Binafsi Ninaamini kwamba changamoto kubwa kwa vijana si ukosefu wa mtaji, bali ni ukosefu wa ujuzi wa Biashara na nidhamu ya pesa, wengi wetu tunaweza kupewa mtaji ila tukashindwa Kugenerate Income
Kuwa na utulivu wa moyo. Ukipoteza utulivu wa moyo kwasababu ya hasira, umemkosea Mungu, umewaudhi wengine, umejihangaisha mwenyewe, na mwishowe itakupasa kuutafuta tena utulivu wa moyo. Linda sana moyo wako, maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.✍️
Ee Baba yetu Mungu Mkuu,
Umenilinda usiku huu.
Nakushukuru kwa moyo,
Ee Baba Mwana na Roho.
Nilinde tena siku hii,
Niache dhambi nikutii.
Naomba sana Baba wee,
Baraka zako nipokee.
Bikira safi, Ee Maria
Nisipotee nisimamie.
Mlinzi Mkuu Malaika wee,
Kwa Mungu wetu niombee,
Nitake nitende mema tu,
Na mwisho nije kwako juu. Amina.
Njia nyepesi sana ya kudumisha urafiki na undugu ni kulipa madeni, ukikopeshwa lipa. Na Inapendeza zaidi ukilipa bila kukumbushwa lasivyo utaona kila mtu ni fake kwako.
Salamu Maria umejaa neema. Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote. Naye Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu. Utuombee sisi wakosefu. Sasa, na saa ya kufa kwetu, Amina🙏
ISHARA YA MSALABA
1. Ishara ya Msalaba ni nini?
Ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka "Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu."
2. Kwa kugusa paji la uso tuna maana gani?
Kwa kugusa paji la uso tu amaanisha kukubali kwa AKILI
3. Kwa kugusa kufua tuna maana gani?
Kwa kugusa kifua tuna maanisha KUUPOKEA NA KUUPENDA MSALABA MOYONI
4. Kwa kugusa mabega tuna maana gani?
Kwa kugusa mabega tuna maana tupo tayari KUBEBA MSALABA KWA NGUVU ZETU ZOTE.
5. Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomoni na kifua kabla ya Injili ina maana gani
Ni kama ahadi kwamba
1. Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu
2. Nitalitangaza kishujaa kwa midomo yangu
3. Nitalipenda na kulishika kwa moyo wangu wote.
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina.
Ee Baba yetu Mungu Mkuu,
Umenilinda usiku huu.
Nakushukuru kwa moyo,
Ee Baba Mwana na Roho.
Nilinde tena siku hii,
Niache dhambi nikutii.
Naomba sana Baba wee,
Baraka zako nipokee.
Bikira safi, Ee Maria
Nisipotee nisimamie.
Mlinzi Mkuu Malaika wee,
Kwa Mungu wetu niombee,
Nitake nitende mema tu,
Na mwisho nije kwako juu. Amina.