Asante kaka @HecheJohn akili kubwa 👊🏽🔥
Ni kwamba jana katuambia Nchimbi shida iko wapi!
Soon tutaongea wote lugha moja kila mtu atafikiwa! Tusimame pamoja tupambanie Haki, Uwajibikaji na Ukweli kisha tupate #KatibaMpya#TutaelewanaTu
Wanangu on my view huyu jamaa @Sativa255 nimejuana naye hapa X na kama miaka mitano 5 sasa....il la hatujawahi kukutana face to face, kitu anachokifanya kwenye Jamie wazeee n massive movement ukiangalia dhoruba alizopitia nusu kufa na akarudi stronger na bado anaishi na msimamo wake uleule aseeee jamaa anahitaji heshima ndo hivyo bongo wana tabia ya kumchukulia mtu poa sana 🙌🙌
Wanangu challenge ni kumaliza hii michango kabla ya siku 20 tangu tuanze michango.
Leo ni siku ya 14 na tuna 218.
Kiufupi tupo nje ya MUDA SANAAAA.
Changia sasa MPESA.
0744446969
Jina: CHADEMA HQ
Repost 200.
Kama ulikuwa hujafuatilia posts zangu narudia - huko ndani hali mbaya - vita imeshakuwa kubwa
Sisi huku nje tuendelee na mapambano dhidi ya utawala huu wa kifedhuli - atakayeibuka mshindi tutajua tutadeal naye vipi! Ila huyu kimama na genge lake wamedhihirisha wako tayari kutuua wote maana wao wanataka waibe rasilimali ZOTE za Tanganyika na watambe wao na familia zao - sisi tumegoma!
Ni mashetani wenye roho nyeusi! Kama kuna wenye roho za kibinadamu wamebaki huko ndani wapambane kwelikweli! Sisi hatujaacha kupambana 👊🏽🔥
Tumeshashinda sema mashetani wamekaza fuvu tu!
“BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya."
Kutoka 14:14
UJUMBE WA DADA WA TAIFA MANGE KIMAMBI KWA NCHIMBI.
Kwako Nchimbi , kama haya unayoyasema ni sehemu ya project ya “kukinusuru chama” naomba nikwambie kwamba baada ya October 29 hakuna chochote kitakachoinusuru CCM na hasira za Watanzania.
Watanzania tunakuomba uangalie jinsi ya KUINUSURU TANZANIA, na sio kuinusuru CCM.
CCM imeshafika mwisho….. Na mioyoni mwetu Watanzania tumeshafunga ukurasa wa CCM.
Kumbukumbu zinasema CCM waliahidi Katiba Mpya ndani ya siku 100 baada ya uchaguzi. Siku 268 zimepita sasa, kimya kimetawala, na aliyekuwa mgombea mwenza wao anasema wananchi wapiganie Katiba Mpya. Huu ni mzaha! Wananchi hawawezi kupambania deni ambalo chama kiliingia mkataba wa kulilipa kupitia ilani yake. Hivi Nchimbi anachukuliaje hili? Tukiita ahadi hii kuwa ni utapeli wa kisiasa tutakuwa tumekosea? Ukweli ni kwamba huu ni utapeli kama utapeli mwingine wowote ule. Wametugeuka mchana kweupe!
‼️HABARI MBAYA‼️
Jioni ya leo Katibu wetu wa CHADEMA kanda ya Serengeti @jacksonmnyawam2 amesomewa kesi ya mchongo ya UGAIDI pamoja na wanachama wengine zaidi ya 10 Shinyanga, usiku huu wamepelekwa Gerezani Shinyanga.
Kwako @nchimbie , kama haya unayoyasema ni sehemu ya project ya “kukinusuru chama” naomba nikwambie kwamba baada ya October 29 hakuna chochote kitakachoinusuru CCM na hasira za Watanzania.
Watanzania tunakuomba uangalie jinsi ya KUINUSURU TANZANIA, na sio kuinusuru CCM.
