehe 18/02/2026 na upande wa Mashitaka kwamba unatokana na pingamizi lililowasilishwa na mshitakiwa.
Notice hiyo ililetwa kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha CPA.
Mshitakiwa alieleza Mahakama kwamba kifungu hicho kinaelezea shahidi ambae maelezo yake hayakusomwa wakati wa mwenendo kabidhi na hivyo walichokileta upande wa mashitaka ni kuleta ushahidi mpya.
Upande wa mashitaka walijibu notice ipo halali kwa mujibu wa sheria na imekibidhi matakwa ya kisheria na ipo kwa mujibu wa sheria.
Huo ndio ulikuwa msingi wa hoja za pande zote mbili.
Mahakama imeona hoja inayopaswa kuamuliwa ni je notice hiyo ipo kwa mujibu wa sheria?
Ili kurahisisha Mahakama imeona ili reproduce notice hiyo inavyosema.
Anasoma notice inavyosema kwamba ni notice ya kuongeza maelezo ya ziada ya shahidi husika ambae ni Amin Mahamba.
Hakuna mashaka kwamba upande wa mashitaka wanataka kuongeza ushahidi wa Amin Mahamba.
Kwa vile Amin Mahamba ni shahidi na statement yake ilishasomwa wakati wa committal ilishasomwa.
Notice inasema ushahidi unaotaka kuletwa ni wakati wa uchaguzi wa tar. 29/10/2026.
Anasoma kifungu cha 308 cha CPA kinavyosema.
Ukiangalia kifungu hicho kinatoa masharti au mazingira ambayo notice hiyo ni reasonable au laaa.
Masharti ni kwamba
1. Maelezo yatoke kwa shahidi
2. Uwe ni ule ushahidi ambao haukusomwa wakati wa committal
3. Uwe ni ushahidi ambao haukusomwa wakati wa proceedings
Kifungu cha 308 ndio kinachosema hawezi kutoa ushahidi hadi watakapoleta notice na hivyo basi ukiangalia hayo kifungu hicho cha 308 kinafungua mlango kwa shahidi ambae alikuwepo na bahati mbaya maelezo yake hayakuletwa.
Amin Mahamba maelezo yake yalikuwepo wakati wa commital, anataka kuleta mambo ya Uchaguzi ambayo hayakuwepo wakati wa committal.
Ipo kinyume na kifungu cha 308 cha CPA.
Hivyo basi kifungu cha 308 kinaweza kuruhusu notice hiyo tumeona kwamba kifungu hicho hakiruhusu kabisa.
Shauri la Remina Omary Abdul tumeona linahusiana na vielelezo vya wakati wa committal. Shauri hilo haliwezi kutibu chochote katika hoja iliyopo mbele yetu.
Hiyo notice ya kuongezwa kwa ushahidi ambayo imeletwa na upande wa mashitaka haitambuliwi na kifungu cha 308 cha CPA.
Kimsingi tunasema kwamba fundamentally haiko sahihi na baada ya kusema hayo basi notice hiyo ni incompetent na tiba pekeee iliyopo ni kwamba notice hiyo lazima iwe struck out. Ni hayo tu.
Anasimaa. RENATUS MKUDE anasema baada ya kupokea ruling tunatafakari tunaomba ahirisho ya lisaa limoja.
Twende kutafakari.
Bado majaji wanashauriana pale juu.
Nafikiri leo KATUGA atajua vizuri nani ni Bingwa wa Sheria😂
Anasimama Mh. Lissu anasema mmesema kuwa mashahidi waletwe leo na mlisema tutasikiliza uamuzi wa pingamizi na tutasikiliza shauri leo.
Sasa wanasema tuahirishe kusikiliza ili wakatafakari.
Wanaenda kutafakari nini? Ili iweje? Huu uamuzi haukatiwi rufaa.
Tusipoteze muda kila tunapopoteza muda anayeumia ni mimi sasa wao walipaswa kuleta mashahidi na wasitupotezee muda kabisa, tuendelee kusikiliza shauri hili.
Majaji wanaandika kidogo
Anasimama Renatus Mkude anasema tumemsikia Mshitakiwa
Tuna mambo mawili.
1. Tumepokea ruling ya Mahakama na tumeikubali
2. Jambo la pili ni kwamba tulimtaja shahidi ambae lazima tuwezi kumuandaa shahidi yetu
Jaji Ndunguru anasema tulisema muwe na mashahidi wakutosha. Tukiendelea kubishana tutapoteza muda, turudi mahakaman saa 5 kamili
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 204
Mhe. Lissu anaendelea na Cross examination.
Mhe.Lissu: ulivosogea pembeni akakwambie twende kituoni ukatoe maelezo, waeleze waheshimiwa Majaji kama hayo maneno yapo?
Shahidi wa kificho P3 : hayapo.
Mhe.Lissu: badala yake yapo maneno yanayosema kwamba alikuja mtu aliyejitambulisha kuwa ni Askari Polisi na kunikakamata. Ni sahihi
Shahidi wa kificho P3 : ndiyo ni sahihi.
Mhe.Lissu: kwa hiyo hapakuwepo na maongezi alifika na kukukamata.
Shahidi wa kificho P3: sahihi
Mhe.Lissu: umesema ulipofika kituoni alikuweka mahabusu na baadae ukahojiwa kuwa unahamasisha uasi sasa waeleze waheshimiwa Majaji kama kuna maneno kwanini ulikuwa unahamasisha uasi.
