#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 229
Anasimama Mhe. Lissu.
Anasema baada ya kusikiliza hoja za Wakili wa mleta maombi naomba nianze kwa kunukuu maneno ambayo Mahakama hii iliyasema kwenye kesi ya Commissioner General of TRA Criminal case namba 62/2022 pale ambapo maombi ya mdaawa yamezuiliwa na sheria, hawezi kufanya drafting ya kuhadaa Mahakama.
Wanasema uamuzi ulifanyika bila wao kusikilizwa, mgogoro ulianza 19 February 2026 ukurasa 391 wa record, Ugomvi ambao umetuleta hapa ulianza siku Tano kabla ya maamuzi ya Mahakama.
Wakili wa Serikali mkuu Renatus Mkude alisema "waheshimiwa Majaji tuko tayari kuendelea na mashahidi 3 lakini kabla ya kuendelea tuna notice of additional substance of evidence, ambayo imejazwa electronically siku ya Jana"
Katika ukurasa wa 392 Mahakama ikaamua kuwa tuendelee na mashaidi kwanza baadae tutarudi kwenye hoja za notice.
February 20, 2026 ukiangalia ukurasa wa 405-419 utayaona maneno niliyoyasema.
Mahakama ikaamua tumesikiliza sehemu zote kesi hii anahairishwa hadi jumatatu ilikuwa 23 February 2026 kuanzia ukurasa 420 unaonesha hayo.
Mkude akasema wako tayari kuendelea na Katuga akafanya submission in chief pg 421, 423 Katuga akajibu PO, nikafanya rijoinder, pg 428 kuna ruling of the court.
Baada ya submission ya Renatus, submission in chief ya Katuga, rejoinder yangu na reexamination in chief ndipo Mahakama ilitoa uamuzi.
Kwa record hiyo yote nguvu ya kusema hawakusikilizwa wanaitoa wapi?
Kwasababu ya maombi haya leo ni siku ya 139 kesi haiendelei kwa sababu ya uongo wao kwamba hawakusikilizwa.
Haki ya kusikilizwa ni haki ya kikatiba ni kweli sasa kwa ushaidi huu wanawezaje wakasema hawakusikilizwa?
Mmemsikia Wakili Katuga akisema Mahakama ilikosea ilipaswa iangalie reasonablity ya hiyo notice, ipokee ushaidi, iangalie competence kisha iamue.
This is an appeal under 6.3 wanayoitaja, it's only clever drafting inayolenga kuiadaa Mahakama.
Iangalie TRA vs New Musoma textile industry kwenye orodha yangu ni kesi namba 7 hawaruhusiwi kuleta malalamiko kuhusiana na hiyo notice kwenye Mahakama hii. Kifungu 6.3 cha AJA mamlaka ya Mahakama hii siyo hiyo wanayoiomba wao.
Ukurasa wa 21 unaonesha mjadala mpana wa ninachokisema sasa na inamaliza huu mjadala, hamuwezi kuanza kuangalia hiki kilicholetwa ni kitu gani mnapaswa kutazama je huu uamuzi ni legal.
Wanasema hawakusikilizwa mnaangalia kwenye record, Je ni kweli hawa watu hawakusikilizwa, hamuendi kwenye huu usikilizwaji ulikuwaje, Mahakama hii haiangalii mambo superficial.
Waheshimiwa Majaji mleta maombi alisikilizwa hivyo ruling ya mahakama ni legal, imeandikwa na Majaji wenye mamlaka baada ya kusikiliza pande zote hata kama hauwafurahishi wanapaswa kukubaliana nao.
Waheshimiwa Majaji waleta maombi hawana hoja yeyote ya maana on the basis of this record. Section 308 ya CPA imetajwa kwa lengo la kuwaalika mtengue kilichoamuliwa na Mahakama kuu nawaombeni msiende huko.
Nitasema kwa kifupi sana juu ya section 308 ya CPA na nini Mahakama ilisema inakataa kuongezwa kwa ushahidi mpya inadeal na Shaidi mpya tu.
Inazungumzia ni katika mazingira gani shaidi ambaye hakutajwa kwenye commital proceedings anaweza kuongeza kwenye trial, mleta maombi hapa analeta ushahidi mpya wa shaidi ambaye ametajwa kwenye commital na siyo shaidi mpya kama Sheria inavyotaka.
Anaendelea Mhe. Lissu
Kwenye uamuzi huu hakuna sehemu ambayo Mahakama imesema ushaidi huo haufai bali imesema ni ushahidi mpya na haufai kisheria.
Hii clever drafting in order to avoid the legal power, kama wanataka kupinga uamuzi huo wasubiri kesi iishe kisha wakapinge uamuzi huo.
Part 230 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo July 3, 2026
Last time kwenye ya Uhaini dhidi ya Mhe. Lissu tuliishia part 224 so leo tunaendelea na -;
Part 225
Mheshimiwa Tundu Lissu anaingia ndani ya chumba cha mahakama, ukumbi namba 01 wa Mahakama Kuu.
