KAMBI MAALUM YA HUDUMA ZA MATIBABU YA KIBINGWA KUIFIKIA KANDA SITA NCHINI.
Na WAF - Dodoma
Wizara ya Afya imeanza utekelezaji wa huduma za kibingwa za Mkoba katika kambi sita kwenye mikoa sita Nchini hii ikiwa ni azma ya Serikali ya awamu ya sita kufikisha huduma za afya karibu na wananchi.
Kwa mujibu taarifa iliyotolewa kwa umma Aprili 29, 2024, na Wizara ya Afya na kusainiwa na Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Bw. Englibert Kayombo imesema mikoa hiyo ni Geita, Morogoro, Lindi, Songea, Tanga na Kigoma. Ambapo Madaktari bingwa kutoka katika hospitali za rufaa za Mikoa, Kanda, Taifa na Maalum watashiriki kutoa huduma 12 za kibingwa na Ubingwa Bobezi.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa Malengo makuu ya huduma hizo za Mkoba ni pamoja na Kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi.
"Shabaha ni kuwajengea uwezo wataalamu wa fani mbali mbali waliopo ngazi zote za kutolea huduma na kuibua wagonjwa wanaohitaji huduma za ubingwa bobezi katika hospitali za Kanda, Maalum na Taifa" imeeleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo huduma za kibingwa zitakazotolewa na Madaktari hao ni pamoja na Ubingwa wa akina mama na uzazi, watoto, Upasuaji, Magonjwa ya ndani, Upasuaji Mifupa, Dharura na ajali, Radiolojia, Utoaji wa dawa za ganzi na usingizi, Afya ya akili, huduma za Utengemao, huduma za Macho na huduma za kinywa na Meno.
"Kambi hizi zinafanyika kuanzia tarehe 29 April mpaka tarehe 11 Mei, 2024 kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 10 jioni. Kampeni hii itafanyika kwa awamu mbili, na kila awamu itadumu kwa muda wa juma moja.
Awamu ya kwanza itafanyika katika Mikoa ya Geita, Ruvuma na Tanga kuanzia tarehe 29 Aprili hadi tarehe 4 Mei, 2024 na awamu ya pili itafanyika katika Mikoa ya Lindi, Morogoro na Kigoma kuanzia tarehe 06-11 Mei, 2024" amesema Kayombo.
Sambamba na kambi hizo za Madaktari Bingwa wa Rais, Dkt Samia katika Hospitali za Mikoa, Wizara pia inaendelea kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kuendeleza Kampeni ya kuimarisha ubora wa huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto kwenye ngazi za Halmashauri na baadhi ya vituo vya afya nchini kupitia kampeni ya Madaktari bingwa wa Mama.
Aidha, Wizara inaendelea pia kuimarisha ubora wa huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto yenye kauli mbiu ya “Jiongeze tuwavushe Salama” iliyozinduliwa mwaka 2023 kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI, Mikoa na Halmashauri. Kampeni hii inafanyika katika hospitali zote za halmashauri, ambapo madaktari bingwa wa huduma za Uzazi, Mama na Mtoto wapo katika Hospitali za Halmashauri kwa lengo la kuwajengea uwezo wataalam na kutoa huduma za uzazi, mama na watoto.
Pia, Wizara inatoa wito kwa viongozi wote wa ngazi ya Mikoa na Halmashauri za Wilaya, Waheshimiwa Wabunge na Madiwani kuwapokea madaktari bingwa na kuhamasisha jamii, kufika hospitali kupata huduma stahiki kwani wananchi watapata huduma hizi karibu na maeneo yao ambapo itawapunguzia gharama ya kusafiri kwa ajili ya kufuata huduma za kibingwa.
MWISHO
Uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuongeza vituo vya Afya vinavyofanya upasuaji wa dharura 523 imesaidia wanawake 226,187 sawa na asilimia 12 kufanyiwa upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni Mwaka 2023.
Waziri @ummymwalimu amesema hayo Januari 10, 2024 wakati akitoa taarifa ya hali ya utoaji huduma za Afya nchini kwa mwaka 2023 wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es salaam.