Shahidi wa kificho P3: hapana hayapo.
Mhe.Lissu: Ahsante.
Mhe. Lissu: Twende tarehe 17 April 2025 waeleze waheshimiwa majaji kama katika maelezo yako kuna sehemu umesema kuwa aliyekuandika maelezo mwanzo ya terehe 4 april 2025 ndio aliyekuandika maelezo tarehe 17 april 2025?
Shahidi wa kificho P3 : Hayapo.
Mhe. Lissu: umesema ulipoandika maelezo mara ya pili akakwambia uendelee kuripoti kila baada ya siku tatu, yapo katika maelezo yako?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana.
Mhe. Lissu: umesema kwamba wewe kazi yako ni dereva wa boda boda kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P3 : kweli
Mhe. Lissu: waambie waheshimiwa majaji kama umeonyesha leseni
Shahidi wa kificho P3 : hapana
Mhe. Lissu: boda boda ni pikipiki kweli si kweli
Shahidi wa kificho P3 : Ni kweli
Mhe. Lissu: Umewaambia usajili wa hiyo pikipiki?
Shahidi wa kificho P3: Hapana
Mhe. Lissu: umewaonyesha waheshimiwa majaji kadi ya usajili wa hiyo pikipiki
Shahidi wa kificho P3: Hapana.
Mhe. Lissu: Shahidi naomba unisaidie, kwasababu kijiwe chako hatukijui kwasababu kimefichwa, kadi huna, leseni huna, je pikipiki umeleta?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: kwa hali hii kuna mtu ataweza kuthibitisha kwamba wewe ni dereva boda boda?
Shahidi wa kificho P3 : Mimi sijui.
Mhe. Lissu: unasema uliwahi kushiriki maandamano aliyowahi kuongozwa na Mbowe, ulijiandikisha sehemu yoyote.
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: Hata uliwahi kupigwa picha ukiwa kwenye maandamano hayo.
Shahidi wa kificho P3 : hata sijui
Mhe. Lissu: Unasema uliwahi kushiriki katika kongamano la vijana, uliwahi kujiandikisha?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: Uliwahi hata kujiandikisha kwa viongozi wa BAVICHA Mkoa wa Mbeya?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana.
Mhe. Lissu: sasa kwanini tusiseme wewe ni pandikizi la akina Kingai na mapolisi wake.
Shahidi wa kifichoP3 : Kimya
Mhe. Lissu: unasema ulishiriki mkutano wangu, ulijiandikisha popote?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: sasa weleze waheshimiwa Majaji wataamini vipi kuwa wewe ni mfuasi wangu na mwanachama wa CHADEMA?
Shahidi wa kificho P3 : Mimi sijui sasa, kama unanikataa mm sio mfuasi wako sawa.
Mhe. Lissu: sikukatai kaka, mimi sikujui na ninaogopa watu wasiojulikana kwasababu wanateka watu, wanabambikia watu kesi na kuua kwahiyo tutajua kama sio wewe mmoja wapo?
Shahidi wa kificho P3 : mimi sijui.
Mhe. Lissu: umesema ulikua na vijana wenzako kijiweni ukiwashawishi, waeleze waheshimiwa majaji kama umetaja orodha yao na majina yao.?
Shahidi wa kificho P3 : sijawataja.
Mhe. Lissu: Umeeleza kwamba ulikamatwa na askari Polisi, umemtaja kwa jina huyo askari polisi? Au hata namba yake tu na cheo je?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: tunaendelea, ninachukizwa na nyie mapandikizi ya polisi mnaletwa hapa halafu mnafichwa ndani ya kizimba, ngoja tuendelee.
Mhe. Lissu: unasema mlifikia uamuazi wa kupiga watu mawe watakaoenda kupiga kura, kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho P3 : kweli
Mhe. Lissu: na huo ulikua ni uamuzi wako binafsi, kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho P3 : Lakini kutoka na ushawishi wako.
Mhe. Lissu: kuna mahali popote katika maelezo yako umesema Mwenyekiti Tundu Lissu amesema tupige watu mawe?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Part 205 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 203
Mhe. Lissu anaendelea na Cross Examination,
Jaji Ndunguru: upande wa mashitaka.
Mkude: No objection.
Jaji Ndunguru : turejee kifungu 194 cha CPA.
Mkude: kifungu cha 194 kwa ujumla wake ni kuhusu protection ya ushahidi, kwa sababu shahidi au mshitakiwa anaweza akaomba impeachment, pale anapoomba shahidi apewe kielelezo hivo tunaweza kuendelea mheshimiwa Jaji.
Mhe.Lissu: Iko hivyo waheshimiwa Majaji, sikuwa nataka kuona jina lake kwenye kielelezo hicho bali nataka asome maelezo yake.
Mhe.Lissu: kwa hiyo shahidi ulitaka kuficha ukweli mahakamani.
Shahidi wa kificho P3 : hapana.
Mhe.Lissu: mbona haukusoma kama wewe ni mwanachama wa CHADEMA na umeiandika kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P3 : mimi ni mfuasi wa CHADEMA labda askari aliyeandika maelezo yangu alikosea.
Mhe.Lissu unaidanganya mahakama, soma kama ilivoandikwa.
Shahidi wa kificho P3 : mimi ni mfuasi/ mwanachama wa CHADEMA.
