#CCM yamjibu #NAPE hoja ya Ushindi katika chaguzi.
Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amos Makalla kimemjibu Mbunge wa Mtama Ndg. Nape Nnauye kuhusu imani yake juu ya ushindi katika chaguzi mbalimbali nchini. Ndg. Makalla amesisitiza kuwa CCM haihitaji mbeleko na itashinda kutokana na rekodi nzuri ya kuwaletea wananchi maendeleo. Aidha, amesisitiza kuwa kauli iliyotolewa na kiongozi huyo haikihusu Chama Cha Mapinduzi na ni mawazo yake yeye mwenyewe. CCM itaendelea kuheshimu demokrasia na maamuzi yeyote ya wananchi kupitia sanduku la kura kama ilivyo siku zote.
#CCMimaraSerikaliImara
#SamiaNiWetuSote
Mh. @Nnauye_Nape what is this !? Really unajivuna haya mbele ya cameras ? Then mnakuja kuhubiri haki na amani wakati mioyo na mikono yenu imejaa dhuluma! Hamtaishi milele... Hivi vyeo vinawasahaulisha kujua everything in this life is for rent.
Ila tunawashukuru kwa kuyasema hadharani.
Hivi mtu huwezi kula ukashiba ukaa kimya ili kesho ule tena gizani kama ulivyozoea mpaka upige kelele huko nje wenye njaa wakusikie kama ulikula mikuku jana yake? Nimeona video ya Pena nimesikitika sana. Anawapa shida tu wenzie kuanza kujieleza bila sababu zozote za msingi.
Hizi kauli zimetoka kwa waziri aliyewahi kusoma goli la mkono
-- Kushinda uchaguzi inategemea ni nani anayehesabu kura , sio kwamba ni zile kura zilizopigwa anayeamua ni yule anayehesabu ndiye anapanga mshindi
-- Mimi mbinu cha kushinda uchaguzi nazijua nyingi tu, uwa tunafanya kisha tunaomba Mungu atusamehe baada ya kufanya mbinu chafu
-- Mbunge wenu nitamfundisha namna ya kushinda uchaguzi nina mbinu nyingi pamoja na zile chafu , miminajua namna ya kushinda uchaguzi
-- Soko lenu ni millioni 300 , tutakwenda huko serikali kutafuta fedha, lakini nikikosa huko nina makampuni ya simu mawili tu yanaweza toa hii fedha ni kidogo sana sio lazima itoke serikarini ... tukumbuke haya makampuni yanatoa CRS na fedha nyingine yote yanampa waziri anayesimamia sekta hiyo tu inaacha maswali, kwa nini iwe kwa waziri wa mawasialino kama nia ni kusaidia bila kuomba chochote kwa waziri? Kuna email kutoka Barick iliwahi onyesha walivyokuwa wanamlipa IGP kinyume na taaritiba na wakasema ni rushwa kwenye hiyo email, Leo waziri wa mawasiliano anasema uwa anasaidia fedha na makampuni ya simu , hii inaitwa nini ?
MWISHO, CCM wanakataa #KatibaMpya kutokana na hoja kwamba wao ndio wanahesabu kura na Nape ameeleza hapo namna wanavyoshinda kwa halamu
Tupigania #KatibaMpya kuziba haya mashimo, wanasiasa wanaongea wazi wazi wanavyotupora chaguzi, uchaguzi ni mchakato wa wananchi kuchagua viongozi wao
#ChangeTanzania #WenyeNchiWananchi
🚨🚨 CCM ADMITTING RIGGING‼️🚨
“Quos Deus vult perdere, prius dementat”
Those whom God wishes to destroy, He first deprives of reason
Minister of Communications admitting to using “semi-legal” and illegal means to win elections in #Tanzania
Mungu anapoamua kukumaliza anakupiga upofu! 😃
Imagine kiongozi anaongea hadharani kutumia mbinu CHAFU katika uchaguzi na anajigamba kuwa ni mtaalam
Eniwei #TutaelewanaTu