Anaonekana mwenye tabasamu na furaha usoni kwake kama ilivyo siku zote.
Upande wa Jamhuri wapo kama kawaida yao
Inapigwa Court…..
Jopo la Majaji watatu wanaingia,
Kesi inatajwa
Anasimama Wakili wa Serikali anajitambulisha jina lake Ajuaye kisha anatambulisha Mawakili wenzake.
Jaji anaamuliza Mhe. Lissu kama yupo tayari
Mhe. Lissu anasema yuko tayari kuendelea.
Kama kawaida yao anasimama Wakili wa Serikali Katuga kuweka pingamizi.
Mhe. Lissu anapendekeza maombi yake ya sikilizwe kwanza ndo pingamizi lao lijibiwe.
Majaji wanasema tuanze kwanza kusikiliza PO, kisha taratibu nyingine zitafuata.
Anaanza Mhe. Lissu Waheshimiwa Majaji kesi hii inatokana na maombi namba 19065 ya mwaka 2025, Juu ya maombi ya kuongeza ushahidi katika muendelezo wa kesi, uamuzi wa tarehe 24 February 2026 wa Mahakama Kuu wa kukataa kuingizwa kwa ushahidi mpya.
Waheshimiwa Majaji uamuzi wa February 24, 2026 ni uamuzi mdogo, uamuzi ambao haujamaliza shauri na kwa mantiki hiyo kisheria kabisa haupaswi kukatiwa rufaa au pingamizi.
Waheshimiwa Majaji wa rufaa, Mahakama hii katika kesi ya Mkurugenzi wa Mashitaka dhidi ya Mohammed Mussa Ussi criminal appeal namba 521 ya mwaka 2023 Mahakama ikiwa imeketi Zanzibar ilisema msingi wa kukataza rufaa ama mrejesho (revision) ya jinai msingi wa hiyo hoja ni kifungu cha 8.2.d kutokana na marejeo ya mwaka 2023 mahakama hii ilisema uamuzi huo hauwezi kukatiwa rufaa kwani ni uamuzi usiomaliza shauri.
Anaendelea Mhe.Lissu
Kesi ambazo nimeziwasilisha mbele yenu waheshimiwa Majaji zinazungumzia uamuzi mdogo ni wa aina gani na uamuzi unaoweza kutolewa kama uamuzi wa mwisho unaoweza kuombewa revision ni wa aina gani.
Uamuzi unaomaliza kesi na kunyima haki za wadaawa ndiyo unaopaswa kukatiwa rufaa, uamuzi unaokuwa treated as the final order ndiyo unaomaliza haki za msingi za wadaawa lakini kama uamuzi haufanyi hivyo hauwezi kukatiwa rufaa.
Sasa waheshimiwa Majaji baada ya kuwapitisha kwenye kesi hizo nirudi kwenye hoja yangu ya msingi je uamuzi wa February 24 mwaka huu ulimaliza kesi hii?
Kama ni hivo ulimaliza kesi hii na kwamba Sasa hivi sina kesi ya uhaini basi hoja yangu haina msingi na maombi haya hayawezi kusikilizwa.
Hoja yangu waheshimiwa Majaji ni kwamba uamuzi wa Mahakama Kuu wa February 24, 2026 haukumaliza kesi namba 19065/2025 na kwasababu haukumaliza maombi haya ya revision yanakatazwa kuletwa Mahakama ya Rufaa.
Anaendelea Mhe.Lissu
Waheshimiwa Majaji uamuzi huo unasema nini, ili tujue kama ulimaliza kesi lazima tuusome huo uamuzi unasema nini.?
Rulling yenyewe iko ukurasa wa 405-432, kwenye ukurasa wa 431 paragraph ya mwisho waheshimiwa Majaji mtaona Mahakama ilichokiamua.
Kilichokataliwa kupokelewa na Mahakama ni notice of additional substance of evidence, Mahakama Kuu haikusema kesi haitaendelea. Mahakama kuu ilitoa Mwongozo haikutoa uamuzi wa mwisho wa kesi, uamuzi wao ulikataa subodinate issue.
Waheshimiwa Majaji ushaidi mwingine huko kwenye maombi yenyewe yaliyoletwa. Mahakama inasema ilijadili na kukataa notice yao ya kuongeza ushahidi haisemi kesi ilifia hapo kutokana na uamuzi huo.
Mahakama imekata notice of additional substance of evidence, kwahiyo wanalalamikia uamuzi wa notice kukataliwa.
Jambo la pili ni Je mleta maombi anayo mamlaka ya kuiambia Mahakama itumie mamlaka yake ya kupitia kumbukumbu ili kuridhisha matakwa yake mwenyewe?
Jibu ni hapana hiyo siyo haki yao kisheria kwani wajibu wa kuangalia record ni wa mamlaka yenyewe.