Mhe.Lissu: Sasa ulikuwa unaficha nini. Shahidi swali langu la pili kwenye maelezo yako umesema kongamano hilo halikufanyika kwa sababu tulitawanywa uwanjani.
Sasa waeleze waheshimiwa Majaji kama kwenye maelezo yako kuna sehemu umeandika kuwa kongamano hilo halikufanyika kwa sababu tulitawanywa uwanjani.
Shahidi wa kificho P3 : kongamano hilo halikufanikiwa.
Mhe.Lissu: hayo maneno yapo au hayapo.
Shahidi wa kificho P3 : hayapo.
Mhe.Lissu: shahidi umesema kwa bahati mbaya au nzuri kongamano hilo halikufanyika lilizuiliwa na serikali kweli au si kweli.
Shahidi wa kificho P3 : kweli.
Mhe.Lissu: wewe mfuasi wa CHADEMA kongamano la CHADEMA shughuli halali ya chama kuzuiliwa kwako ni bahati nzuri.
Shahidi wa kificho P3: sijui, mimi sielewei
Mhe.Lissu: ndiyo maana nikakuuliza tutajuaje kama wewe siyo pandikizi.
Shahidi wa kificho P3 : hilo swali nimeshalijibu tuendelee.
Mhe: Lissu: usijali tutaendelea kwenye maelezo yako ya Leo umesema ulikuwa na simu, Sasa kwenye hayo maelezo yako ya Polisi kuna sehemu uliandika kama ulikuwa na simu.
Shahidi wa kificho P3 : haipo.
Mhe.Lissu: waeleze waheshimiwa Majaji kama unajua au haujui kuwa unaweza kufuatilia YouTube kwa kutumia compyuta.
Shahidi wa kificho P3 : sijui, mimi sina utaalamu huo wa kutumia compyuta.
Mhe.Lissu: waeleze waheshimiwa Majaji kama unajua kuwa unaweza kufuatilia YouTube kwa kutumia Television.
Shahidi wa kificho P3 : utaalamu huo sina.
Mhe.Lissu: unajua kama unaweza kufuatilia YouTube kwa kutumia tablet.
Shahidi wa kificho P3 : sijui huo utaalamu.
Mhe.Lissu: Kwenye maelezo yako kuna sehemu umeandika kuwa ulikuwa na simu
Shahidi wa kificho P3 : hapana
Mhe.Lissu: kwenye maelezo yako umesema uliyasikia maneno yangu kupitia video YouTube, kuna mashahidi wengine wamesema video hiyo ilikuwa na masaa 3 na madakika, waeleze waheshimiwa Majaji kama kuna sehemu umeandika video hiyo ilikuwa na muda gani.
Shahidi wa kificho P3 : hakuna
Mhe.Lissu: umesema umemfahamu mheshimiwa Lissu kupitia mitandao ya kijamii. Waeleze waheshimiwa Majaji kama kwenye maelezo yako umeandika hilo jambo.
Shahidi wa kificho P3 : hapana hayapo.
Mhe.Lissu: umesema mwezi march 2025 ulihudhuria mkutano uliohutubiwa na Mheshimiwa Tundu Lissu katika viwanja vya Ruanda nzovwe, waeleze waheshimiwa Majaji kama hayo maneno yapo kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P3: hayapo
Mhe.Lissu: umesema wakati ukiwahamasisha vijana wenzako hapo kijiweni alikuja mtu aliyejitambulisha kuwa ni Askari Polisi na kukuita pembeni kwamba njoo tuongee, waeleze waheshimiwa Majaji kama hayo maneno yapo kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P3 : napitia kidogo
Mhe.Lissu: haujapaona hadi mwishoni kwenye paragraph ya mwisho.
Shahidi wa kificho P3 : naomba nikusomee, alikuja mtu aliyejitambulisha ni Askari Polisi.
Mhe.Lissu: swali langu ni kwamba hayo maneno akaniita pembeni akaniambia njoo tuongee, hayo maneno yapo au hayapo.
Shahidi wa kificho P3 : hayapo.
Part 204 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 202
Mhe. Lissu ameanza kumfanyia Cross examination Shahidi wa kificho P3.
Mhe. Lissu: shahidi hapo ulipo unaweza kuniona?
Shahidi wa kificho P3 : hapana
Mhe. Lissu: kwa taarifa yako hata mm siwezi kukuona kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P3 : sahihi.
Mhe. Lissu: nataka nikuhoji kutokana na ushahidi wako na nashukuru umesema wewe ni mfuasi wa CHADEMA, sasa naomba uwaeleze majaji, mfuasi wa CHADEMA anakua na kutambulisho gani?
Shahidi wa kificho P3 ; anakua hana kitambulisho kwasababu anakua bado hajawa mwanachama.
Mhe. Lissu: mimi kiongozi wa CHADEMA na mtu yoyote aliyeopo hapa mahakamani atajuaje kama wewe ni mfuasi wa CHADEMA, huna kitambulisho na pia sikuoni?
Shahidi wa kificho P3 : hilo ni suala la imani
Mhe. Lissu: twende taratibu kaka, waeleze majaji kama wafuasi wa chadema huwa wanaorodheshwa mahali ili kuwatambua.
Shahidi wa kificho P3 : binafsi sijajua huwa wanaorodheshwa wapi?
Mhe. Lissu: kwahiyo hujaorodheshwa?
Shahidi wa kificho P3 : sahihi.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama wafuasi wa CHADEMA kuna mahali huwa wanaenda kujitambulisha ili wajulikane
Shahidi wa kificho P3 : hakuna.
