Waziri Wa Mambo ya ndani acha Kuvunja Katiba.
MLINZI WA KATIBA ? AU MVUNJA KATIBA?
Waziri wa Mambo ya Ndani hana Mamlaka yeyote ya Kuzuia au kutozuia Mikutano ikiyoruhusiwa Kisheria. Aidha siyo jukumu la IGP kutoa vibali vya mkutano au ruhisa ya mkutano.
Mukutano ya ndani ya vyama inaratibiwa na vyama vyenyewe na Jukumu la Polisi nikutoa Ulinzi tu.
TLS imepokea kwa mshtuko taarifa hizi na tutakaa na kuona namna ambayo tutachukua hatua za kisheria za ndani ya nchi na nje ya nchi dhidi ya yeyote atakaye jaribu kutekeleza agizo hili Haramu na Batili kwa kukiuka Katiba na sheria za nchi.
Tafsiri
“Guardian of the Constitution… or Its Chief Violator?”
The Minister for Home Affairs has no legal authority whatsoever to prohibit or permit meetings that are lawfully allowed under the law. Equally, it is not the mandate of the Inspector General of Police (IGP) to issue permits or authorizations for meetings.
Internal meetings of political parties are regulated by the parties themselves, and the role of the Police is strictly limited to the provision of security and maintenance of public order nothing more.
The Tanganyika Law Society (TLS) has received these developments with profound shock and concern .
We shall convene urgently to determine appropriate legal measures, both domestically and internationally, against not only against this position but also against any individual or authority who will attempt to implement this unlawful and void directive, in blatant violation of the Constitution and the laws of the land.
BAK MWABUKUSI
PRESIDENT, TANGANYIKA LAW SOCIETY (TLS)
@Aloysious012894@AlexSamoja hizi vitu huwa mnaongea kwa kupata ushahidi halisi ama kuangalia movie?
na mnatumia sample gani?
kama ingekuwa kweli basi % ya watz tungekuwa na kasoro maana malezi ya single parent ndo makubwa zaidi hapa kwetu
Moja ya kitu kinaninyima usingizi recently ni hili swala la wanaharakati kuwa wanalipwa!! (Kama ni kweli)🤔
Hizo taasisi au watu binafsi wanaolipa wanaharakati, huwa wanatazama vigezo gani kukulipa?
Influence? au Numbers (Followers)
au uwezo wa kuongea na kuandika au engagement ya social media au nini?
Binafsi nimeanza hii course ya harakati tokea siku namaliza form six na kutoa wimbo wangu wa kwanza Tanzania (2007) nikiwa very young!
Hadi leo nina Teremsha bunduki 2026!
Miaka 19 kwenye hizi harakati
NA SIJAWAHI KUPEWA HATA SHING 10 TOKA KWENYE HIZO TAASISI!!
WALA KULIPWA NA MTU BINAFSI ILI NIFANYE HIKI NINACHOKIFANYA!!
Na kuna muda unakuwa na uhitaji haswa, tena sometimes ni uhitaji wa kufanya projects hizi hizi za kusaidia hizi harakati….. you just end up using your own pocket money!!
Kwenye hizi harakati nakutana na challenge nyingi, nakosa opportunities na michongo kwasababu naonekana niko against na gavoo na kuna muda napoteza hata kidogo nilichobakiza!!
Nabaki empty hadi familia inakwambia si utemane na hizo mbanga……nawajibu I WAS BORN TO DO THIS!!
Ni kama roho/nafsi inakataa ku-give up!!
Tunafanya haya kwa passion,
kuna a driving force tu inatusukuma kutetea, kukemea, kushauri na kupaza sauti tunapoona haki inakosekana, maendeleo hakuna, rushwa na ufisadi kwa viongozi vinakithiri, umasikini unazidi kwetu sisi raia, uongozi na utawala mbovu, shida za ajira na miundo mbinu, watu kutekwa, kufungwa na kuuliwa bila hatia na kucreate awareness kwa raia kuhusu issue za kisiasa na kijamii etc.
Nikisikia mtu anasema kuyafanya hayo ni unalipwa…..nawaza nakosa majibu!!
