@SuluhuSamia Mheshimiwa Rais @SuluhuSamia
UPENDO wa watanzania juu yako ni mkubwa sana... Endelea kuchapa kazi, Tuna amini miradi yote ya kimkakati inayo endelea nchi nzima imekamilika na ambayo haijakamilika itakamilika. TAIFA LETU KESHO YETU @tkmovement__
@TuliaAckson Pole sana Mheshimiwa, kazi ya Mungu haina makosa.... Umefanyika baraka katika Mkoa wa Mbeya hususani Mbeya Mjini hivyo msiba huu ni wetu sote maana umekuwa ukishiriki misiba mbalimbali bila kujali hadhi ya mtu MUNGU AKUBARIKI. 2030 chukua fomu ya Urais @TuliaAckson we love you!
@SuluhuSamia Mheshimiwa RAIS @SuluhuSamia nafurahishwa na namna unavyo tuongoza, Utendaji wako wakazi umeleta tija na maendeleo kwa taifa LETU. Changamoto zipo na wakati mwingine husabishwa na baadhi ya wasaidizi wako kutowajibika aidha kwa makusudi au kwakutokujua. @tkmovement__ TUPO NA WEWE
@nonitz01@MalisaGJ_@SuluhuSamia Changamoto za ki usalama zipo katika taifa letu na Serekali ndio wana simamia usalama wa raia na mali zao kupitia jeshi la polisi, nadhani jambo la msingi ni kuongeza uwajibikaji na kila mwananchi kuwa makini, @SuluhuSamia anatupenda hapendi haya yatokee kwani haya faida
TK Movement idara ya wanawake kwenye wiki ya Vijana inyofanyika mkoani Mwanza 🔥🔥
TK movement katika kuunga mkono jitihada za serikali na wadau kwenye lishe bora na kuhamasisha matumizi ya Nishati safi ya kupikia @SuluhuSamia#MamaYetuTaifaLetu#TaifaLetuKeshoYetu#SSH
Nikiwa na wananchi wenzangu wa Kitongoji cha Sokoine, Chamwino katika foleni ya kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024. Serikali za Mitaa ni Sauti ya Wananchi. Tujitokeze sote kujiandikisha na kushiriki Uchaguzi huu muhimu.
Siku nzuri ya kazi na mazungumzo na wananchi Mbinga ambapo pamoja na mambo mengine, kazi inaendelea katika ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay (kuwapa fursa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kufanya biashara ya uhakika kwenye Ziwa Nyasa) na ujenzi wa barabara ya lami ya kilometa 66, Mbinga hadi Mbamba Bay.
Faraja kubwa kuona miradi ya maendeleo inavyobadili maisha ya mamilioni ya wananchi katika kona mbalimbali za nchi yetu.
Ahsanteni sana Mbinga.
Ziara ya Kikazi Mkoa wa Ruvuma
Baada ya kazi kwenye mradi wa maji Mtyangimbole na ghala la nafaka Luhimba (sehemu ya maghala 28 ya nafaka tunayojenga katika mkoa huu, nilipata wasaa kusalimiana na wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Chief Zulu. Nimepokea zawadi yao ya shilingi 1,800 walipomuunga mkono mwenzao aliyeanza kwa kunipa shilingi 50.
Hongera kwa vijana wetu Taifa Stars kwa ushindi wenu dhidi ya Guinea katika hatua ya makundi kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Tunawaunga mkono na kuendelea kuwatakia kila la kheri katika hatua hii muhimu.