Mhe. Lissu: hapo ulipo kwenye kiboksi na mimi hapa nilipo kama kuna namna mimi naweza nikaelewa au kujua kama wewe ni mfuasi wa CCM na sio CHADEMA?
Shahidi wa kificho P3 : sijui utajuaje ila mm ni mfuasi wa CHADEMA
Mhe. Lissu: na nitajua kama ww sio pandikizi la Polisi kwasababu hujajiandikisha popote wala huna chochote cha kukutambulisha kuwa ni mfuasi wa CHADEMA?
Shahidi wa kificho P3 : itabidi uamini tu na uiamini mahakama tukufu kwasababu mimi sijui kwa kweli utawezaje kunitambua.
Mhe. Lissu: mfusi wa CHADEMA huwa anaalama usoni au kifuani kuwa yeye ni mfuasi wa CHADEMA?
Shahidi wa kificho P3: sijui
Mhe. Lissu : waeleze majaji kama uliandika maelezo Polisi tarehe 17 april 2025?
Shahidi wa kificho P3 : ndio
Mhe. Lissu: ukionyeshwa hayo maelezo yako utayatambua?
Shahidi wa kificho P3 : ndio
Mhe. Lissu: naomba shahidi apewe maelezo yake ya tarehe 17 april 2025.
Mkude: Hatuna pingamizi.
SHAHIDI ANAPEWA MAELEZO YAKE.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama hayo ndio maelezo uliyoyaandika tarehe 17 april 2025?
Shahidi wa kificho P3 : ngoja kidogo nayapitia.
Mhe. Lissu: waeleze waheshimiwa majaji kama hayo ni maelezo yako?
Shahidi wa kificho P3 : ndio yenyewe
Mhe. Lissu: waheshimiwa majaji nataka ku-impeach credit ya shahidi huyu, nitamsomea maelezo yake, nitaonyesha maeneo ambayo nataka kumhoji halafu nikimaliza nitakuomba uyawasilishe kama kielelezo.
Shahidi wa kificho P3 : sawasawa.
Mhe.Lissu: anamsomea shahidi maelezo yake.
Mhe.Lissu: waeleze waheshimiwa Majaji kama nilichokisoma ndicho kilichoko kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P3 : ndiyo ulichokisoma ndicho kilichoko kwenye maelezo yangu.
Mhe.Lissu: Sasa shahidi nataka nikuhoji kwenye eneo unalosema wewe ni mfuasi wa CHADEMA na maeneo mengine kadri nitakavyokuhoji kutokana na ushahidi wako.
Mheshimiwa Lissu anamsomea shahidi maeneo yote anayotaka kumhoji.
Maeneo 8.
Mhe.Lissu: Sasa hili nikuhoji sawasawa naomba uwaeleze waheshimiwa Majaji kama ungependa maelezo yako yapokelewe kama kielelezo mahakamani.
Shahidi wa kificho P3: ndiyo napendelea iwe hivyo.
Mhe.Jaji: itakuwa D12
Mhe.Lissu: ahsante waheshimiwa Majaji, naomba shahidi apewe kielelezo D12
Mhe.Lissu: Sasa swali langu la kwanza ni kwamba kwenye ushahidi wako leo umeieleza mahakama kuwa wewe ni mfuasi wa CHADEMA tangu mwaka 2021, ni kweli au si kweli.
Shahidi wa kificho P3 : ni kweli.
Mhe.Lissu: kwenye kielelezo D12 wasomee waheshimiwa Majaji pale unapoanzia mimi pia ni........ endelea hadi nitakapokwambia inatosha.
Shahidi wa kificho P3 : mimi pia ni mfuasi wa chama hicho.....
Shahidi anasitasita katika kusoma.
Mhe.Lissu: naomba pia nipewe kielelezo hicho naona kama shahidi anatupoteza.
Part 203 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 197
Katuga anasema: Kuna chama kinasema lazima mashahidi wote wa kificho watajulikana, sisi ni rai yetu kwamba ipo siku hata mimi nitakuja kuambiwa nilishawahi kuwa shahidi wa kificho, kwahiyo tunaomba mahakama itolee maamuzi ili kuondoa shida ya kupunguza uaminifu wa mahakama;
Wengine ni mawakili kabisa wanazungumzia hii kesi kwa upotoshaji tena ni wanasheria wakubwa kabisa wanaheshimika katika jamii.
Mhe. Lissu anasimama: waheshimiwa majaji mimi nawaomba msikubali huo mualiko mnaopewa na mawakili wa serikali, malalamiko yao ni malalamiko ya kijinai ambayo hayajafanyika mbele yenu, hamjayaona, hamjayasikia na wala hamjaambiwa ni kitu gani, Hayo mambo yote hayajatokea mbele yenu mahakama ikiwa inaendelea.
Mkiambiwa mtolee maamuzi juu ya mambo hayo mtakua mmefungua mambo yasiyowezekana.
Kama wanahisi kuna jinai waende kwenye mahakama proper wakafungue kesi, kama ni mawakili kuna utaratibu wa kudeal na mawakili wanaokiuka taratibu za kiuwakili.
Kwahiyo mnaalikwa kwenye uwanja ambao hauna rules, sio uwanja wa kisheria.