Wanatumia vigezo gani kukulipa?
Hebu mtu anieleweshe pengine napishanaga na gari la mshahara!!
Followers ninao (1.3M) influence pia si haba nikitoa miwa inapokelewa mtaani!! MBONA MIMI SILIPWI?
Nways tusiache hizi harakati hata kama hazitupi pesa kwa sasa, faida yake mbeleni ni kubwa zaidi kwa nchi nzima na vizazi vijavyo!!
Kama nimeandika kwa hisia sana ee?😁
Sikumoja mfalme aliwaita mawaziri wake 3 👑
akawaagiza kila mmoja achukue kiroba 🧺
Kisha aende kwenye bustani ya kasri 🌿
na akijaze kiroba hicho kwa matunda na mazao mbalimbali yaliyo mazuri 🍎🍇🍌
Aliwaambia pia kuwa hawapaswi kushauriwa na mtu yeyote katika kazi hiyo.
👇🏽👇🏽👇🏽
Hizi Ni Mbinu Za Kivita Ambazo Huwezi Fundishwa Shuleni:
1. Usipende kuwasha location ya simu yako kila mara.
2. Usipende kutembea mwenyewe nyakati za usiku.
3. Hakikisha kabla hujalala kuna mtu umempa taarifa au umemtakia usiku mwema na amejua upo wapi.
4. Wakija watu kukukamata hata wakijitamburisha kwamba wao ni Polisi hakikisha kuna mtu amejua, wakitaka kukuchukua kwa nguvu lia kilio cha kufiwa na mama.
5. Ukitongozwa na Binti au Binti akijilengesha kirahisi kaanae mbali.
6. Rafiki yako akikupigia simu mkutane, hakikisha kuna mtu amejua, anaweza akakamatwa yeye ili wakupate wewe.
7. Usipende kununua Luku kwa njia ya simu kwani, watekaji wana uwezo wa kujua unaishi maeneo gani kirahisi zaidi.
8. Ukipita maeneo ukiwa na mashaka chukua simu mpigie mtu uwe unatembea huku unaongea nae ukigushwa tu, mwambie huyo mtu kwamba unatekwa.
9. Usiishi kama mfu, muombe Mungu, pia ishi vizuri na watu watakusaidia siku moja.
UTAJUAJE KAMA UNAELEKEA KUPOTEZWA:
1. Hata kama umekamatwa na watu waliojitamburisha kwamba ni Polisi ila ukienda kituoni hautaingizwa kwenye reja book.
2. Ukiona umeenda kituo cha Polisi umewekwa chumba cha peke yako na vyumba vingine vikiwa na watu hakikisha ukipata upenyo unatoa ujumbe wakusema wewe ni nani na umetokea wapi, kwani hapo utakua umehifadhiwa tu wazee wa kazi watakuja kukuchukua.
3. Ukipandiswa kwenye gari utafungwa pingu na utawekwa katikati, kulia kwako na kushoto atakaa mtu, tambua haupo salama.
KWA LEO TUISHIE HAPA NINA ZAWADI YAKO👇
@MrDepalitto9 1. Ukifika na kuanza kuchagua menu wanafunika karatasi za bei hivyo huoni... ile unamaliza kula ukija kudai bill ndo unakuta wamefunua karatasi zao za bei sasa 😃.
2. Pale ukiwa mgeni utapigwa sana, ukishazoea ndo unaelewa kuwa eneo lilelile chapati ileile inauzwa 3k kwa 0.5k
Nimepata morali zaidi. ✊🏾
Mwenezi wa wahuni wa mbogamboga anapiga marufuku Watanzania wasituchangie, sisi tunaongeza kasi. Usiku huu nimebarikiwa chochote kitu na kuchangia Tsh 100,000 kuunga mkono harakati za ukombozi wa kweli.
Ikiwa 'Tone Tone' inawanyima usingizi kiwango hicho, basi tujue tuko kwenye mstari sahihi. Ungana nami kuwezesha mabadiliko leo. Kama unaguswa na mustakabali wa nchi yetu, usisite kutoa ulichonacho.