Part 226 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
Sema hili Picha ni underrated sana, hili picha linatakiwa liwekwe pale Mbezi, kuwakumbusha vijana mawakili wanaosubiria ajira wakiwa ndani, liwakumbushe vijana haki haiombwi inapiganiwa.
Mwaga moto kwa hii timu kama unaikubali 🔥 📌
Lissu anamuomba hiyo nakala ya hiyo kesi. Katuga anasema ipo mtandaoni. Lissu anamuuliza uko serious kweli mimi niko jela unasema uamuzi wa Mahakama uko mtandaoni? Jamaa wameenda kutafuta huo uamuzi. 😂
Mh. Tundu lissu 🔥🔥🔥
Repost bila kuchoka ✌️
Kesho NCHI NZIMA itakuwa darasani kupata shule ya SHERIA Kutoka kwa BABA WA HAKI.
Tutakuwa live wanangu mwaga moto hapo chini kama hutakosa.
Repost 200
HII COMEBACK imepigwa USIKU WA MANANE bila shaka hawa ni Gen Z wa Diaspora😁
Bado masaa 24 Tukamilishe zoezi letu la "FUNGA MWAKA NA LISSU" Jambo hili ni kuonyesha mshikamano na BABA YETU huko Gerezani.
Tumezuiwa kuenda kumuona kwa zaidi ya siku 271, hatuna njia nyingine ya kufikisha salamu zetu zaidi ya hii. Tushambulie kwa miamala asije kujiona yupo pekeake.
Hii ikamtie moyo huko Gerezani kuwa VIJANA ANAOWAPAMBANI BADO WAPO NAE NA WANAVUKA NAE MWAKA KIBABE.
Salamu hizi ni Chukizo kwa WAKOLONI WEUSI, HAWAPENDI NA WANAUMIZWA SANA-TUTUMIE HII KAMA NJIA YA KUWAKERA KWA WINGI WETU WA MIAMALA.
KUNA SISI TULICHANGA JANA, LAKINI KWASABABU NI FUNGA MWAKA NA LISSU NA LEO NDIO SIKU YA KUFUNGA MWAKA TUNACHANGA NA LEO TENA MAMAE TUPO NJE YA MUDA WANANGU.
MWAGA MOTO KAMA MADRAGON, NAMBA ZA KUTUMA MCHANGO ZIPO KWENYE BANGO HAPO TUSHAMBULIE CHAP CHAP MAGEN Z🔥😆😆
REPOST 200
TUTAKUWEPO🫵😎
⛔️ Viewer discretion is advised!
‼️🚨ANOTHER MORTUARY ON OCT 30 - MOUNT MERU HOSPITAL IN ARUSHA‼️
The mortuaries were full of bodies mostly young men and women
This is the what the butcher of Kizimkazi @SuluhuSamia did when they switched off the internet! These bodies were disposed off and that is where the cover up began
@SusanNamondo your failure to act swiftly to bring in international independent investigation team will be on your CV forver - act now!
This is URGENT
Cc @volker_turk@AminaJMohammed@antonioguterres @OHCHR_EARO @UN@UnitedNationsTZ@UNHumanRights
#SamiaMustGo
Hii ni tarehe 30 Oct pekee sasa kumbukeni hadi Nov 3-4 walikuwa wanabeba na kutokomea hadi na wagonjwa kibao KILA SIKU kutoka mahospitali yote!
Kuna shujaa kafunikwa na bendera yetu 🇹🇿 Chozi limenitoka! Mkaenda kuzichoma sijui kuzifukia! Washenzi mbwa ninyi 🚮
Mashetani wakubwa! Na Shetani mkuu ni @SuluhuSamia
Lazima Jezebel aondoke au aondolewe MARA MOJA!
Mnasubiri nini mlio karibu naye? Huyu asubuhi na mapema tumkute gerezani!
#TanzaniaMassacre
Nimetoka Ukonga kumuona Mwenyekiti, Yuko imara na anawasalimia wote.
Anatoa pole kwa Watanzania wote waliopoteza maisha, familia ndugu na marafiki.
Anatambua watu waliopoteza viungo na kubaki na ulemavu.
Ametoa pole kwa wote waliopoteza mali pia.
Damu ya wenzetu haijamwagika bure na hakuna atakaefunika jambo hili bila uwajibikaji.
Msimamo wa Mwenyekiti uko thabiti, Yuko imara na mwenye afya njema.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 150
Anaendelea Mhe. Lissu
Hivyo naomba sheria hii kama Jaji Mtembwa aliitumia, naiomba Mahakama hii isiendelee kukosea, isiendelee kuitumia.
Waheshimiwa Majaji mkiangalia sheria namba 7 ya 2018 utaona imeandikwa kwenye header note kuwa sheria hii imetolewa kwenye gazeti maalum la Serikali la tarehe 15 Septemba 2018, waheshimiwa majaji huo ni uongo.