La mwisho na hii ni hofu yangu wanataka giza katika kesi kubwa kama hii, kwenye kesi ya uhaini hawataki kuwe na mjadala wanazungumzia Umma kitu ambacho hakiwezekani, mnataka kuwafunga, mtafunga nchi nzima na hamtaweza. Ni hayo tu waheshimiwa.
Katuga anasimama: tuliialika mahakama chini ya kifungu 114, sisi tunasisitiza vinavyoendelea ni kutoa uthibitisho wa mashahidi wa kificho na sisi inatupa shida katika kuleta mashahidi wetu, tusipovisema ivi vitu proceedings hazitakuwa sawa.
Kuna vingine hatuvisemi kwanini mashahidi hawaji yeye anaulizia kila siku lakini ni vitu kama hivyo.
Katuga anadai hizi proceedings za kinachondelea Mahakamani zinachapishwa pia mtandaoni sasa hii haiwezi kuwa sawa.😂
Mawakili wa Serikali wanataka kesi iwe Gizani mazima ili Watanzania na Dunia isijue nini kinaendelea kwenye shauri hili.
Kwa kifupi hawa ndugu wmaechanganyikiwa na mambo yanavyokwenda. Wanaona wako uchi kabisa. Kila kitu chao kiko hadharani. Naona hapa wanataka kusema mashahidi wanagoma kuja kwasababu wanaogopa kuwekwa hadharani.
Nafikiri wangekuwa wakweli waseme mashahidi wanaogopa kudhalilishwa hata kama hawaonekani kwenye kile kibox chao. Naona joto la mle kwenye mambao ukichanganya na maswali wanahadisiana huko waliko. 😂😂
Kumbuka hizo discussion Majaji wamesema wanazifanya off record kwanza. Ni kama zinapigwa soga ili kuona ni vitu vya msingi au sio vya msingi. 😂
Majaji wamemaliza kuteta sasa.
Jaji Nduguru anasema amesikia hoja zote anasema siku zote anasisitiza Matumizi ya kifungu 114 kama kunamambo hayako sawaa hawawezi kusubiri mtu aliibue jambo hilo. Wao pia wanaona na watachukua hatua.
Hivyo anaendelea kusisitiza kifungu Cha 114 na kusema tujiepushe na uvunjifu wa kifungu hicho.
Matumizi ya kifungu Cha 114 ni domain ya Mahakama itatumia kifungu hicho endapo itaona kunaulazima wa kukitumia hivyo tuendelee mashahidi.
Wakili wa Serikali anasemaa anasema tuendelee na mashahidi Leo ni shahidi wa wazi wa 12 wa upande wa mashitaka.
Kwa Maneno mengine tukitafsiri kilichosemwa na Majaji ni kwamba wamewaambia Jamhuri acheni umbea. Fanyeni Kesi. Msitufundishe kazi. Tunajua tunachofanya. 😂😂😂
Wamenywea sana hapa.
Ngoja tukomae na huyo Polisi anaekuja muda huu.
Part 198 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
@HildaNewton21 Kwwni shida ninini lakini? Kwsni jamhuri dhidi ua Lissu maana yake watu wa jamhuri dhidi ya Lissu, kwani watu wa jamhuri hii ninani hasa? Sio sisi wananchi? Kwanini akina katuga hawataki sie watu wa jamh7ri hii tuzungumzie maswala ya kesi hii? Aisee! it doesn't work that way.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 189
Wakili wa Serikali anaendelea kumuongoza shahidi wa kificho P4
Wakili: Nini kingine?
Shahidi wa kificho P4 : Tulivyoenda kuripoti Tarehe 17/04 tuliambiwa tusubiri tuandikwe maelezo, nikaandikwa hayo maelezo.
Wakili: Unamfahamuje huyo Tundu Lissu?
Shahidi wa kificho P4 : Namtambua kama Mwanasiasa Mkubwa kwenye hii Nchi.
Wakili wa Serikali Winiwa Kasawa anasema Waheshimiwa Majaji ni hayo tu.
Jaji Ndunguru: Maswali ya Dodoso Karibu Mshitakiwa.
Mhe. Lissu: Sasa shahidi jibu maswali kama hujui sema hujui sema najua kama unajua na kama umesahau sema nimesahau.
Mhe. Lissu: Umesema unakaa Arusha?
Shahidi wa kificho P4 : Kweli
Mhe. Lissu: Wambie Majaji umekuja Dar es salaam lini?
Shahidi wa kificho P4 : Leo nina siku ya pili.
Mhe. Lissu: kwahiyo umekuja Jumapili ya juzi?
Shahidi wa kificho P4: Ndio.
Mhe. Lissu: Nani alikwambia uje Dar es salaam
Shahidi wa kificho P4 : Hiyo nashindwa kusema hapa.
Mhe. Lissu: Utasema tu. Mimi sikuoni na watu hawakuoni. Wambie majaji ndio wanaokuona pekee kuwa nani alikwambia uje Dar es salaam
Shahidi wa kificho P4 : Nilipigiwa simu.
Mhe. Lissu: Na nani alikupigia simu.
Shahidi wa kificho P4 : Mtu alijitambulisha kuwa ni Wakili wa Serikali.
Mhe. Lissu: Alikwambia jina lake?
Shahidi wa kificho P4 : Ninazo sababu binafsi
Mhe. Lissu: Kwahiyo majaji waandike kuwa umekataa kusema sababu kwanini hutaki kumtaja aliyekuita Dar es salaam sawa muraaaaa
Shahidi wa kificho P4 : Ndio.
Mhe. Lissu: wapo wakurya wenzako humu.
