KENYA AIRWAYS MARUFUKU ANGA YA TANZANIA:
Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) imeiondoa Kenya Airways (KQ) kwenye orodha ya ndege zinazoruhusiwa kutumia anga ya Tanzania kuanzia Agosti 1 ikiwa ni hatua baada ya Serikali ya Kenya kuzuia raia wa Tanzania kuingia nchini humo
Mshindi wa kura za maoni CCM Ubunge Viti Maalum (Vijana) Mkoa wa Pwani ni Khadija Khalid Ismail mwenye kura 15 kati ya kura 40 zilizopigwa, nafasi ya pili imeenda kwa Mary Daniel mwenye kura 8 akifuatiwa na Mufandi Hamisi mwenye kura 6.
#MillardAyoUPDATES
โIlibidi niende Dar es Salaam kwa kutumia Ndege kutokea Mtwara lakini nimepita hii Barabara (Mtwara- DSM) makusudi nione hali yake, hii Barabara imeharibika, 90 KM zote zimeharibika. magari yenye uzito mkubwa yameharibu hii Barabaraโ-JPM njiani kuelekea DSM
#MillardAyoUPDATES
Rais JPM ameagiza Wakazi wa Kibiti kujisaidia kwenye vyoo wanavyotumia DC na DED wa Kibiti majumbani mwao kufuatia soko la Kibiti kukosa choo. โnatoa wiki moja DC na DED jengeni vyoo hapa, wafanyabiashara kuanzia leo msilipe ushuru hadi wajenge vyoo na kwa sasa tumieni vyoo vyaoโ
Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia kwa muda mchezaji wa Yanga, Bernard Morrison katika kituo cha Osterbay. RPC wa Kinondoni Rodgers Bukombe amesema Morrison alikamatwa baada ya kupishana maneno na askari waliotilia shaka gari lake.
Tuna Msiba
Tuna Uchaguzi
Tuna Vitu Vingi Vya Msingi Kujadili
Lakini Utakuta Wapwa Tunajadili Kuhusu Mwanaume Anatakiwa Awe Na Boxer Ngapi????
Kwani Aliyetuloga Ni Nani?
Wanakijiji wa Lupaso na vijiji jirani wanaendelea na usafi nyumbani kwao na marehemu Rais wa Awamu ya tatu Benjemin Mkapa kwaajili ya kuweka mazingira vizuri, tayari kwa kupokea wageni mbalimbali wakaofika kwaajili ya shughuli za kuaga za mazishi.
#RIPMkapa
Aggrey Mwanry "Mzee wa Sukuma ndani" amekuwa kivutio katika mkutano wa wagombea wa nafasi ya Ubunge katika kura za maoni kwa majimbo tisa ya mkoa wa Kilimanjaro wanaokutana kwa lengo la kuvunja makundi baada ya kukamilika kura za maoni