INASIKITISHA: Baadhi ya wanafunzi wa kike katika Shule za msingi na Sekondari Mkoani Mwanza, wanalazimika kufanya mapenzi kinyume na maumbile, ili kukwepa kubeba ujauzito kwa kuhofia kufukuzwa Shule. #update24
Klabu ya Chelsea imemthibitisha kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Frank Lampard kuwa kocha mpya wa timu hiyo. Uamuzi huo umefikiwa siku tisa tangu klabu ya Derby kuruhusu Lampard kufanya mazungumzo na Chelsea.#updates24
RCP ARUSHA ATANGAZA KUWA MCHUNGAJI: Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana, ameeleza kazi anayotarajia kuifanya baada ya kustaafu kazi ya Upolisi, anatamani kuwa Mchungaji wa kuhubiri Injili na si kuingia kwenye Siasa #update24
Waziri Mwakyembe: Mimi nawahakikishia kuwa mtaiona Taifa Stars mpya ndani ya miaka miwili ijayo. Mashabiki kazi yao ni kutazama mchezo uwanjani lakini kuna vitu vingi ambavyo kocha anajua. Ndani ya muda mfupi tutaitisha kikao kutathmini ushiriki wetu AFCON.#update24
#update24 Nchi ya Marekani imefanikiwa kugundua kifaa kipya kitakachoweza kutumia hata ukiwa nyumbani ambapo kimeundwa na kukubalika na taasisi ya kukagua dawa na chakula Marekani.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Kigwangala amesema Rais Magufuli atazindua rasmi Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato July 9 mwaka huu, Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato ilikua pori la akiba lililojulikana kwa jina la Burigi kabla ya kupandishwa hadhi.#update24
#update24 Jeshi la polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu watatu kwa makosa ya ulawiti na ubakaji wa watoto na wazee huku mtuhumiwa mmoja akiuawa na wananchi wenye hasira Kali baada ya kukutwa akimbaka mwanafunzi wa miaka minne.
AFCON 2019
Leo ni siku ya pili ya michuano ya kuwania ubingwa wa Afrika.
Kama huna mpango wa kuondoka kuitazama mechi maeneo fulani fulani, usiwe na hofu.
BBC Ulimwengu wa Soka itakutangazia mechi ya
DR Congo ๐จ๐ฉ v ๐บ๐ฌ Uganda mubashara.
Je karata yako unampa nani?#update24
Baadhi ya wadau wameichangamkia kauli ya mbunge wa jinbo la mtama Nape mnauye baada ya kutupia fumbo katika mtandao wake wa kijamii huku wakimuambiwa amefanikiwa kupita kwenye chujio lililomtoa Khadija Shaban, Taya maarufu kama Keisha.#update24
Umati wa watu wakiwa kwenye eneo la wageni wanaowasili tayari kwa kuipokea timu ya taifa 'Taifa Stars' kutoka nchini Misri katika michuano ya AFCON.#update24
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza katika Uwanja wa Ndege wa JNIA kwa ajili ya kuipokea timu ya taifa, Taifa Stars inayotarajia kuwasili leo mchana kutokea nchini Misri.#update24
RC Makonda: Hapa katikati tuliparaganyika kidogo, wapo waliokuwa wakiombea Taifa Stars ifungwe, wakifikiri kuwa ushindi wa Taifa Stars ni ushindi wa Makonda.#update24
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Asad amesema mwarobaini wa kuondoa rushwa kwenye sekta ya umma na binafsi ni kuweka uwazi katika kila jambo linalofanyika ikiwemo tenda mbalimbali.#update24
Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Kigwangala amesema Rais Magufuli atazindua rasmi Hifadhi ya Taifa ya Bugiri Chato July 9 mwaka huu, Hifadhi ya Taifa ya Bugiri Chato ilikua pori la akiba lililojulikana kwa jina la Bugiri kabla ya kupandishwa hadhi.#update24
BEIJING, CHINA: UWANJA MKUBWA ZAIDI WA NDEGE KUFUNGULIWA
> Uwanja huo wenye mita za mraba milioni 1.4 unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuhudumia wasafiri milioni 45 kwa mwaka ifikapo mwaka 2021 na kuhudumia watu milioni 75 ifikapo 2025.#update24
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Ijumaa July 05,atafanya ziara binafsi ya siku 2 hapa nchini kwa mwaliko wa Rais Magufuli,Kenyatta atatua uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na kuelekea nyumbani kwa Rais Magufuli Kijiji cha Mlimani ambako wawili hao watafanya mazungumzo.#update24
Instagram na Facebook nazo zimekumbwa na tatizo ambapo baadhi ya watumiaji wameeleza kushindwa kupakia picha, hukuwa wengine wakisema hawawezi kuperuzi picha. Baadhi ya watumiaji wa Instagram wanapata ujumbe kuwa picha/video zao haziwezi kupakiwa mtandaoni.#update24