Akizungumza kwa njia ya Mtandao, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole amekosoa mchakato wa upatikanaji wa wagombea Ubunge kupitia CCM, akidai kuna mazingira ya upendeleo kwa Watoto na ndugu wa Viongozi
Polepole alisema “Haipendezi unatazama kwenye mchakato wa Ubunge ni Watu wa familia za Viongozi, hii nchi sio ya Kifalme, muwe na soni."
Zaidi soma
https://t.co/36ZjgO1WVi
#JamiiAfrica #JamiiForums #Demokrasia #UchaguziMkuu #Siasa #Uchaguzi2025
@mrembo_og Hilo lipo wazi huyo simba chawene nenda jimboni kwake kibakwe na mpwapwa yote pamoja kua ndio wilaya kongwe mkoa wa Dodoma km 60 tangu kuumbwa kwa ulimwengu hakuna rami
Kuna mambo yanaumiza, tuna Serengeti, Kilimanjaro, Zanzibar, Ngorongoro, Ruaha, Mafia na kadhalika, bado tunashindwa na nchi kama Afrika Kusini, imepokea watalii 8.92 milioni 2024, sisi tumepokea 2.14, hii haiko sawa. Tukisimamia tu utalii ipasavyo, tunaacha kabisa kukopa.
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kupita bila kupingwa kwa Mgombea wa CCM Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete si jambo la ajabu imekuwa ni kawaida kutokana na Wilaya ya Bagamoyo kuwa na Wingi wa Wananchama wa CCM.
Kikwete ameyasema haya leo Julai 31, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Viwanda Kwala, Kibaha mkoani Pwani ambapo Mgeni Rasmi amekuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, ameongeza kuwa hata katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na 2015 pia Ridhiwani Kikwete alipita bila kupingwa akiwa ni Mgombea pekee ndani ya Chama hicho cha CCM.
#MillardAyoUPDATES