Uthibitisho kuwa ilichapishwa kwenye gazeti la serikali ni kulitoa gazeti lenyewe, proof sio what the law says, bali ni physical existence or electronic existence.
Nawaomba waheshimiwa majaji msiitumie hii sheria, msipoitumia maana yake mashahidi waje watoe Ushahidi hadharani, hii ya kufichaficha mashahidi gizani haitakuwepo kabisa na haitakiwi kabisa kuwepo.
Anasimama Wakili wa Serikali Nassoro Katuga yupo kama amechanganyikiwa au ametoka kubeba gunia la mchanga ni mdogo kama Pilton.
Amesimama akiwa amenywea sana na kusema,
Kwa hoja nyingi zilizoletwa tunaomba muda wa kujiandaa kujibu hoja nyingi sana ambazo mshtakiwa amezisema.
Tunaomba tarehe ambayo tutapangiwa kwaajili ya kuja kujibu.
Lissu hajapinga ila ameomba tarehe ya karibu zaidi wapewe.
Kesi imeahirishwa kwa muda usiojulikana hadi pale ambapo Mahakama itatoa Notisi ya siku ya kusikilizwa kwasababu notisi ya awali ilionyesha mwisho wa kusikiliza kesi hii ni leo Novemba 12, 2025.
Naomba Repost yako.
Tunahitaji SAINI 20,000 kabla ya saa 6 usiku. Mpaka sasa tumepata 16,420. Naomba usaini na Share kwa wengine chap chap. Usilale kabla hujasaini hii ni Muhimu kwaajili ya ndugu zetu waliouliwa KIKATILI NA SAMIA.
REPOST 500
https://t.co/hMj55Mczjm
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Novemba 10, 2025
Last time tuliishia part 144 so Leo tunaendelea na-;
Part 145
Imepigwa Courttttttttt.
Majaji wanaingia sasa.
Watu wamesimama na kuinama kutoa heshima.
Majaji wanakaaa na karani anasoma namba ya shauri.
Mheshimiwa Lissu hajaletwa leo maana kesi inasomwa bila mtuhumiwa.
Mawakili wa Serikali yupo Job Mrema, Thawabu Issa na Cathbert Mbiringe.
Naona wanateta jambo hapa kimya kimya.
Majaji nao wanateta jambo sijui wanaambiana nini? Kuna kimya kinatawala kidogo.
Hata wale maaskari magereza ambao huwa wanamleta Mh. Lissu leo hawapo kabisa. Wapo wengine. Sijui kwanini hawajamleta.
Anasimama Wakili wa Serikali sasa, anajitambulisha na kuwatambulisha wenzake.
Anasema Waheshimiwa Majaji kama mnavyoona Mshitakiwa hayupo mahakamani na sababu za kutokuwepo ni suala la usalama kuwa mdogo.
Hivyo tunaomba tupatiwe ahirisho la siku 14 ili tuweze kuja kuendelea kama usalama utakuwa umetengamaaa. Leo ameshindwa kufikishwa kutokana na sababu hiyo tuliyotoa ya hali ya usalama waheshimiwa Majaji.
Wakili Thawabu Issa ndio anayeiaddress Mahakama.
Anaendelea kusema wao hawakujua kama Mshitakiwa hataletwa walipofika Mahakamani wakashangaa hawamuoni ndio wakaamua kuwasiliana na Mkuu wa Gereza ndie amewaambia kuwa hawatamleta kwa sababu za kiusalama.
Thawabu kanyanyuka hapa na inaidress Mahakama ya kuwa Leo wameshindwa kumleta TAL kwa sababu za kiusalama hivyo wanaomba hairisho la siku 14 waweze kuendelea.
Jaji anawasha kipaza sauti na kusema;
Mahakama baada ya kusikiliza hoja za State attorney inasema kwa leo hatutaendelea kwa kuwa mshitakiwa hajaletwa.
Lakini tunaelekeza kwa State Attorney next time waseme hizo sababu za kiusalama ni zipi zinazofanya hadi shauri liahirishwe?
Na pia Mahakama haiwezi kuwapa siku 14 kama walivyoomba hivyo shauri linapangwa tena kusikilizwa tarehe 12/11/2025 (Jumatano ya wiki hii) na summons za mashahidi na Mshitakiwa zitolewa na kesho zifuatiliwe na wahusika wafikishiwe.
Kwahiyo tunaomba tukutane hapa kesho kutwa.
Inapigwa High Courttt nyingine kubwa na ya kidaku sana wanasimam Majaji wanatoka.
Leo Jamhuri wameweka mpira kwapani tena.
Kumbe Nchi yetu haiko salama kabisa.
Tulidanganywa mambo yanaendelea kama kawaida lakini Magereza na Mawakili wa Serikali leo wanatuambiana Mahakamani nchi sio salama kama watu wanavyoweza kudhani.
