Yule dogo uliyemuita kwenye interview, na wakati umeandaa majina yako, amepoteza tumaini tayari
Yule kijana uliyemfelisha mtihan kwasababu anapendwa na binti anayekukataa, karudi kwao kulima
Yule mchizi uliyemchongea kwa boss, kafukuzwa kazi na hana maisha๐
Kizazi cha leo kitu chenye thamani ni hela peke yake, unaweza amfanyia mtu vitu vyenye thamani kubwa kuliko pesa ila kwa kuwa siyo pesa havitakuwa na thamani machoni pake.
YAFANYIE KAZI MAWILI HAYA
Usiwasaidie Watu ili wakusifie na usiwasifie ili wakusaidie
Saidia kwaSababu ni jambo sahihi kufanya,Si kwaSababu unataka kusifiwa
Msifie Mtu kwaSababu anastahili,Si kwaSababu unataka kitu kutoka kwake
Usifanye Wema kua Biashara ya kubadilishana Faida
Kati ya ngoma zote za kuchanana zilizowahi kutoka hapa Bongo, ni Diss Track gani ambayo ilimaliza kabisa ubishi na kumfanya mpinzani aonekane kaenda vitani bila silaha?
Twende kazi sasa...๐๐ค
Soma https://t.co/vRd4LQL7tX
#JamiiForums#JFBurudani
Kuna mtu anafungwa kiasi kwamba hela ya kula kwake ni tabu ,mwingine pesa anapata sana ila anafungwa akipata hafanyi maendeleo,akipata hela haikai,atatumia ovyo au akipata mikosi itamsonga ilimradi zile hela atumie nje ya malengo yake mwisho ashindwe kufikia daraja analostahili
Ukikutana na mtu mwenye akili au ujuzi mkubwa kukuzidi, usimfanye mpinzani wako ili uthibitishe ubora wako. Shirikiana naye. Jifunze kwake mkue pamoja, badala ya kupoteza nguvu kwenye ushindani usio na tija.
Kuna mwanamke atakuja kwenye maisha yako na hatataka ubadilike kwa ajili yake.
Atataka ukue.
Atataka utimize malengo yako.
Atataka uwe karibu na Mungu.
Atataka uwe version bora ya wewe mwenyewe.
Huyo ni tofauti na wengi.
Ukimpata TULIA .
Kama kuna tabia imenisumbua kupambana nayo muda mrefu na ilikwamisha mengi ni kuchelewa kuanza na kuacha mapema ninachoanza. Kuchelewa kuanza, nikitafakari, naona tatizo ni vile nilikuwa naogopa kutokufanya kwa kiwango cha ukamilifu ninaoutaka. Kuliko fedheha ya kufanya chini ya ubora, nachagua kuahirisha kuchukua hatua ya kwanza nikiamini nitakuwa tayari zaidi baadae.
Ukamilifu, kwa mazingira haya, unakuwa tatizo kwa vile unakugeuza mtumwa wa ubora usioweza kuuonesha. Kumbe ukamilifu wa kufikirika (na saa nyingine usiohitajika) unakuwa ndiye โmchawiโ anayenizuia kuanza.
Hili la kuacha ninachoanza, kwa kiasi kikubwa, kilitokana na kukosa subira na mchakato usioleta matokeo kwa wakati. Kila nilipoona dalili za kukosea niliona bora kuacha nisiaibishe ukoo. Kuna namna nilikuwa naamini muda upo wa kuanza kingine kwa gharama ya kutelekeza nilichokwisha kukianza, matokeo yake, muda mwingi ulitekea kuanzisha kisichokamilika.
Ilinichukua muda kuelewa kumbe hata sihitaji ukamilifu kuanza. Ukamilifu ni uongo nilioutumia kujichelewesha wakati kumbe hata niliodhani wanategemea huo ukamilifu hawakuwa na matarajio hayo.
Ingawa kuona matokeo kunaongeza hamasa, nikajifunza kumbe saa nyingine inachukua muda juhudi kulipa. Ukisubiri kuona matokeo haraka hutokaa uone thamani ya mchakato mgumu unaokupeleka kwenye matokeo. Hata hivyo, nilijifunza umuhimu wa kujiwekea vigezo vidogo vidogo vinavyonionesha hatua fupi fupi ninazopiga kuelekea kwenye lengo.
Somo: Unaweza kutafuta namna yako ya kuanza jambo na kuliendeleza.