WANANCHI CHUKUENI TAHADHARI DHIDI YA RED EYES
Wizara ya afya imewaasa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa macho mekundu (Red eyes) Maambukizi ya Kirusi kwenye ngozi ya juu ya gololi ya jicho yajulikanayo kitaalamu “Viral Keratoconjunctivitis” iliyoibuka nchini hivi karibuni.
Hayo yamesemwa leo Januari 15, 2023 na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya Prof Pascal Ruggajo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali Prof Tumaini Nagu wakati akitoa taarifa ya uchunguzi wa awali ya ugonjwa huo ambao umeripotiwa kuathiri watu wengi nchini.
Prof. Ruggajo amesema dalili ya ugonjwa huo ni pamoja na macho kuwasha, kuchomachoma, kuuma, macho kutoa machozi na kutoa tongo tongo za njano.
"Taarifa za uchunguzi zinaonesha Maambukizi ya Kirusi hiki kwenye ngozi ya juu ya gololi ya jicho yajulikanayo kitaalamu “Viral Keratoconjunctivitis” ni maambukizi yanayosambaa kwa kasi kubwa. Hakuna tiba maalumu kwa ugonjwa huu na hata bila tiba dalili huisha zenyewe ndani ya wiki mbili". Amesema Prof Ruggajo.
Prof. Ruggajo amesema mwenendo wa ugonjwa huo unaonyesha kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wanaofika katika Vituo vya kutolea huduma za afya wakiwa wanasumbuliwa na ugonjwa huo.
“Katika kipindi cha Desembe 22, 2023 hadi Januari 11, 2024 kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaosumbuliwa na ugonjwa huu kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya matibabu, kwa mfano katika mkoa wa Dar Es Salaam kuna wagonjwa wapya 869 huku hali ya kawaida katika kipindi cha mwezi Desemba 2023 kulikuwa na wagonjwa 17 pekee” amefafanua Prof. Ruggajo.
Aidha amesisitiza suala la usafi ni jambo muhimu katika kuzuia maambukizi kusambaa kwa wengine Kutokana na tabia ya ugonjwa huu kusambaa kwa kasi, maambukizi haya huleta mlipuko ambao husambaa kupitia kirusi kwa asilimia zaidi ya 80%.
Prof Ruggajo amewashauri wananchi kutokutumia dawa zisizo rasmi na ambazo hazijaandikwa na daktari kwa wakati huo na kutotumia dawa za macho anazotumia mgonjwa mwingine ili kuepuka madhara kwa kuwa dawa za macho ni tofauti na kwa matumizi tofauti.
Wizara ya afya imewaasa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa macho mekundu (Red eyes) Maambukizi ya Kirusi kwenye ngozi ya juu ya gololi ya jicho yajulikanayo kitaalamu “Viral Keratoconjunctivitis” iliyoibuka nchini hivi karibuni.
Hayo yamesemwa leo Januari 15, 2024 na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya Prof Pascal Ruggajo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali Prof Tumaini Nagu wakati akitoa taarifa ya uchunguzi wa awali ya ugonjwa huo ambao umeripotiwa kuathiri watu wengi nchini.
Waziri wa Afya Mhe. @ummymwalimu akielezea mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya Afya mwaka 2023 amesema kufikia Disemba 2023 vitanda vya wagonjwa mahututi (ICU) vimeongezeka nchini kufikia vitanda 1,000 kutoka vitanda 528 mwaka 2022
#nambazinaongea#mamayupokazini
HOSPITALI ZA RUFAA NCHINI ZATAKIWA KUWA NA MFUMO RASMI WANANCHI KUTOA MAONI YAO
Na. Majid Abdulkarim , Tumbi- Pwani
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amesisitiza Hospitali zote za Rufaa nchini kuhakikisha zinakuwa na mfumo rasmi ambao unajulikana kwa wanachi wanaowahudumia ili kutoa mrejesho wa Huduma wanazotoa
Dkt. Jingu amebainisha hayo wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani -Tumbi, kwa lengo la kujionea hali ya utoaji wa huduma Huduma za afya katika hospitali hiyo.
Dkt. Jingu amesema njia pekee ya kuhakikisha wanaboresha Huduma kwa wananchi wanaowahudumia ni kupata mrejesho kutoka kwa wananchi wanao wahudumia.