Ndio maana barabara na vyombo vya kumleta Lissu Mahakamani vimeshindikana.
Leo siku imekuwa fupi kihivyo.
So Tukutane Hiyo Tar. 12/11/2025 saa tatu kamili asubuhi.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 89
Wamesimama Mawakili wa Serikali wanasema tunapinga nyaraka kupokelewa kwasababu hatua hazijafuatwa.
Wanasema Mhe. Lissu hajacontradict anataka ipokelewe.
Mhe. Lissu anawajibu Waheshimiwa Majaji wao wenyewe waliniletea hizi kesi siku ya kwanza leo nimetumia utaratibu huo huo ambao waliusema wao na kuniletea kesi tena wameona nongwa.
Kwanza wanasoma sana kesi ya High Court wakati kesi ninayoitumia mimi ni kesi ya Mahakama ya rufani.
Kwahiyo naomba maelezo ya shahidi yapokelewe.
Wanarudi kufanya rejoinder Mawakili wa Serikali amesimama Igans Mwinuka, anasema Majaji mimi sipingi kabisa alichosema kuhusu kesi ya Mahakama ya rufani nakubaliana nayo kabisa.
Hivyo hata hiyo kesi utaratibu wake ni huo kabisa.
Hajaonesha hizo contradiction ni hayo tu.
Majaji wanaandika hapa kidogo.
Jaji anasema na sisi tunahitaji muda kidogo tuweze kwenda kuandika uamuzi mdogo.
Tutaendelea Jumatatu asubuhi itakuwa ni tarehe 13/10/2025.
Kesi imehairishwa mpaka siku ya Jumatatu asubuhi.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 6
Anaendelea Mhe. Lissu
Katuga anasema kifungu cha sheria 266(1) cha CPA kwamba nyaraka nitapewa trial ikianza.
Hoja yangu ni kwamba what is a trial?
Sasa ngoja niwapeleke kwenye Black's Law Disctionary ni likitabu kubwa sana jekundu mtoto wa miaka mitano habebi. Analifungua kwa mizuka.
A trial does two things, examine evidence and adjudicate legal claims. Hiyo ndio trial.
Sasa hapa tuna àdjudicate legal claim. Hatujafika kwenye mashahidi lakini tayari tuko kwenye trial tunajadili masuala ya kisheria.
Sasa kama mahakama hii haiko kwenye trial ipo kwenye nini hapa?
Kwenye kesi zote ambazo mahakama kuu ina original jurisdiction.
Lazima zije hapa kupitia committal proceedings. Iwe ya Kisutu au ya Mbinga.
Sasa kama mahakama ya Kisutu haikuwa na mamlaka maana yake kazi yao ilikuwa ni SUFULI.
Hii ameitamka kama nilivyoandika. Kaitamka kinyaturu kabisa🤣🤣
Anaendelea kwahiyo kinachoendela hapa ni SUFULI pia.
Hatuwezi kuendelea na mambo ya SUFULI. yaani sifuli au zero.
Ndio anamaanisha hapo muelewe.🤣
S. 263 ya CPA aliyoisema Katuga sasa nakala niliyopewa ina kurasa 16 na nilipoanza kusema mambo yako tofauti ndio ikabidi nipewe rekodi za mahakama.
Sasa Katuga alikuwa ana justify anasema utaratibu tuliokuwa tunatumia siku zote ni huo.
Mambo ya practical experience kama ni kweli wamekuwa wanafanya hivyo. Basi naomba niseme huo ni uzoefu katika uvunjaji wa sheria.
Unajisifia uzoefu kuvunja sheria hoja hapa ni sheria inasema nini? Kama wao wamekuwa wanavunja sheria basi mahakama hii isiwakubalie kuendelea uzoefu huo.
Na kuna kifungu naona kama kinawatatiza sana na hawakielewi mawakili wa serikali sasa naomba nikisome ili wakielewe.
Anakisoma hapa. Mhe. Lissu nae anapiga Kingereza fulani ambacho sijui kama hawa Mapolisi angeamua kuwa anaongea nao kingereza huko Polisi wangeweza kumuhoji lolote.😁😁😁
Anaendelea hapa Mhe. Lissu.
S. 263(6) of CPA inasema nyaraka gani napaswa kupewa na mahakama ya ukabidhi na mimi sijapewa hizo nyaraka.
Practical experience itatupeleka kwenye shimo refu sana.
Katuga amehoji kwamba kuna criminality kuhusu nyaraka. Katuga anasema je hizi nyaraka ni za kughushi?
Waheshimiwa majaji naomba niseme Na nitafafanua.
Sio tu kuna ushahidi wa kughushi bali kuna conspiracy to defeat justice.
Anasimama Katuga anasema conspiracy haikuwepo asiende huko.
Lissu anasema siendi subiri sasa.
Waheshimiwa majaji sorry makaratasi yamekuwa mengi.
