#VIDEO Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, amesema wivu wa mapenzi ni miongoni mwa sababu zinazochangia matukio ya mauaji na majeraha yanayotokana na migogoro ya kifamilia mkoani humo.
DCP Mutafungwa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Dawati la Habari la Jeshi la Polisi pamoja na mwandishi wa chombo cha habari cha nchini, ofisini kwake.
Amesema ukatili wa kijinsia hujitokeza kwa namna mbalimbali, zikiwamo kupigwa, kutukanwa na kujeruhiwa, huku baadhi ya matukio yakifikia hatua mbaya zaidi kutokana na migogoro baina ya wanandoa na wapenzi.
Akizungumzia hali ya migogoro ya ndoa, Kamanda Mutafungwa amesema jumla ya migogoro 21 ya ndoa imeripotiwa polisi katika mwezi Oktoba, akibainisha kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuzuia matukio hayo.
Ameeleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kukabiliana na ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto kwa kushirikiana na watoa huduma mbalimbali, huku maafisa na askari wenye mafunzo maalumu wakishiriki katika kushughulikia kesi zinazohusu masuala hayo.
Kamanda Mutafungwa amesisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kutoa taarifa na kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kukabiliana na migogoro ya kifamilia kabla haijageuka kuwa vitendo vya ukatili vinavyoweza kusababisha majeraha au vifo #EastAfricaRadio
#UPDATES Kenya imethibitisha kifo cha pili cha Ebola. Mwanamke mwenye umri wa miaka 65 aliyefariki alikuwa ndugu wa karibu wa mgonjwa wa kwanza, na alianza kuonyesha dalili akiwa karantini jijini Nairobi.
Kenya imethibitisha kifo cha pili kutokana na ugonjwa wa Ebola, huku mamlaka za afya zikisema hakuna ushahidi wa maambukizi kusambaa katika jamii nje ya kundi la watu waliokuwa na uhusiano na mgonjwa wa kwanza.
Wizara ya Afya ilisema Ijumaa, Oktoba 23, kuwa aliyefariki ni mwanamke mwenye umri wa miaka 65, aliyekuwa ndugu wa karibu wa Mkenya aliyefariki kutokana na ugonjwa huo mapema mwezi huu.
Mwanamke huyo alikuwa miongoni mwa watu waliowekwa karantini baada ya kuwa karibu na mgonjwa wa kwanza.
Alianza kuonyesha dalili siku kumi kabla ya kifo chake na kulazwa katika kitengo cha magonjwa ya kuambukiza jijini Nairobi, ambako alipatiwa huduma za kupunguza makali ya ugonjwa na kusaidia mwili kupambana nao.
Wizara ilisema wahudumu wa afya walifanya kila lililowezekana kuokoa maisha yake, lakini alifariki Ijumaa jioni. Familia yake imejulishwa na mipango ya mazishi salama yenye kuheshimu utu wa marehemu itaandaliwa kwa kushirikiana na ndugu zake.
Wagonjwa wengine saba wanaendelea kutibiwa katika vituo viwili vya kutengwa. Kwa jumla, Kenya imethibitisha maambukizi tisa, yakiwemo ya watu wawili waliofariki. Hakuna maambukizi mapya yaliyotangazwa katika taarifa hiyo. #EastAfricaRadio
#HABARI Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amewashutumu viongozi wa nchi za kigeni kwa kutumia maandamano yanayoendelea nchini humo kujinufaisha kisiasa na kuongeza uungwaji mkono katika chaguzi za nchi zao.
Macron amesema baadhi ya viongozi hao wanatumia matamshi kuhusu ghasia zilizotokana na maandamano dhidi ya kupanda kwa gharama za maisha nchini Ufaransa kama nyenzo za kampeni za uchaguzi, bila kuwataja kwa majina.
Matamshi hayo yanatajwa kuelekezwa kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, anayekabiliwa na uchaguzi wa bunge, pamoja na Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye nchi yake inajiandaa na uchaguzi wa katikati ya muhula wa Bunge.
Tangu ghasia zilipozuka Paris na miji mingine ikiwemo Lyon, Marseille na Nice, karibu watu 150 wamehukumiwa, huku zaidi ya 800 wakifikishwa mahakamani kutokana na matukio hayo.
#EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
Baada ya kufanya utafiti mshauri wa malezi Noell Tenga anasema watu wenye nia ovu wana dhumuni la kurudi kuitawala bara la Africa bila ya wanaume kuwepo.
#PilikaPilika
π£ @eddienyota5 na @yustamsowoya wanashauri watu wawe na wapenzi ambao watawapelekesha mputamputa ili kufanikisha malengo waliyoyapanga na yale wanayoyatarajia.
#PilikaPilika
Prime EATV ilikuwa na Salama, Seki, Dullah, Sam Misago, Bhoke, TBway, Patrick Nyembera, Zembwela, George Bantu, Kennedy the remedy, Jamal, Ian Dialo, Anna Peter, Ben Kinyaiya, Maimatha wa Jesse!
Kuna mmoja wapo anarudi unadhani ni nani?
KipengaXtra: @nsajigwa_senior anasema Israel Mwenda ni mchezaji pekee ambaye amethibitisha ubora na uwepo wake kwenye kikosi cha Yanga kila kitu kinaweza kwenda sawa hata bila Yao , kwaiyo Yanga kwa sasa inamuhitaji zaidi Mwenda kuliko Mwenda anavyoihitaji Yanga.
#KipengaXtra #HainaKuchoka #EastAfricaRadio
KipengaXtra: @mandala_simba anasema Yanga walimuandaa Mwenda mapema ili awe mbadala wa Yao endapo atapata majeraha, kwa sasa Yanga hakuna mbadala sahihi wa Yao zaidi ya Mwenda.
#KipengaXtra#HainaKuchoka#EastAfricaRadio
KipengaXtra: @mandala_simba anasema Yanga kuna wachezaji waliosajiliwa ambao ni wazee kwaiyo kwa uchezaji wa Kangwanda wasiseme anacheza kibishoo yule amezeeka .
#KipengaXtra#HainaKuchoka#EastAfricaRadio
#MICHEZO: Klabu ya Simba SC imefanikiwa kupata ridhaa ya kuruhusu mashabiki kuingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kushuhudia mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya 15 de Agosto, utakaopigwa Oktoba 21, 2026.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Simba imesema uamuzi huo umefikiwa baada ya mazungumzo ya kina kati ya viongozi wa klabu hiyo na wenzao wa 15 de Agosto, ambao wamekubali ombi la kuruhusu mashabiki kuhudhuria mchezo huo.
#Michezo #Hainakuchoka #EastAfricaTV
Bonyeza Link ya #PilikaPilika leo ipo kuhusu mtazamo wa mwanaume kufa kwa ajili ya mke wake kama ambavyo rapa na muimbaji wa Nigeria Odumodublvck ameweka wazi.
#PilikaPilika