Mhe. Lissu: Ieleze Mahakama kama ulipata summons ya Mahakama?
Shahidi wa kificho P4 : nilipigiwa simu nikaenda kituoni nilipata barua ya Mahakama.
Mhe. Lissu: Nani aliyekulipia nauli ya kutoka Arusha Kuja Dar es salaam?
Shahidi wa kificho P4 : Nilikuja na nauli nililipa mwenyewe maana nilikuja kwenye shughuli zingine binafsi.
Mhe. Lissu: Una nyumba hapa?
Shahidi wa kificho P4 : Sina.
Mhe. Lissu: Nani anayelipa gharama za kula na kila kitu?
Shahidi wa kificho P4 : leo nimekuja na gari ya wanasheria
Mhe. Lissu: Tarehe 03/04/2025 ulipelekwa kituo cha Polisi mjini na kabla ulikuwa kituo cha Muriet
Shahidi wa kificho P4 : Ndio
Mhe, Lissu: Hayo maelezo yalikiwa yanahusu kosa gani?
Shahidi wa kificho P4 : Walisema tuna kesi ya kutaka kuzuia Uchaguzi.
Mhe. Lissu: umewahi kupelekwa Arusha kwa hilo kosa ulilokamatwa nalo?
Shahidi wa kificho P4: Sikuwahi kupelekwa Mahakamani.
Mhe. Lissu: Hiyo kesi iliishia wapi?
Shahidi wa kificho P4 : Mimi sijui.
Mhe. Lissu: Hayo maelezo ya Tarehe 03/04 yako wapi?
Shahidi wa kificho P4 : Sijui.
Mhe. Lissu: Nilikwambia kwamba ulikamatwa bure tu hukuwa na kosa lolote we utasemaje?
Shahidi wa kificho P4 : Sijui mimi.
Mhe. Lissu: Siku hiyo ya Tarehe 03/04 wewe na wenzako mlikuwa mnazungumza juu ya maneno mlioyaona kwenye mtandao na wengi mliyaunga mkono
Shahidi wa kificho P4 : Ndio.
Mhe. Lissu: Je hilo lilikuwa kosa nyie kuunga mkono na kuzungumza kauli hizo.
Shahidi wa kificho P4 : Sijui
Mhe. Lissu: Maelezo yako ya 17/04 ukionyeshwa unaweza kuyatambua?
Shahidi wa kificho P4 : Naweza
Shahidi wa kificho P4 ameyatambua maelezo yake na Mh. Lissu anamsomea Maelezo ambayo shahidi aliyaandika pale Polisi.
Mhe. Lissu: Niliyosoma hapa ni sawa na maelezo uliyonayo hapo.
Shahidi wa kificho P4 : Ndio
Mhe. Lissu: Sasa shahidi nataka kukuhoji kuhusu hayo maelezo.
Shahidi wa kificho P4 : Sawa.
Mhe. Lissu: Maeneo hayo ni
1. Uliperuzi kwa simu yako
2. Nilisema tutakinukisha
Anamtajia maeneo kama 8 hivi ambayo atamuuliza maswali.
Mhe. Lissu: Je ungependa yawe sehemu ya ushahidi?
Shahidi wa kificho P4 : ndio.
Jaji: Jamhuri mnasemaje?
Wakili Renatus: sina pingamizi.
Jaji: Hiyo itakuwa ni D9 upande wa utetezi.
Part 190 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 187
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi ASP Geofrey Lutufye.
Mhe. Lissu: Mnajifanya mapolisi mnawasingizia watu vitu vya bure haya itakushangaza hao mliowakamata baada ya kesi yao kuisha ni mashahidi wa kesi hii?
ASP Geofrey Lutufye : Hainishangazi.
Mhe. Lissu: haikushangazi kwasababu huo ndio utaratibu wenu mapolisi wa Tanzania.
Mhe. Lissu: Au unabisha nikufungulie ripoti ya Jaji Mkuu Othman Chande amesema mnawafungulia watu makosa ya uongo.
Sasa nikuulize swali lingine, umewahi kuona video mimi nikiwa nazungumza habari za huo uchaguzi mkuu?
ASP Geofrey Lutufye : amekaa kimya
Mhe. Lissu: Unajua kwanini nimeshitakiwa kwa Uhaini ASP geofrey lutufye? Unajua sababu.
ASP Geofrey Lutufye : Sababu ya ile kauli uliyotoa.
Mhe. Lissu: Ipi hiyo?
ASP Geofrey Lutufye : Ulisema utazuia uchaguzi wa mwaka 2025.
Mhe. Lissu: Ndio nakuuliza uliiona hiyo video?
ASP Geofrey Lutufye : Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Hawa ndio kesho watakuwa ma RPC siku inayofuata utashangaa anakuwa IGP,
Sina maswali mengine Waheshimiwa majaji.
Watu wanasonya tu hapa.
Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude kwa ajili ya Re-examination
Maelezo yako uliandika kama nani?
ASP Geofrey Lutufye : Kama shahidi.
Wakili: Unalizungumziaje kuhusu kujiandika mwenyewe?
ASP Geofrey Lutufye : naweza kujiandika mwenyewe au kuandikwa.
Renatus Mkude: Sina swali lingine. Re Examination imeishia hapo.
Jaji anamruhusu Shahidi.
Shahidi anatoka akiwa ameshika kipaza sauti.
Jaji Ndunguru: Unasahau maji yako hapo.