Kwanini nasema kuna forgery
1. Niliyopewa ina kurasa 16 na iliyopo mahakamani ni 101
2. Scanned berg pia nyaraka ya mahakama lakini ile ya karatasi 18 haikuwa na uthibitisho kuwa ni nyaraka ya mahakama na imeletwa na mahakama na ameitoa Kiswaga. Nikapewa
3. Inaanzia tar. 18 na inaishia siku hiyo hiyo. Document ya mahakama inaanzia tar. 10/04 hadi 18/08
4. Angalia ukurasa wa 1 wa nyaraka niliyoletewa gerezani haina submission kwenye page 1 lakini page ya 86 ya document ya mahakama inaonesha kulikuwa na submission page 86. Mahakama ilitoa uamuzi nyaraka inaonesha.
Aliyetengeneza hizi nyaraka alikuwa na nia gani kama sio kughushi ni nini?
Na Katuga alisema tuangalie kifungu cha 393 kuhusu forgery lengo ni kudanganya.
Hiyo nyaraka ilikuwa na lengo la kunideceive. Inawezekanaje kesi ya miezi mitano inaletwa rekodi ya siku what was the intent if it was not to deceive?
Part 7 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 8
Anaendelea Mhe. Lissu
Katuga jana anasema mahakama ilikuwa inapewa sababu na mahakama inaamua.
Sasa nimwambie Katuga S. 265 inasema sababu zinazohitajika ni za mahakama na sio za wakili wa serikali.
Alipaswa kutuambia mahakama ilisema nini wakati inaahirisha na sio Katuga aliiomba nini ili mahakama iahirishe.
Ni anakili kuwa mahakama haikuwa inatoa sababu ila sababu zilikuwa ni zake.
Hakuna mahakama imezifanya hizo sababu kuwa zake na kuzitoa yenyewe.
Wakili wa Serikali Mkuu, Katuga anasema utaratibu uliofanywa na Hakimu Kiswaga na yeye kuandika amri zake nje ya amri zilizotolewa na Jaji Mtembwa.
Sasa naomba niseme kwamba kuna ukiukwaji wa sheria hasa kwenye committal proceedings zinajumuisha proceedings za sect. 194 za witness protection measures.
Nilisema mtakumbuka effect ya mahakama kutoa amri ya kuficha mashahidi.
Amri ya Jaji Mtembwa hakikisheni mnaficha utambulisho wa hao mashahidi. Sasa clearly S. 194(2) cha CPA hakikuzingatiwa.
Sasa wao wamenipa nyaraka ambazo zina ninafanya niwafahamu hao mashahidi.
Kanuni ya 8 inasema endapo amri ya ulinzi imetolewa nyaraka zote zinazohusiana na amri ya ulinzi vitaambatanishwa na kupewa mtuhumiwa.
Sasa committal proceedings zilitakiwa kuendeshwa kwa mujibu wa amri ya Jaji Mtembwa na sio amri ya Franco Kiswaga PRM.
Amri ya ulinzi ya Jaji sio ya Franco Kiswaga. Ieleweke hivyo.
Waheshimiwa majaji wakili wa serikali sikuonesha sheria iliyovunjwa?
Sasa nilipaswa kuonyesha nini zaidi ya haya?
Kwa kumalizia hiyo hoja, Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu haikuwa na mamlaka yoyote once the high Court made six orders the commitall Court was duty bound to respect and act in accordance with the High Court directives.
Sasa mahakama kuu itaendeleaje kwa kutumia committal order ambayo haikuzingatia amri ya mahakama kuu.
Magistrate should not in this country have power to vary orders of superior courts.
Wakili Kiswaga sorry Wakili Katuga.
Alisema kwani kulikuwa na shida gani kwa mahakama kufunga live streaming wakati yenyewe ndio iliyotuhusu hiyo live streaming.
Kwahiyo tulipata kwa ufadhili wa mahakama na na imeondoa kwa ufadhili huo.
Rekodi ya tarehe 13 au 18 nilisema pale Kisutu kuwa wayu wa nchi hii wana haki ya kikatiba kuona kinachowahusu. Kesi ya uhaini niliwaambia juzi kuwa they come once every two generation.
Nilisema juzi kuwa kwenye katiba yetu inasema kwamba kosa kubwa kuliko yote ni kosa la uhaini.
Mahakama ya hakimu kisutu iliombwa ikakubali na yakatangazwa karibu miezi miwili.
Anaendelea Mh. Lissu Mahakama kuu haikukataza live streaming, haikukataza publication of the proceedings. Hayo hayakukatazwa.
Yaliyokatazwa nilishasema na anayataja hapa kutoka kichwani amezikalili zozote.
Sasa haya ya kisutu yalitokea wapi? Kiswaga alisema ukisema hata kwenye social media utaenda jela. Sasa wapi Mtembwa alizungumzia watu kupost kwenye mitandao.
