@MariaSTsehai Yule mganga wa mchongo wa kesi ya Temba mwanafunzi wa IFM hivi wameishia wapi?
Kusahau kama Chaula alitekwa kwa kuchana picha aliyochora mwenye labda nisahau mimi ila wazazi na ndugu zake hawawezi kusahau
Leo #MariaSpaces tunajadili: Aluta Continua #FreeTunduLissu
Tumekubaliana kuwa hakuna kumwachia Mungu suala la Lissu na njia kuu ni maandamano!
Mapambano yanaendelea sasa tujipange hakuna kurudi nyuma!
Njoo uchangie mawazo tunatokaje?
Leo saa 2 uck
“Waheshimiwa Majaji nashukuru kwa fursa ya kuzungumza. Naomba mnisikilize kwa makini kama ambavyo mmenisikiliza kwa makini mwaka mzima. Naomba pia m’rekodi proceedings kama mlivyo’rekodi vizuri mwaka mzima na nusu. Leo Waheshimiwa majaji ni siku ya 577 nikiwa gerezani kwa kosa la uhaini. Ndiyo kosa kubwa Kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano. Ndiyo kosa pekee lililotamkwa katika katiba, kosa la uhaini. Kwa siku 577 nimeitwa mhaini. Kosa ambalo kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) ambapo adhabu yake inaeeza kuwa ni KIFO. Baada ya siku 577 baaada ya wingu jeusi la adhabu ya kifo kuning’inia juu ya kichwa changu. Leo Waheshimiwa Majaji mmeniita MCHOCHEZI. Kosa ambalo wala halijapangiwa adhabu. Unaona hapa, wakili mkuu wa serikali anahangaika kutafuta hii adhabu yake ni nini., anasema nipewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine, nihukumiwe kifungo cha miaka mitano gerezani. Hii maana yake ni nini Waheshimiwa Majaji? Waheshimiwa majaji mmesema wenyewe hakukuwa kosa. Kwa hiyo nimekaa gerezani siku 577 bila kosa lolote. Kuna kitu kimoja hamjakisema nitakisema kwa ajili ya kumbukumbu za Mahakama. Ushahidi wangu umethibitisha kwamba hii ilikuwa kesi ya kisiasa. Kugeuza Mahakama kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa, it’s an obvious political persecution. Kwa sababu ni political persecution inabidi vi’sababu vitangenezwe vya kumfunga huyu mgomvi wetu. Vi’sababu vya kumfunga huyu mpinzani wetu. Hili kosa la UCHOCHEZI ni kisa ambalo ninyi Waheshimiwa Majaji mmelitengeneza. Mimi nilishitakiwa kwa UHAINI na kusambaza taarifa za uongo. Mmetafuta kosa ambalo halikuwepo, mmenipa. With all due respect mmefanya hivyo kwa sababu za kisiasa na kwa maelekezo ya kisiasa tu. Ni kama mmeambiwa, huyu mtu hana kosa lakini tafuteni kosa lingine dogo, isije ikaonekana serikali imepata aibu. Mimi ninajua mtani’hukumu. Na mnaonekana tayari mnayo hukumu, l feel it in my heart.”
Tundu Antiphas Mughwai Lissu, O6 November 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania katika hukumu ya kesi yake ya uhaini.
No one should face the death penalty.
Tanzanian opposition party chair Tundu Lissu is charged with treason for peacefully calling for electoral reform.
Release him immediately and unconditionally and drop all charges against him.
#JusticeForLissu#HakiKwaLissu
As an American constitutional lawyer, I have personally litigated cases defending the rights to free expression and due process. These are fundamental principles of human liberty. For that reason, I am closely following the outcome of Tundu Lissu’s trial proceedings, and the broader implications for the rule of law.