Serikali kupitia Wakala wa Vipimo (WMA) nchini imekagua na kuhakiki vipimo 1,013,859 ambavyo ni sawa na asilimia 99.2 ya lengo la kukagua vipimo 1,022,342 katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Rais wa FIFA Gianni Infantino amesema shirikisho la mpira wa miguu duniani halina uwezo wa kuamua ni nani anaweza kuingia katika nchi inayoandaa kombe la dunia.
#WorldCup#FIFA
“Lengo la kuonana naye ni kutoa salamu za mshikamano toka kwa chama changu cha @actwazalendo baada ya CHADEMA kufunguliwa kufanya siasa.”
“Niliambatana na Katibu wa Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi, Ndg Maharagande.”
Kiongozi Mkuu wa ACT Wazelendo Bi. Dorothy Semu leo tarehe 25 Aprili 2026 amezungumzo na @hechejohn Makamu Mwenyekiti Bara wa @CHADEMA ofisini kwa makao makuu.
Papa Leo XIV amesema hana “hofu yoyote” dhidi ya utawala wa Rais Donald Trump na ataendelea kutoa msimamo wake wa kupinga vita, kufuatia mashambulizi makali ya maneno kutoka kwa Rais huyo wa Marekani kuhusu msimamo wake juu ya mzozo wa Iran.
RC James amesema mazishi hayo ya kitaifa yataongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt Mwigulu Nchemba.
RC James amesema msiba huo ni pigo kubwa kwa taifa na Mkoa wa Iringa, akisisitiza kuwa marehemu atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, leo Machi 27, 2026amesema mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi yatafanyika Mkoani Iringa siku ya Jumatatu, Machi 31, 2026 katika kijiji cha Idodi.
Makamu Mwenyekiti Bara, Mhe. @HecheJohn, leo tarehe 27 Machi amefika Iringa kutembelea familia ya Marehemu Frank Nyalusi aliyekuwa Mwenyekiti wa jimbo la Iringa Mjini na kuweka shada la maua kwenye kaburi lake, katika Mtaa wa Mtatifikolo, Kata ya Mwangata.
#PoliticsToday
#PICHA Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Marehemu William V. Lukuvi ukitolewa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa kuelekea nyumbani kwake Area D jijini Dodoma.
Mchezo kati ya TRA United vs Simba SC ambao ulipangwa kufanyika leo saa 10:00 jioni umehairishwa kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha jijini Arusha
Kaimu Mkuu Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, David Kimaro amewataka wananchi kuacha tabia ya kuzika maeneo ya makazi kwani ni kinyume cha sheria na kuhatarisha afya ya jamii.
Imethibitishwa kuwa kiungo wa Singida Black Stars Khalid Aucho ameomba radhi kwenye klabu yake baada ya kupewa adhabu ya kinidhamu na kukaa nje kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union na kuukosa mchezo dhidi ya Yanga SC.
Israel kwa kushirikiana na Marekani imeshambulia Mji Mkuu wa Iran, Tehran katika Operesheni ya Kijeshi ambayo Waziri wa Ulinzi wa Israel amedokeza kuwa ni “shambulio la kujihami”
Unaambiwa Kocha wa PSG Luis Enrique ameitaja Chelsea kama timu anayotamani kukutana nayo katika hatua ya 16 bora ya Uefa Champions League msimu huu.
Ikumbukwe kuwa Kocha Enrique alifungwa na Chelsea mabao 3-0 katika mechi ya Fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu 2025.
Wilson Nangu beki wa kati wa klabu ya Simba amefanyiwa upasuji wa kifundo cha mguu nchini Afrika Kusini katika jeraha alilopata kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Espérance Sportive de Tunis.
Infantino ameipongeza Tanzania kwa kazi kubwa inayofanywa ya kujenga miundombinu ya michezo kuelekea AFCON 2027, huku akiahidi FIFA kuunga mkono jitihada hizo.
Rais wa FIFA, Gianni Infantino amekutana na kuzungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda pamoja na ujumbe wake nchini Morocco, ambapo ameahidi kushirikiana na Tanzania katika kutengeneza fursa kwa vijana ili kunufaika na mpira wa miguu.