Amri ya Kiswaga ilikuwa kinyume na sheria na kinyume na amri ya Mtembwa.
Sasa kila saaa tunasikia hilo tu, hiyo tu. Ndio tufute proceedings yote? Wanasema hivyo.
Sasa naomba tuelewane kuwa tunapaswa kuziangalia hizi irregularities that was very systematic.
If that was the case mahakama kuu haiwezi kuassume hizi records za namna hii.
Waheshimiwa Majaji naomba sasa nizungumzie yale maelelzo ya mtuhumiwa.
Wakili Kiswaga ala samahani sana. Alisema huo utaratibu wa s. 263(4)(5) ya CPA unahusika pale mtuhumiwa anapokiri kosa tu yaani admission au confession.
Kwamba baada ya kukiri asomewe hayo maneno yake ili aongeze hayo maneno ndio anasema hivyo.
Kwa vile mimi sikukiri kosa kwahiyo hakukuwa na sababu ya mimi kupewa nafasi.
Kwa maneno hayo nashukuru upande qa jamhuri wanakubali kuwa hayo masharti hayakufuatwa.
Na hayakufuatwa kwasababu sikukiri kosa.
Part 9 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 9
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa hoja ni je yanayozungumzwa kwenye hivyo vifungu yanazungumzia confession peke yake?
S. 263(3) of CPA inasema you may say anything that relevant to charge against you and will be written and may be used in evidence at your trial.
Sasa kwenye kifungu hiki kuna admission yoyote?
Kesi ya Dodoli Kapufi mahakama ya kabidhi hairuhusiwi kufanya maamuzi ya maswala ya kisheria 266(6)
Anasoma hapa hiki kifungu....
Anaanza kuelezea hapa kwamba Hakimu alipaswa kuandika maelezo ya Lissu kama yalivyo na sheria imeandika kabisa kuwa inampasa na kumlazimu kuandika maelezo hayo ila mahakama ya kabidhi ilizuia maelezo hayo kuandikwa.
Kwahiyo Waheshimiwa Majaji haya maneno niliotakiwa kusema yalikuwa ushahidi wangu unaopaswa kutumika kwenye mahakama hii.
Wakili Katuga anasema bila kusomewa hayo maelezo Lissu kaathirika vip?Lissu anajibu kuwa maelezo yangu ambayo ni ushahidi hayakuchukuliwa hio ilikuwa kinyume na sheria na kinyume na haki.
Anaendelea hapa anasema twende kwenye mashahidi wangu mtakumbuka mashahidi aliowataja walikuwa Rais, Waziri Mkuu, Makamu Rais.
Ukisema Shahidi yangu Yesu basi atakuuliza nipe anuani yake hiyo ndio gist ya 264 ya CPA.😂
Sio kusema sitaki kuandika.
Presidential affairs Act imesemwa jana na imerudiwa leo hii mahakama hii imeambiwa kuwa hawa wana kinga za kupewa summons za mahakama kuja kitoa ushahidi mahakamani.
Mmesomewa kifungu cha 10 jana kilitajwa cha 9 leo wamerekebisha.
Anasoma kifungu cha 10 cha Presidential Affairs Act. .....
Kwahiyo Rais hawezi pelekewa Summons ya Mahakama kwa maneno hayo niliyosema.
Sheria inasema unatakiwa umuone Katibu Mkuu Kiongozi au Katibu wa Rais au Katibu Mkuu baada ya kuombwa na mahakama wa kuomba msaada wa kumserve Rais huyo Katibu wa Rais au Katibu Mkuu kiongozi watatoa utaratibu.
Sasa haya ndio yanayotoa zuio? Au wanasoma sheria kwa namna gani?
Walisema kifungu hiki kinawahusu Waziri Mkuu na Makamu wa Rais sasa katika kifungu hiki wapi wamesemwa hawa aliowataja Mrema leo?
Sasa Mheshimiwa Jaji kuna kitu hakisemwi naomba nikiseme mimi.
Sect. 9 ya sheria hiyo ya Sasa. Presidential Affairs Act.
Kinasema immunity of Arrest au kumlazimisha aje mahakamani.
Sasa mimi nimeomba Rais akamatwe? Hakuna nilipoomba.
Kifungu cha 9 kinasema kama yupo mtu atahitaji Rais awe shahidi Mahakama itamnotify Rais kuhusu nia ya mtu huyo.
The court is required to notified the President. Ana kinga ya kutokushitakiwa tu na sio kinga ya kuja kutoa ushahidi.
Mahakama inapaswa kumpelekea Katibu Mkuu kiongozi au katibu wa Rais na hao wanapaswa kuisaidia mahakama kumfikishia Rais sio kwa mujibu wa sheria kuwa jambo hilo limekatazwa. Sio kweli.