“Tukiimarisha njia za kupata mrejesho kutoka kwa wananchi tunaowahudumia itasaidia kujua ubora wa Huduma tunaotoa upo kiasi gani kwani jukumu la hospitali za Rufaa ni kutoa Huduma kwa viwango vya juu”, ameieleza Dkt. Jingu
Dkt. Jingo ametolea mfano kuwa baadhi ya Hospiatli zimeaanza kutekeleza Mfumo huo kwa kuwa na watu maalumu wakiwa wamevaa nguo zenye maneno niulize mimi au kuwa na vituo vya huduma kwa wateja vilivyopo kusikiliza maoni, kero na pongezi za wananchi wanaowahudumia.
Amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshafanya uwekezaji wa kutosha katika sekta ya afya hivyo ni jukumu la wataalamu wa afya kuhakikisha wanatoa Huduma bora kwa wananchi ili kunufaika na uwekezaji huo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumain Nagu ametoa wito kwa wataalamu wa afya kufanya kazi kwa kuzingatia Miiko na maadili ya kazi zao ili kuleta ufanisi katika kuwahudumia Watanzania.
“Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuwahudumia wananchi na niwakumbushe kuwa tumekuwa na magonjwa mbalimbali ya mlipuko hivyo hakikisheni mnafanya utambuzi wa haraka kwa makini kila mgonjwa anapofika hospitali kupatiwa Huduma za a”, amesema Prof. Nagu
"Asilimia 74 ya watanzania wanapata huduma za afya katika ngazi ya msingi yaani Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali za Wilaya/Halmashauri. Hivyo, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kuongeza nguvu ya kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa utoaji wa huduma za afya ngazi ya msingi” Waziri @ummymwalimu
"Serikali imeendelea kuboresha huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi ili kuhakikisha huduma hizi zinapatikana ndani ya nchi. Huduma hizi zimetolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road and Hospitali za Rufaa za Kanda, Mikoa ikiwemo Hospitali binafsi" Waziri @ummymwalimu
"Mwaka 2022 kulikuwa na mahudhurio ya wagonjwa wa nje (OPD) 41,347,690, Mwaka 2023 kulikuwa na mahudhurio ya wagonjwa wa nje 42,252,741. Wagonjwa waliolazwa (IPD) Mwaka 2022 walikuwa ni 1,630,722 huku Mwaka 2023 walikuwa wagonjwa 1,622,979. Wagonjwa / wateja hawa walipata huduma katika ngazi zifuatazo: Zahanati - 33%, Kituo cha Afya - 18%, Hospitali za Halmashauri - 23%, Hospitali za Rufaa za Mikoa – 9% pamoja na Hospitali za Rufaa za Kanda, Maalum na Taifa – 17%" Waziri @ummymwalimu
Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel akimjulia hali mwananchi aliyefika katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke kupata huduma za Afya, leo Novemba 20,2023 wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Hospitali hiyo.
VIONGOZI WA SEKTA YA AFYA SIMAMIENI UBORA WA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
Na. WAF, Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Molel, amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia ubora wa huduma katika Hospitali na Vituo vya kutolea Huduma za afya na kuhakikisha wanawajengea uwezo watumishi ili kuepuka changamoto na uzembe unaofanywa na baadhi ya wataalamu wa afya nchini.
Dkt. Mollel ametoa agizo hilo leo Jijini Dar Es Salaam wakati akizungumza na watumishii wa afya katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke.
Dk. Mollel amesema yanapotokea matatizo katika vituo vya afya alafu Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawana taarifa au hawajachukua hatua hadi viongozi wa taifa wanafika watu hao wanatakiwa wajitafakari.
Amesema yanapotokea matatizo katika sekta ya afya pamoja na daktari aliyefanya uzembe watu wengine watakao kuwa watuhumiwa ni waganga wakuu wa wilaya na mikoa kwa kutoona na kutatua changamoto kabla hazijatokea.
