Kesi ya Tundu Lissu ni fedheha kwa Taifa letu. Lakini pia ni kipimo cha uwezo wa majaji wetu kusimamia haki na boldness ya kulinda hadhi ya mhimili wa mahakama.
TAFAKAURI YETU WANANCHI
Kama JAJI Ndunguru ni Mteule wa RAIS Anawezaje kutenda HAKI kwenye kesi ambayo SAMIA ni mnufaika ?
WANANCHI sio wajinga kiwango hicho kama wasidizi wa Rais ambao hawana kinga kisheria ila MAHAKAMA inaogopa kuwaandika summons kunaDALILI za HAKI hapo ?
Sijashangaa Twaha Mwaipaya kukatwa kugombea ujumbe wa CC.
Mwaipaya ni askari mwaminifu sana pale CDM.
Ila Freeman Mbowe hataki agombee ujumbe CC.
Anahitaji CC ya watu wepesi anaowamiliki.
Mzee @freemanmbowetz, haujabakiza aibu kiasi kulinda legacy yako? Shame on you.
TUJIELIMISHE ILI KUJISAHIHISHA.
KESI YA LISSU: HAKUSHINDWA BALI MAHAKAMA ILIAMUA KUWA ANA KESI YA KUJIBU HIVYO UTETEZI UNAFUATA.
Pamoja na kuheshimu uamuzi wa Mahakama, mimi ninaendelea kuhimiza busara na hekima zitumike katika ngazi zote za maamuzi ili taifa letu liondokane na jambo hili la kusikitisha. Tuweze kuambizana ukweli, kusameheana na kuridhiana.
Sizungumzii hatia au kutokuwa na hatia kwa Lissu; hilo ni jukumu la Mahakama. Ninazungumzia mazingira ya kesi hii, historia yetu na umuhimu wa sheria kutumika kwa usawa. Tutambue:
1. Kesi ya Tundu Lissu ina tofauti kubwa na kesi nyingi za uhaini zilizowahi kutangulia hapa nchini. Katika kesi hizo za kihistoria kulidaiwa kuwepo njama, washirika, mipango ya pamoja ya kuipindua Serikali, na katika baadhi ya kesi washirika kutoka jeshini na madai ya kupanga kumuua Rais.
Katika kesi hii Lissu ameshtakiwa peke yake, na kiini cha shtaka kinahusu kauli zake za hadharani. Hii ni tofauti muhimu inayostahili kutafakariwa bila kuingilia kazi ya Mahakama.
2. Lissu anashitakiwa kwa uhaini chini ya kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, kutokana na kauli alizotoa katika mkutano wa CHADEMA tarehe 3 Aprili 2025. Kaulimbiu yake ilikuwa “No Reforms, No Election.” Upande wa mashtaka unadai kwamba kauli zake kuhusu “kukinukisha”, kuzuia au kuvuruga uchaguzi zilivuka mipaka ya siasa za kawaida.
Kauli hizo ni kali. Lakini katika historia ya siasa zetu tumewahi pia kusikia kauli kali zaidi. Mfano wimbo maarufu: “Wapinzani tuwashike, tuwachanechane, tuwatupe.”
Hata Bungeni wimbo huo uliwahi kulalamikiwa lakini ikachukuliwa ni utani wetu wa jadi. Pia mitandaoni leo tunasikia kauli za kutishia watu, kuwaua au kuwapoteza bila hatua zinazoonekana kuchukuliwa kwa kiwango sawa.
Ndiyo maana wapo wananchi wanaojiuliza: Je, sheria inatumika kwa usawa kwa kauli za wanasiasa wa pande zote? Bibi yangu aliwahi kunikanya kuwa :Ukitania uwe tayari kutaniwa".
3. Lissu alitoa matamko yake hadharani au katika mikutano ya kisiasa. Wananchi wengi waliyasikia na wanayajua. Kwa hiyo, pamoja na kuacha Mahakama ifanye kazi yake kwa uhuru, ni vigumu kuzuia mjadala wa wananchi kuhusu jambo ambalo liko hadharani na linagusa siasa, sheria na haki za kiraia.
Ili mradi staha izingatiwe na mjadala huo usibadilishwe kuwa hukumu ya hatia au kutokuwa na hatia kabla ya Mahakama kumaliza kazi yake.
4. Kama Mahakama ingelikuwa imeamua kuwa hakuna kesi ya kujibu, hatua ya utetezi isingefunguliwa. Sasa Lissu ameomba kuwaita baadhi ya viongozi wakuu, akiwemo Rais Samia na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, kutoa ushahidi.
Historia ya nchi nyingine inaonyesha kuwa jambo la Rais aliye madarakani kutoa ushahidi katika shauri la jinai lina utata lakini si geni kabisa.
Mwaka 1807, katika kesi ya uhaini ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani Aaron Burr, Burr aliomba ushahidi kutoka kwa Rais Thomas Jefferson, bosi wake. Jaji Mkuu John Marshall ndiye alikuwa muamuzi na alikataa "dhana kwamba Rais ana kinga ya moja kwa moja dhidi ya mchakato wa Mahakama pale ushahidi wake unapohitajika katika kesi ya jinai".
Jefferson hakulazimishwa kusimama mwenyewe kizimbani, lakini alitoa ushahidi kwa nyaraka na kanuni muhimu ikawa: hadhi ya Urais haimaanishi kwamba ushahidi muhimu kwa mtuhumiwa hauwezi kupatikana.
Baadaye, Marais wengine wa Marekani wamelazimika kutoa ushahidi au taarifa katika mashauri ya jinai inapohitajika. Ni pamoja na:
James Monroe — 1818
Ulysses S. Grant — 1876
Gerald Ford — 1975
Jimmy Carter — 1978
Jimmy Carter tena — 1980
Bill Clinton — 1996
Richard Nixon mwaka 1974 aliamriwa kutoa kanda za Watergate.
Mara nyingi ushahidi huo ulitolewa kwa maandishi, nyaraka, viapo/deposition au video badala ya Rais kufika mwenyewe mahakamani.
5. Hakika Hatua inayofuata katika kesi ya Lissu ni nyeti. Itatuonyesha mwanga katika masuala haya muhimu kuhusu utawala wa sheria na haki ya mshitakiwa kupata utetezi stahiki.
6. Kiuhalisia Wengine tumejikita kwenye swala la HEKIMA, BUSARA na HURUMA YA MUNGU.
Barua ya Wazi kwa Ndugu @freemanmbowetz .
Ndugu,
Hongera sana kwa kula matunda ya kazi yako. Hakika unastahili.
Wako,
Ndugu, jamaa, na marafiki wa waliotangulizwa ili kukufanikisha.
madhara makubwa ninayoyaona mimi ya tabia na mwenendo mpya wa freeman mbowe ni kuwavunja moyo vijana na kuwafanya wasite kuunga mkono harakati za ukombozi. anathibitisha msemo usiyo sahihi wa 'siasa ni mchezo mchafu,' na kujenga kizazi 'apathetic.' labda hiyo ndo 'new mission.'