Hiyo hoja ni ya bure. 😁😁😁
Naomba sasa nijielekeze kwenda kusoma haya maamuzi waliyonipa ili tuweze kurudi kesho nije kujibu kuhusu hayo.
Jaji anasema Katuga unasemaje.
Katuga anajibu kuwa mimi sina shida. Akasomeee tukutane kesho.
Majaji wanateta hapa kidogo.
Wanaandika wakiwa wameinama chini. Tusubiri maelekezo. Kuna dalili tutakutana kesho hapa.
Jaji anasema kutokana hakuna pingamizi lolote tunaahirisha shauri hili saa tatu asubuhi kesho tutakuja kukusikiliza umalizie
Shauri limeahirishwa hadi kesho asubuhi saa tatu.
Naomba repost kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 6
Anaendelea kuongea Mhe. Lissu
Kifungu kinasema hicho cha 265(1) of CPA kinasema kama kuna haja ya kuahirishwa kwa shauri basi mahakama itaamuru mtuhumiwa apelekwe gerezani kwa siku 14.
Mahakama inapaswa kusema kwanini kesi imeahirishwa? Kila siku lazima iandike hivyo.
Naomba niwapeleke sasa kwenye hizi records za kutoka Kisutu.
Mimi nilikamatwa tar. 09/04/2025 usiku Mbinga hadi Dar es salaam usiku kwa usiku nakufika Dar es salaam niisafirishwa.
Niliwekwa pale Shimoni police central.
Tar. 10 hiyohiyo nilipelekwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu kusomewa hili shtaka la uhaini.
The treason charge was read on 10/04/2025 pale Kisutu.
Nikapelekwa gereza la Keko hiyo tar. 10/04/2025.
Ilisema kesi itakuja tar. 24/04 tena.
Hawa majaji hawamuingilii kabisa Mhe. Lissu tofauti na kule Kisutu labda wabadilike kwenye eneo hilo huko mbele.
Ta. 24/04 wakati naenda Kisutu nilikuwa natokea Ukonga sio Keko tena.
Waliahirisha kesi siku hiyo hadi 19/05/2025 kwamba upelelezi bado.
Walisema pia upelelezi bado ikaahirishwa 02/06 na mara zote nimerudishwa gerezani na leo ni 153 siku niko gerezani.
Tar. 16/06 ikaahirishwa tena, upelelezi bado ndio sababu yao.
Tar. 01/07 nikapelekwa ikaahirishwa tena na mahakama ikasema tar. 15/07 ikaahirishwa tena walikuwa hawajajiandaaa ndio walichosema mahakamani.
Tukarudi tar. 30/07 ikaahirishwa tena na muda wote napelekwa gerezani na ninakaa na wafungwa waliohukumiwa kifo.
Tar. 13/08 tukarudi tena Kisutu ndio upande wa mashitaka wakasema wako tayari.
Ikaahirihswa tena lakini mpaka tarehe 18/08 ndio mahakama ikafanya kile kinachoitwa Commitall hearing.
Sasa Wah. Majaji imeahirishwa mara 10 kuanzia 10/04 na 18/08 mwaka huu.
Muangalie hiyo record kuanzia tar. 10 hiyo yote yaliyofanyika yako wapi kwenye hii record yako wapi?
Yaliyopo humu ni ya tarehe 18/08 tu ndio yameletwa huku mahakama kuu.
Hayo mengine yote yako wapi?
Kwanini wameficha wanaficha nini?
Kesi imeahirishwa zaidi ya mara 10 lakini kwenye hizi records hayapo kabisa.
S. 265(1) ya CPA ukiahirisha hata mara moja lazima uandike sababu za kuahirisha.
Records ziko kimya tena UKIMYA WA KABURINI.
Hazisemi chochote kuhusu hayo mengine yaliyotokea huko nyuma.
Waheshimiwa Majaji naomba niwapeleke kif. Cha 266(3) cha CPA
Amesimama KATUGA anasema Mh. Tunaona kama mwenzetu amepewa proceeding fupi tofauti na tulizonazo na sisi.
Mh. Lissu amemjibu kuwa nilichopewa ndio hicho na ndio ninachokisema hapa Mahakamani kuwa nimepewa nyaraka zinazoanzia tarehe 18/08.
Mahakama imeibua vicheko. 😂😂😂
Jaji anasema wahudhuriaji wawe watulivu tafadhali. Majaji wanaandika kidogo.
Mh. Lissu amewapa proceedings ambazo amepelekewa ili majaji nao wazipitie na kusoma kama kweli ziko sahihi au haziko sahihi.
Kimya kimetanda hapa. Hali ya hewa imeshachafuka.
Kuna wahuni nafikiri walishafanya kazi yao.
Ngoja tuone. 🤣🤣🤣
Majaji wanateta na kushauriana.
KATUGA yeye anazo proceedings zilizokamilika.
Halafu Mh. Lissu wamempelekea gerezani proceedings ambazo hazijakamilika.
Part 7 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.