Uhuru wa Kifedha: Chama cha siasa kinachofadhiliwa moja kwa moja na wananchi wenyewe kinawajibika moja kwa moja kwa wananchi, si kwa wafadhili wakubwa au mifumo ya siri. CHADEMA ni mali ya Watanzania.
Ujumbe wa Kisiasa: Kuchangia harakati za kisiasa ni kura halali ya maoni kabla ya sanduku la kura. Michango ya fedha na mali ya hiari inatuma ishara kwamba kuna watu wako tayari kugharamia kile wanachokiamini.
Nguvu ya Umma: Dhana ya ‘Tone Tone’ inajenga bahari kubwa. Shilingi 1,000 kutoka kwa watu milioni moja ni nguvu kubwa kuliko bilioni moja kutoka kwa mtu mmoja. Tusiogope. Tuchangie wengi. Wameogopa.
Kila tone linahesabika. Namba ya Kuchangia: 0744446969 (CHADEMA HQ).
MARIDHIANO BILA UKWELI NA UWAJIBIKAJI NI USALITI.
Historia haina huruma kwa watawala katili. Historia inatunza kumbukumbu za sauti zilizopazwa wakati wa mchana kweupe, lakini zikamezwa na giza totoro. Leo watawala wanazungumzia Maridhiano, neno tamu vinywani, lakini lenye makovu makubwa moyoni.
Kumbukumbu hazidanganyi. Humphrey Polepole alisimama, akanyoosha kidole akasema: “Tupatane kwanza kabla ya uchaguzi” Matokeo yake? Akapotezwa. Je, alipotea kwa hiari au alipotezwa kwa lazima? Sauti yake ikawa kama mwangwi uliopotea bondeni.
Mzee Warioba, mbeba maono ya katiba, akapaza sauti: “Tusikimbilie sanduku la kura bila maridhiano.” Badala ya kumsikiliza, mawe yakawa majibu yake. Mzee wa heshima akazuiwa, akawa mfungwa wa mawazo yake mwenyewe ndani ya kuta za nyumbani kwake.
Askofu Josephat Gwajima, akajitokeza, akashauri chama chake na watawala, nchi inahitaji uponyaji, majadiliano kabla ya kwenda katika uchaguzi. Akashauri, uchaguzi huru na haki ni tunda la amani. Hakusikilizwa. Akapuuzwa. Akatukanwa. Akashambuliwa sana.
Vipi kuhusu Captain Tesha? Alisema mengi, akataka maridhiano ya dhati. Akasema mifumo imeharibika na inahitaji marekebisho. Leo, sauti yake imekuwa kama redio iliyozimwa ghafla katikati ya msiba mzito. Tesha na wengine, walioona mvua kabla ya mawingu..
CHADEMA hatuwezi kusahau hata kidogo. Chini ya jua kali na mvua za el nino, kwenye ngurumo nzito na radi, tulipita katika matope tukidai kitu kimoja: Mageuzi ya kimsinhi kabla ya Uchaguzi. Lakini majibu yalikuwa ni kutekwa, magereza, na kuzuiliwa kufanya siasa.
Shingo za watawala zilijawa na kiburi, mioyo ikawa migumu, mkiamini kuwa ushindi ni kuiba kura na si kuchaguliwa na wananchi. Hamkutaka kuchaguliwa. Mliamua kujitangaza washindi kwa ushindi wa kishindo. Watu milioni 32 walishiriki uchaguzi wapi?
Vongozi wa kiroho hawakukaa kimya. TEC, Bagonza, na Gwajima, wote walionya. Walisema maridhiano si chaguo, ni hitaji la lazima ili taifa lipumue. Lakini, shingo zilikuwa ngumu. Mkajiona miungu watu msiohitaji ushauri wa ardhi wala mbingu. Mkasonga mbele.
Fr. Dkt. Charles Kitima, mwanatheolojia, alipojaribu kutoa ushauri wake wa busara kuelekea uchaguzi mkuu akiwa salama ndani ya makazi ya Maaskofu, alivamiwa na maharamia. Alishambuliwa. Akaonewa sana. Akayaona mauti moja kwa moja usoni kwake. Mbaya sana.