Shahidi: Hapana siyataki tena.
Jaji: Basi turudishie hiyo MIC tafadhali.
Anairudisha na kutoka nje akiwa anatikisa kichwa.
Watu wanacheka.😂😂😂
Kesi inaahirishwa watu wakale.
Tutaendelea baada ya lisaa limoja.
Naomba repost yako.
MAHAKAMA KUU YAFUTA MATUMIZI YA MASHAHIDI WA KIFICHO
Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Mwanza imetoa uamuzi wa kuzuia upande wa Jamhuri kutumia mashahidi wa kificho au siri katika kesi zote za jinai, ikitangaza kuwa utaratibu huo ni kinyume cha katiba ya nchi.
Mhe. Lissu: Polisi walikwambia ukiwa shahidi kwenye kesi hii watakufutia mashitaka yako si ndio?
Shahidi wa kificho P6: Hapana Mheshimiwa we acha tu. 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Elimu ya bure kwa mr President chapa reposti 100 kwaeshima 😂😂😂
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 173
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa kificho P6.
Mhe. Lissu: Pameandikwa tarehe 06/04 kutakuwa na ziara ya Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Songea, umeona vizuri hapo.
Shahidi wa kificho P6: Naweza kurudia pia wilaya ya songea anaisoma. 😂
Shahidi ni kama Futuhi kwakweli.
Mhe. Lissu: Twende Tarehe 10/04 umesema hivi ukiwa umekusanyika uwanja wa shule ya Msingi Matalawe na kuwataja viongozi ghafla gari ya polisi ilifika na kuwatawanya. Waeleze majaji kama hayo maneno gari la polisi lilifika na mkatawanywa.
Shahidi wa kificho P6: Hayapo hayo.
Mhe. Lissu: kuhusu kwenda ofisi za Chama Mfaranyaki mlikoenda na viongozi wakataka kuzungumza na waandishi wa Habari kuwa polisi walifika na kuwapiga mabomu?
Shahidi wa kificho P6: Kutupiga mabomu hayapo kwenye maelezo.
Mhe. Lissu: Je wapi kuna maneno kuwa polisi waliwatawanya ofisi za Chama.
Shahidi wa kificho P6: Hayapo kwenye maelezo yangu.
Mhe. Lissu: Sasa ngoja nikuulize mengine baada ya kumaliza kukutembeza kwenye maelezo yako.
Mhe. Lissu: Kwa ufahamu wako Kiongozi wa Chama kama mimi kuitisha mkutano na kusema bila mabadiliko hakuna uchaguzi ni kosa la jinai?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu mimi.
Mhe. Lissu: Kusema tutazuia uchaguzi nalo ni kosa la jinai?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu pia.
Mhe. Lissu: unafahamu hakuna sheria yoyote nchi hii inayokataza kuzuia uchaguzi?
Shahidi wa kificho P6: Huko kwenye sheria mimi sifahamu.
Mhe. Lissu: Polisi hawakukwambia kuwa sio kosa? Hao waliokuwa wanakufundisha kuja kusema hapa.
Shahidi wa kificho P6: amenyamaza
Mhe. Lissu: Ulisema mikutano ya Songea ilizuiwa kufanya mikutano na kupigwa mabomu. Je hiyo ni sawa na ni haki ya kisheria kwa Chama?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Mhe. Lissu: unafahamu polisi wa Tanzania hawana mamlaka ya kukataza mikutano?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Mhe. Lissu: Unajua Mikutano hiyo ilitolewa taarifa siku mbili nyuma?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Mhe. Lissu: Kwani wewe si ndio umesema ulikuwa umehamasika na Chadema?
Shahidi wa kificho P6: Ndio hivyo sasa sifahamu.
Mhe. Lissu: Ulivaa tshirt imeandikwa No Reforms, No Election ni kosa?
Shahidi wa kificho P6: sifahamu.
Mhe. Lissu: Ulikamatwa Tar. 20/04/2025 mkiwa katika eneo la DS Kitimoto mkakamatwa kwa tuhuma za kufanya maandamano yasiyo ha hiari ni kweli?
Shahidi wa kificho P6: kweli
Mhe. Lissu: maelezo ya hayo mahojiano yako wapi?
Shahidi wa kificho P6: sifahamu.
Mhe. Lissu: Hizo tuhuma ziliishia wapi za kutaka kufanya maandamano na kuhojiwa?
Shahidi wa kificho P6: ndio tulipelekwa Mahakamani ila kaka angu alikuwa ananiwakilisha.
Mhe. Lissu: Kwahiyo Kaka yako alishtakiwa badala yako?
Shahidi wa kificho P6: ndio yeye alikuwa anaisimamia
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji ilikuwaje ukabadilika kuwa mtuhumiwa wa kupanga njama za kufanya maandamano na leo ukawa shahidi?
Shahidi wa kificho P6: Hata mimi sijui nini kilitokea.
Mhe. Lissu: Polisi walikwambia ukiwa shahidi kwenye kesi hii watakufutia mashitaka yako si ndio?
Shahidi wa kificho P6: Hapana Mheshimiwa we acha tu.
Mhe. Lissu: Wewe ni Mwanachama wa Chadema?
Shahidi wa kificho P6: Ndio.
Mhe. Lissu: Umeingia lini? Niambie tarehe na mwezi.
Katuga amesema hilo swali akijibu ataweza kujulikana maana kwenye mfumo wanajulikana watu waliosajiliwa ni akina nani siku fulani.