“Tukija kwenye mkoa wako tukakuta uzembe umetokea mama mjamzito amefariki na Mganga Mkuu wa Wilaya na Mkoa ni mtuhumiwa mpaka vyombo vitakapo chunguza, tukikuta mama, mtoto au mtu yoyote amepata shida alafu mganga mkuu wa mkoa, wilaya na wewe unashangaa inabidi ujitafakari".
Ameeleza Dkt. Mollel.
Aidha, amewataka watoa huduma na watalaamu wa afya kutunza vizuri vifaa tiba vinavyotolewa na Serikali kwani Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya nchini.
Hata hivyo amesema kuwa Rais Dk. Samia ameshafanya kazi yake ya kuwekeza katika sekta ya afya kwa kununua vitendea kazi vingi, ikiwemo kuwekwa mashine za CT Scan ili mtanzania apate huduma bora.
HALI YA MATUMIZI YA VYOO BORA KATIKA MIKOA YOTE TANZANIA BARA
Mikoa inayoongoza kwa kuwa na vyoo bora ni Dar es Salaam (98.5), Ruvuma (92.1) na Njombe (87.6) na mikoa yenye idadi ndogo ya vyoo bora ni Tabora (40.5%), Katavi (52.5%) na Manyara (53.9%). Mikoa anbayo haina vyoo bora ni Katavi (24.3%), Simiyu (24.3%) na Manyara (22.3%).
Kwa mujibu wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ya 2030 “Sustainable Development Goals - SDG 2030”, lengo la 6.2, Nchi zote Wanachama wa Umoja wa Mataifa zinatakiwa kuhakikisha watu wote wanatumia vyoo bora na salama yaani “Safely Managed Sanitation” ifikapo mwaka 2030. Taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya mwaka 2022 inaonesha kuwa asilimia 57 pekee sawa na watu Bilioni 4.6 Duniani wanatumia vyoo bora na salama.
Ripoti ya Tafiti ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria ya Mwaka 2022 (Demographic and Health Survey and Malaria Indicator Survey) imeonesha kuna ongezeko kubwa la watu wanao tumia vyoo bora kutoka asilimia 21 mwaka 2016 hadi asilimia 74.8 mwaka 2022. Takwimu hizi ni hatua chanya katika kufikia lengo la 6.2 la SDG ifikapo mwaka 2030.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiwa bungeni leo Novemba 4, 2023 katika Kikao kinachojadili Taarifa za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu hesabu zilizokaguliwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali CAG kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 na taarifa za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC)
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati akijibu hoja zilizoibuliwa na Kamati za PAC, PIC na LAAC Bungeni kuhusu ukiukwaji wa sheria ya ununuzi wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh. Bilioni 3.4 uliofanywa na MSD kutoka Kampuni ya Misri ya Al Andasia amesema Serikali ilianza kuchukua hatua za kiutawala ambapo ilimuondoa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa mwezi Aprili 2022 pamoja na Wakurugenzi wengine sita akiwemo wa Utawala, Fedha na mipango, Ununuzi, Usambazaji wa huduma za kanda, Meneja wa Sheria na Mkaguzi Mkuu wa ndani wa MSD. Aidha ulifanyika ukaguzi maalum wa eneo la ununuzi na kubadilisha watumishi 24 kabla ya CAG kati ya Juni - Desemba 2022.
Kuhusu deni la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) linaloidai Serikali Waziri @ummymwalimu amesema Serikali imekubali kulipa Shilingi Bilioni 228 za NHIF ambazo ni deni la Wizara ya Mambo ya Ndani Tsh. Bilioni 45.4, Taasisi ya Mifupa (MOI) Tsh. Bilioni 18.2, NIDA Tsh. Bilioni 17.3 na Hospitali ya Benjamin Mkapa Tsh. Bilioni 129. Madeni haya yatalipwa ili kulinda uhai na uendelevu wa Mfuko. Mhe. Ummy ameyasema haya Bungeni wakati akijibu hoja za ripoti ya CAG ya mwaka 2021/2022.
"Kila senti inayotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenda kwenye Sekta ya Afya tutaisimamia, na nitume salamu kwa Watendaji wote wa MSD na wengine wa Sekta ya Afya watakao fanya ubadhirifu hatutawavumilia, tutachukua hatua mara moja ili kulinda fedha za Serikali". Waziri @ummymwalimu