Mliamua kushughulika hata na viongozi wa dini. Hakika, mlivuka mipaka. Mdude Nyagali alivamiwa, akatekwa na kupotezwa kabisa. Deusdedith Soka alitekwa na kupotezwa. Dioniz Kipanya alitekwa na kupotezwa. Mamia ya vijana wa CHADEMA, wafuasi wazalendo, watoto wa Tanzania. Walitekwa, wakapotezwa.
Baada ya kuitimiza azma yenu ya kishari; baada ya kuwapoteza wenye sauti na kuwapiga mawe wenye hekima; baada ya kuvuna mlichokusudia kwa nguvu. Mmefikia kile mlichokusudia. Mlichokikinga, mlichokilinda, mlichokitimiza kwa nguvu zote.
Mnataka Maridhiano ya aina gani? Je, ni maridhiano ya kumsafisha aliyetenda makosa bila kutubu? Je, ni maridhiano ya kunyamazisha waliojeruhiwa ili msisikie sauti za maumivu yao? Ni maridhiano ya dhati yanayoanza na KUKIRI MAKOSA na KUWAJIBIKA?
Maridhiano bila haki ni usaliti. HAKI za watu ambao wameuwawa, wamepotezwa, wamefungwa, wamejeruhiwa. Maridhiano bila ya wahusika kukiri makosa ni kiini macho. CHADEMA hatuwezi kutumika katika safari ya wananchi kuelekea kusikojulikana.
Maridhiano ya kweli yanahitaji ujasiri wa kukiri makosa, si ujasiri wa kuficha yaliyopita. Yanahitaji haki, si hila. Yanahitaji sauti zote zisikike, si sauti za wapinzani kuzimwa ili zao pekee zisikike. Wapinzani waseme wapi panavuja. Watawala wakiri makosa yao. Tusonge.
Kama mmetimiza mlichokusudia, angalau kuweni na ujasiri wa kusema: Tulikosea, tuanze upya. Tanzania mpya inawezekana. Lakini huo upya wa Tanzania hauji kwa kufuta kumbukumbu za matukio mabaya yaliyotokea. Unakuja kwa kukabiliana na ukweli.
NB; Hakuna mgao wa kipande cha keki ya maridhiano kwenye sahani yenye damu.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Tundu A.M Lissu, kiunoni ana risasi ambayo madaktari wameshauri, isiondolewe. Mwili wake una makovu ya risasi na makovu ya visu, oparesheni zaidi ya 22. Mguu wake mmoja ni mfupi kutokana na oparesheni hizo.
Tundu A.M Lissu ni mlemavu wa kudumu sasa kutokana na madhila ambayo amepitishwa na wahuni ambao walipanga njamaa za kumuua ili waendelee kusalia madarakani. Walihofia, akiwa hai, atawasumbua.
Tundu A.M Lissu anatakiwa kuonana na madaktari wake kila anapohudhuria kliniki nchini Belgium. Amezuiwa. Hakuna kliniki. Lakini, TAL akifikishwa Mahakamani ana furaha kuliko watu wengine wote walio huru uraini.
Tundu A.M Lissu amekaa gerezani (mahabusu katika gereza la Keko na gereza la Ukonga, Dar es Salaam) kuanzia alipokamatwa akiwa Mbinga, Songea April 9, 2025 hadi leo April 9, 2026, ni takribani siku 365.
Tangu upande wa mashtaka walipokimbilia Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu uliompa ushindi Tundu Lissu ni mwezi sasa umepita, Jaji hajapangwa na tarehe ya shauri haijapangwa…
Viumbe waliomtungia mashtaka ya uongo ya uhaini ili akae gerezani na wakajichagua kwa kishindo na kujitangaza kibabe, wakaingia Serikalini na bungeni, wao wanaanguka na kuondoka kama mshumaa.
Wakati mwingine, Mungu hatumii radi kuwaangamiza watu ambao ni wadhalimu; anatumia tu muda na ustahimilivu wa yule anayeteswa kuwaonyesha kuwa ndiye Mwenye Mamlaka ya mwisho. Takbīr.