CCM imeshafika mwisho….. Na mioyoni mwetu Watanzania tumeshafunga ukurasa wa CCM.
Nimekuja chuo fulani kidogo kinaishia ngazi ya diploma. Nimeacha gari inatengenezwa kwenye idara ya mechanical engineering, laptop inatengenezwa idara ya IT na mimi nachekiwa meno hapa kwenye ofisi ya dentist. Hizo kazi zote zinafanya na wanafunzi wa hapa kwa bei punguzo. Sisi tunashindwa kufanya hivi vyuoni Kwetu?
Nimechukua muda kutafakari uliyoyasema @nchimbie sasa acha nikujibu:
Leo umeonyesha uungwana kwa maneno maana umesema kuwa uanaharakati si uhasama - na ulinitaja kabisa pamoja na kwamba ninajua kuwa jina langu akilisikia kimama chenu anakasirika - so clearly umeonyesha ujasiri kuliko wana CCM wenzako huko ndani! Sad that we have reached so low!
Pia kuongelea Haki na kukubali hakuna Amani bila Haki na kutaka wanaharakati walindwe na kugusia kesi za kubambika na kutaka watu waachiwe ni jambo jema sana
Mwisho umetumia muda kuongelea Katiba Mpya na kutaka tupambanie
Kwa maneno haya mazuri umefanya jambo jema na wapo wengi ambao wamepata matumaini maana wamechoka na chokochoko zenu CCM na kimama chenu kutwa kuwinda na kuumiza watanganyika!
Sasa baada ya haya nataka ninyooke na mambo kadhaa maana mi si mnafiki
Kwa kifupi maneno mazuri hayatoshi kwa hapa tulipofika maana hata Samia alikuwa ana kauli positive na 4R zake ila I was not impressed!
Kwa sababu mi nathamini matendo!
👉🏽 Kuna sheria zaidi ya 40 ambazo ni kandamizi na ktk sekta tofauti zinatumika kutuadhibu na kutuumiza katika harakati zenu za kutunyamisha hii ni pamoja na sheria za Cybercrime, Takwimu, Ugaidi, uhujumu uchumi, Statistics law, NGO law nk
Bila kufuta hizi sheria mtaendelea kutupa haki zetu kama hisani - FUTENI
👉🏽 MO29 hatuwezi kuweka kando na kuongelea KatibaMpya na Maridhiano bila kwanza kukabili hili DOA kubwa! Watu waliuwawa, damu ilimwagwa kwa hiyo LAZIMA waliohusika wawajibishwe na tuambiwe ukweli - nani alihusika, miili iko wapi nk. Wewe ni mnufaika wa mauaji haya - sasa kama utaonyesha ujasiri kukubali na kuhakikisha Haki na Ukweli unapatikana hakuna mtu atakuwa na mashaka na uwezo wako kama kiongozi!
👉🏽 Katiba Mpya tunautaka ila kwa mazingira ya sasa na bunge hii hapana hatuwezi kupata Katiba Bora - so turudi kule kwenye serikali ya mpito! Rais haramu anataka hataki - we don’t care! Katiba ni Yetu wananchi! Hatusubiri mtupatie! Ila tutafurahi mkikubali kushiriki tukiwa wote sawa na si ninyi kama watawala
👉🏽 Una uwezo hata leo kuhakikisha Lissu anaachiwa na vijana na lecturers waliopewa ugaidi wanafutiwa kesi hata kesho! Wote waliotekwa kabla na baada ta MO29 akina Mdude, Polepole, Soka nk tuambiwe hatma zao na waliohusika kisha wawajibishwe wote! Mi NINAJUA ukiamua unaweza - so do it!
