Dk. Juma Omera, Waziri wa Katiba na Sheria naye alinukuliwa akisema yafuatayo juu ya Katiba Mpya:-
“Mchakato wa Katiba Mpya utaanza rasmi baada ya kufikiwa maridhiano ya kitaifa”
Kwa kauli hizi za viongozi wenzie na Nchimbi, utabaini mwanzoni kabisa Mh. Rais hakuwa hata na wazo la Katiba Mpya alipodai “kuna kazi nyingine za kufanya kuliko kubadilisha Katiba”
Baada ya maafa ya Oct 29, rais anarudi nyuma kidogo kwa kuizungumzia Katiba Mpya lakini akiweka sharti kuwa jambo hili linapaswa kutanguliwa na maridhiano kauli ambazo Mwigulu na Homera wakazitumia pia.
Sasa hapa ndipo wakosoaji wanajiuliza kama ndani ya serikali kuna mawasiliano ya pamoja yenye lengo la kutuletea katiba mpya?
Wengi wamejiuliza kama Nchimbi anaona kitu cha kwanza ni “kupambana” kuipata Katiba Mpya, hakuona kama kuna sharti la maridhiano kutoka kwa bosi wake?
Au inamaanisha Nchimbi anatushauri katika hayo mapambano ya Katiba Mpya tuharakishe kuridhiana ili tuifike nchi ya ahadi mapema?
Kama maridhiano ndio njia ya kufikia katiba mpya je, Serikali yake kwa upande wake imeandaa njia bora ya kufikia maridhiano wakati wakosoaji wa serikali wanaendelea kuitwa magaidi na kupewa kesi za ugaidi na uhaini?
Baada ya hotuba ya Nchimbi, tayari ndani ya CCM, wameshajitokeza watu wanaopingana naye hadharani huku wengine wakimfananisha na muasi.
Mwana CCM mmoja akafikia hatua ya kumtaka Nchimbi aachie kiti cha umakamu ama kwa hiyari au kwa kuondolewa.
Namnukuu,
“Walk away willingly, or be forced out. Your choice.
Mwingine akahoji inawezekana vipi Makamu ambaye ndiye ameshiriki kuandika Ilani ya CCM asilete katiba mpya? Au makamu anacheza game na wanaharakati wampende?
Maoni haya kutoka kwa watu hawa sijayapuuza hata kidogo nikianza kuamini sasa kumeanza kuwa na wazo la either kumtaka VP ang’atuke kwa hiyari au ambanduliwe (be impeached)
Tulishawahi kuona hali kama hii punde tu marehemu Spika Job Ndugai alitotofautiana na mwenyekiti wake juu ya mikopo ya serikali.
Spika aliishia kuondolewa na ikinong’onwa kuwa hata ile barua ya kujiuzuru hakuwa ameidraft yeye mwenyewe
Lakini katiba inasemaje kuhusu ukomo wa kiti cha Makamu wa rais?
Ibara ya 50(2) ya katiba ya JMT inasema Kiti cha Makamu rais kinaweza kukoma kwa sababu zifuatazo:-
(a) Ukiisha muda wake wa utumishi wa miaka mitano
(b) Akifia madarakani
(c) Akijiuzuru
(d) Akiwa rais baada ya nafasi ya urais kuwa tupu (e.g Samia kwa Magufuli)
(e) Akikutwa na hatia ya jinai
(f) Akiapishwa rais mwingine
(e) Akiondolewa na bunge kwa kufata masharti ya ibara ndogo ya (50)(3) nitafafanua
Tukianza na masharti hapo juu, endapo Nchimbi hatajiuzuru au nafasi ya rais haitabaki tupu, kukutwa na hatia ya jinai au kupatikana rais mwingine, ndoto hii ya watu hawa itakuwa ni ya mchana.
Bila hayo, nafasi ya Nchimbi itakoma baada ya kuisha muhula wa miaka mitano
Sasa tuelekee ibara ndogo ya (3) katika ibara ya 50 ya katiba ya JMT
Ibara hii inaongelea jinsi ya kumng’atua rais au makamu wake
Ibara inasem kuwa “Bunge linaweza kuwa na mamlaka ya kumuondosha makamu wa rais , kwa kuzingatia tu masharti yafuatayo;-
(a) Endapo rais atawasilisha kwa Spika cheti cha daktari kinachothibitisha makamu hawezi kuendelea na majukumu yake kama makamu wa rais
(b) Endapo Makamu atathibitika kufanya vitendo vinavyokiuka katiba na sheria za uongozi wa umma
(c) Amefanya matendo yanayokiuka misingi ya usajili wa vyama vya siasa
(d) Matendo yake binafsi yanaidhalilisha ofisi ya rais wa JMT
Kwa ibara hii ndogo, endapo Makamu hataugua kiasi cha kuwa “incapacitated” kimwili na kiakili, hii pia inaweza kuwa ndoto ya mchana.
Labda ilazimishwe kuwa, Kauli za Makamu kukinzana na za bosi wake, inaweza kuwa sawa na kuidhalilisha ofisi ya rais
Hatuombei haya yatokee kwa maslahi mapana ya JMT, lakini hizi kauli za Yuda, Shetani, Msaliti nk bila kukemewa hadharani, zinatuweka sana rada.
Sie yetu ni macho tu
Umuofia kwenu Paratroopers
@Ntahondi_@fbuyobe Ni neno la kibantu lenye maana ya kijipere. Kijipere kina tabia ya kujipitisha kwenye nguo uliovaa ili mradi tu usipate uturivu wa nafsi. Ndipo neno "kiherehere" lilipotokea.