Baba Yetu uliye mbinguni. Jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu. Kama nasi tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi. Lakini utuopoe maovuni, Amina🙏
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limelazimika kuzima mitambo mitano kwakuwa majitaji ya umeme yapo chini huku uzalishaji wa umeme ukiwa ni mwingi.
TANESCO imesema hayo wakati Afisa wa Shirika hilo akiongea mbele ya Waziri Mkuu kwenye Maonesho ya Wiki ya Nishati yaliyofanyika Viwanja Vya Bunge Jijini Dodoma.
“Mh. Waziri Mkuu kwa sasa hivi tunavyopngea tuna mitambo karibu mitano ipo nje, haifanyi kazi yoyote ni kwamba tu mahitaji yapo chini uzalishaji upo mwingi kwahiyo tumeiweka tu stand by kwa ajili ya kusubiria mahitaji yakiwa juu tunaiwasha, karibia megawats 175, umeme tunaozalisha ni mwingi mahitajii ni madogo Nchi nzima, narudia tuna mitambo mitano minne Kituo cha Kinyerezi I na mmoja Kituo cha Ubungo III, hii mitambo tumeizima kwasababu mahitaji yapo chini na uzalishaji wa umeme ni mwingi imebidi tuizime, kuhusu mgao hamna mgao kwa sasa”
#MillardAyoUPDATES
SALA KABLA YA KULALA.
Sasa siku imekwisha,
kwako Mungu napandisha,
Moyo wangu wa shukrani,
Nipumzike kwa Amani,
Mema mengi umenipa,
Nashindwa kukulipa,
Baba mwema ondolea,
Yote niliyokukosea,
Yesu mpenzi nijie ,
Ombi langu usikie.
Unifiche mtoto wako,
Ndani ya jeraha Zako,
Ee Mama unipe neema,
Raha na usiku mwema,
Roho mlinzi kakeshe ,
pepo wasinikoseshe,
Naiweka Roho yangu,
Mikononi mwa Baba yangu,
Bila hofu napumzika,
Mwisho kwako nitafika.
AMINA.