👉🏽 kuhusu wanaharakati - hakuna hata mmoja wetu aliyeamka na kuamua kuwa mwanaharakati! Sote tulikuwa na kazi zetu ila tuliamua kutokaa kimya kwa sababu ya dhulma! So hili si suala la sisi kujuana au kutojuana - tuamue kwa pamoja kuwa tusikubali tena mtu awindwe kwa sababu ya utofauti wa kimawazo - hata akikutukana usitumie wadhifa wako kumkomoa! Kila mtu ahakikishiwe usalama na walio nje wakiamua kurudi wasibugudhiwe! Hii isiwe hisani au ishu ya kujuana!
Mwisho kabisa mi nina trust issues na CCM maana nawajua kama vile nimewazaa!
So kujenga imani tunahitaji VITENDO zaidi kuliko maneno!
Mungu akupe uwezo wa kunielewa na kufanya yote
All the best!
Baada ya Nchimbi kuwakojoza kwa maneno matupu, jioni hii tumepokea taarifa mbaya kuwa Ndg Jackson Mnyawami, Katibu wa CDM Kanda ya Serengeti, amepewa kesi ya Ugaidi.
Sababu ni zilezile. Sababu za kijinga!
This is so heartbreaking and unfair!💔
Tupiganie Katiba Mpya kivipi Wakati Lissu alipigania Katiba Mpya mkamfungulia kesi ya Uhaini?
Tukomae na Katiba Mpya kivipi wakati Vijana walipokomaa na Katiba Mpya mwaka jana mliwapiga risasi za moto na kuwaua?
Tupiganie Katiba Mpya gani ambayo vijana wa CHASO Mbeya, Mwanza, Iringa na mikoa mingine wakifanya hivyo wanafunguliwa kesi za Ugaidi na Uhaini?
Tupiganiaje Katiba Mpya wakati Dr. Melkisedeki Kaijage wa UDOM amewaambia wanafunzi wake Darasani kuwa kuandamana ni Haki ya Kikatiba leo amefunguliwa kesi ya Ugaidi?
Unasemaje kama unataka Amani lazima Utende Haki na usione aibu kutamka haki katika mazingira ya nchi ambayo Vijana wanatekwa, wanapotezwa, wanafunguliwa kesi za uongo za ugaidi na uhaini ? Wanaoruhusu haya yafanyike ni akina nani Bwana Nchimbi atueleze tumuelewe.
BAVICHA tumesema huu ni wakati tunaohitaji VITENDO dhidi ya MANENO. Hatuhitaji kauli tamu za kutufurahisha.
Wanaokula kodi zetu watanzania tunahitaji watuambie:
Katiba Mpya itapatikanaje kabla ya 2029 na 2030 wakati hadi sasa hakuna Bajeti ya Mchakato huo?
Hakuna Calendar ya matukio ya namna mchakato huo utakavyofanyika na kukamilika. Tutaaminije?
Msimamo wa BAVICHA na Chama chetu ni No Reforms: No Election kwa Uchaguzi wa 2029 na ule wa 2030. Ni muhimu wanaotumia kodi za Watanzania wakawekeza kwenye kuhakikisha mazingira ya kupatikana Katiba Mpya ya Wananchi inapatikana kweli na sio mbwembwe na propaganda.
Deogratias Mahinyila @AdvMahinyila
Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa.
24/07/2026.
Hatuwezi kuwasaliti wapiganaji na mashujaa wote waliouwawa wakipigania uadilifu wa bendera yetu kwa kauli tupu za Imanweli Nchimbi.
We ain’t sellouts.
We need truth, justice and accountability!
Madai yetu yako palepale!
Na mauaji ya Oktoba 29 remains at large in our hearts 💔
‼️ALERT ‼️
Muda huu huko Kilwa Madalali wamekusanya Watu wa CCM, wamewavalisha nguo za CHADEMA na kuwarekodi wakimshambulia Mhe. Heche kwa malipo ya laki moja moja.
Muda wowote kuanzia sasa mtaona video yao ambayo inatokana na hii picha niliyowapostia, Vibaraka wa Nduli Idd Amin Mama wanahangaika sana.😂😂😂