@Bigsyke20@NewwerThiso Kila mtu atapata thawabu yake kwa kadiri ya Mahusiano yake na Muumba
Ondoa hofu, safari ya kuiendea Mbingu ni mwendo wa kinafsi na sio mwendo wa kijiji
Mwishoni ni Mungu tu ndiye ajuaye waliowake. Ishi kwa nafasi yako ukimpendeza Muumba wako na jirani zako, ili uvikwe taji lako
@Bigsyke20@NewwerThiso Mazoea ndiyo yaliyotujengea maadili na ustaarabu mwema ambao tunayaishi hivi leo.
Kuepuka mazoea ambayo hayakuwa na athari hasi kwa mtu na jamii ndio chanzo cha maovu.
Fikiria mtu anaamini kwenye jambo ambalo hashurutishi mtu mwingine aamini kama yeye. Je kuna ubaya?
@Bigsyke20@NewwerThiso Uhuru wa kutoa maoni, haukuwa na lengo la kuonesha udhaifu wako;
Umezaliwa umekuta watu wakiishi kwenye imani hiyo, wewe ni wajuzi tu umeanza kuwa mwalimu juu ya imani iliyoanzishwa karne ya kwanza. Na punde tu, utaondoka na utaacha imani hiyo itaendelea hivyo hata kwa vizazi.
@AbdallahAl91947@bantubikoI60519@EsirEid Dogo mmoja mlevi, aliwahi kumwambia Baba yake mzazi tena kwa hasira na mshangao... "Huwezi kunifundisha hata, maana ningezaliwa mapema ningeweza kukuzaa hata wewe!"
Heshima juu ya imani yako, hupimwa kwa namna unavyoweza kuheshimu imani za watu wengine.
@EsirEid Hata siku moja kifo hakijawahi kuwa sehemu ya adhabu. Kwani kifo ni sehemu muhimu ya ukamilifi wa maisha ya mtu hapa duniani.
Kama kifo kingekuwa ni adhabu basi tuseme manabii na mitume nao walitumikia adhabu hiyo.
@kadugaGK@AhmedSmsha84547@Celsius015 Binafsi sijakuzwa kwenye uzushi. Kwa maana, Mama yangu Mzazi ni Muislam na Baba yangu mzazi ni Mkatoliki, na mimi ni Mkatoliki.
Nimebahatika kufahamu malengo ya siku kuu zote zinazosherehekewa na waislamu pamoja na wakristo. Wazazi wangu pamoja na ndugu zangu hawakuwa wazushi.
@kadugaGK@AhmedSmsha84547@Celsius015 Je unaamini tangu karne ya 3 wakristo wamekuwa wakiadhimisha siku ya Valentine kwa kukumbuka ufuska na umalaya na zinaa? Na kwamba wazazi wetu (sisi wakristo) waliruhusu kabisa na sisi kusherehekea hivyo?
@kadugaGK@AhmedSmsha84547@Celsius015 Kwenye malezi kukanya inaruhusiwa lakini sio uzushi. Huwezi kukanya watoto kwa mambo ya kuzusha,eti kwa sababu unaowakanya ni watoto hawana wajualo.
Malezi yanaenda na ukweli, kukanya watoto kwa mambo ya kuzusha (uongo) unawaanda waongo wa baadaye na wasiopenda kuutafuta ukweli.
@kadugaGK@AhmedSmsha84547@Celsius015 Ni sahihi, lakini kwa muungwana anafahamu habari za Ngoswe muachie Ngoswe mwenyewe.
Kujifanya Ngoswe na kusema habari za ngoswe ni uhuni, kukosa heshima na kuwahudhi watu tu.
@fumbokhanJr@EsirEid Katika karne tuliyopo sasa binadamu amechafukwa na nafikiri kuliko nyakati za Sodoma.
Dhambi ya uzinzi inaweza ikafanywa wakati wowote hata kwenye nyakati za mfungo na hata kwenye siku kuu za kiislamu.
Anayetenda dhambi achagui majira wala siku kuu๐
@EsirEid Ni kama vile Siku za Kiislamu ambazo asili zake ni katika dini ya kiislamu. Na kamwe huwezi kukuta inatolewa ufafanuzi kwa wakatoliki, kwa sababu kwa mafundisho ya wakatoliki tangu kwenye katekisimu hayapo.
@EsirEid Historia ya siku kuu ya Valentine inaanzia ndani ya Kanisa Katoliki. Ni siku kuu ya kukumbuka matendo ya Mt. Valentino aliyekuwa Padre, kwa kuwafungisha wapendanao (wanajeshi na wasiokuwa wanajeshi) ndoa. Ikumbukwe sheria ya Roma ya wakati huo ilizuia askari jeshi asiwe na ndoa.