Majaji wamejadili kama dakika tano. Tunasubiri watasema nini?
Part 174 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 169
Mazingira aliyokuwa anayatolea ilikuwa ni kama sehemu ya Ukumbini, ndo nilimuona hapo.
Muda huu ameingia Mtaalamu, Wakili Msomi Peter Kibatala wakati kesi inaendelea.
Amekaa pale karibu na Kizimba cha Mhe. Tundu Lissu, nimeona wanasalimiana kimya kimya Mhe. Lissu anacheka anamuonyeshea kidole cha Upendo ni kama anamwambia wewe kijana wangu wewe.😂
Wakili wa Serikali: Muonekano wa Lissu ulikuwaje?
Shahidi wa kificho P6: Alivaa Kombati ya Kaki.
Namfahamu Tundu Lissu kama mwanasiasa mkongwe na mwanasiasa maarufu.
Wakili: Baada ya kuona hiyo hotuba wewe ulifanya nini?
Shahidi wa kificho P6: Nilivyoona hiyo video maneno yake yaliniingia moyoni na kunishawishi.
Hiyo agenda ya kukinukisha ni kufanya vurugu au kuharibu miundombinu.
Wakili: huo uchaguzi ni upi?
Ukisikiliza majibu ya huyu Shahidi wa kificho ni wazi kaingia na desa anasoma majibu.
Anajibu hapa ni Uchaguzi Mkuu wa 2025 unaohusisha wabunge na Rais na Madiwani.
Wakili: Ikawaje baada ya kushawishika?
Shahidi wa kificho P6: Nikamfuata Mwenyekiti wa Vijana wa Songea alikuwa anaitwa Chiza maarufu kama Mwamba wa Kigoma.
Wakili: ikaendelea nini?
Shahidi wa kificho P6: Nikamueleza nilivyoshawishika na maneno ya Mwenyekiti na kutaka kuwa miongoni mwa watu tutakaokinukisha.
Wakili: Kikaendelea nini?
Shahidi wa kificho P6: Alinisifia sana kwa uamuzi mzuri na wakishujaa na akanipongeza na kuniambia Vijana kama nyie ndio vijana mnaotakiwa kulikomboa Taifa.
Wakili: Nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Aliniambia ataniunganisha kwenye magroup yanayojadili mipango ya kuzuia Uchaguzi, akaniunga Group la SIASA YETU.
Group lilikuwa linaitwa SIASA YETU UPDATES.
Wakili: Nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Niliendelea na shughuli zangu na yeye akaendelea.
Tarehe 06/04/2025 nilipata taarifa kuwa Mwenyekiti wa Chadema atakuwa ziarani mkoani Ruvuma.
Wakili: Mwenyekiti ni nani?
Shahidi wa kificho P6: Ni Mh. Tundu Lissu, hiyo taarifa nilipata kutoka kwa ndugu Chiza.
Wakili: Ikakutaka ufanye nini?
Shahidi wa kificho P6: Ilitutaka tufanye maandalizi na tarehe 10/04 atakuwepo Songea.
Wakili: Mlipanga nini kuhusu mkutano?
Shahidi wa kificho P6 ; Tulipanga mkutano ufanyike uwanja wa matalawe. Tarehe 09/04/2025 nilipata taarifa kuwa Mwenyekiti amekamatwa Wilaya ya Mbinga akiwa kwenye ziara ya Mikuta.
Watu wanashangaa mikuta ndio nini? Mashahidi wa siri wanasoma.. 😂😂😂
Shahidi wa kificho P6: Nilimtafuta Chiza kumuuliza kuhusu taarifa za Mwenyekiti kukamatwa Wilaya ya Mbinga.
Wakili: ikawaje?
Shahidi wa kificho P6: Akanijibu ni kweli amekamatwa lakini ratiba ya Mkutano wa Tarehe 10/04/2025 itakuwepo palepale. Kwahiyo jiandae kuwepo eneo la Mkutano Tarehe 10.
Wakili: hiyo Tarehe 10 sasa nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Tulikusanyika uwanja wa Matalawe kusubiri viongozi walioambatana na Mwenyekiti kuhutubia mkutano.
Alikuwepo Godbless Lema na Dr. Wilbroad Slaa pia alikuwepo Mh. Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Mh. Heche.
Wakili: nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Wakati tunasubiria likatokea gari ya Polisi na kusema kwa siku hiyo hakuna mkutano utakaofanyika eneo hilo. Na haruhusiwi mtu kukaa eneo hilo.
Wakili: nini kikaendelea?
P6: Ikabidi tutawanyike na kuelekea ofisi za Chama ili tufahamu kwa siku hiyo nini kitaendelea?
Wakili: Ziko wapi hizo ofisi?
P6: Ziko Songea sehemu inaitwa Mfaranyaki.
Wakili: kikaendelea nini?
P6: tuliwakuta viongozi ambao ni Adel Mayala ambae kwa wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini.
Wakili: Nini kiliendelea?
P6: Wakaja Polisi wakapiga mabomu ya machozi na kusema watu wote watawanyike.
Wakili: Saa saba mchana nini kiliendelea?
P6: Alikuja kiongozi Makamu Mwenyekiti na kusema kwamba amepokea barua kutoka Polisi kwamba kwa siku hiyo usifanyike Mkutano wa aina yoyote katika eneo hilo.
Wakili: Akasema nini kingine?
Part 170 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.