Huu tunaijua ni UONGO mtupu ila hata kama ni kweli sisi inatuhusu nini mambo ya Mtu na familia yake. Let's assume ni kweli taarifa hizi zinatusaidia nini ?
Matopeni Hon. Lissu Jela Acheni Ngonjera na NGEBE.
#FreeTunduLissu
'Karia alisema mimi natishwa mkuu'
Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Paul Makonda ameyasema haya wakati akitolea ufafanuzi sakata la mkataba wa jezi za timu ya taifa ya mpira wa miguu.
Moja ya mambo hatari zaidi kwa taifa ni kuruhusu wanasiasa kuchezea mhimili wa Mahakama. Mahakama inapaswa kusimama juu ya sheria na haki, si chini ya matakwa ya wanasiasa.
Uhuru wa Mahakama ni nguzo ya kulinda haki za wananchi na mustakabali wa taifa.
Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo, Paul Makonda (Mb) amesema hakuna mahala ambapo wamekubaliana bei ya jezi iweje ili kila mtanzania awe na uwezo wa kununua jezi hiyo iliyozinduliwa na Kampuni ya Sandaland.
Akizungumza na waandishi wa habari Makonda ameeleza kuwa jezi za timu ya taifa zimepanda bei tofauti na mwanzo ilhali mkataba wa jezi bado upo vilevile.
Aidha Makonda amewaasa wale wanaopewa Posho za jezi waendelee kula kama kawaida kwakuwa ni faida ya jezi zao za taifa.
#KemgongoUPDATES
MAHAKAMA IMEANZA TAR.24 SEPT.2026
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa?
Lissu: Nipo tayari, Mheshimiwa Jaji.
Jaji Ndunguru: Tuendelee.
Lissu: Nashukuru. Naomba kwanza nikumbushwe niliishia wapi.
Jaji Ndunguru: Ulisema unamaliza kwenye sheria, unaanza kuzungumzia ushahidi sasa. Unakumbuka?
Lissu: Waheshimiwa Majaji, nashukuru. Kabla sijaendelea na ushahidi, naomba nizungumzie kitu kimoja muhimu ambacho Mahakama hii ilipata kusema kwenye kesi ya Freeman Aikael Mbowe.
Kuto kufafanua "Essential Elements" kwenye Hati ya Mashitaka
Mahakama hii, katika kesi ya Freeman Aikael Mbowe, ilikuwa inajadili kushindwa kwa upande wa mashtaka ku-disclose mamlaka halali.
Mamlaka halali maana yake ni nini?
Mahakama hii ilisema katika ukurasa wa 53 wa hukumu:
<<"Statutes must give fair notice or warning to those subject to them.
They must guard against arbitrary and discriminatory enforcement and they must not reasonably ...">»
Sheria zinatakiwa kutoa tahadhari sahihi/muafaka kwa wale wanaotegemewa kuzifuata.
Ziwalinde watu dhidi ya mamlaka holela/matumizi holela ya madaraka yanayotumiwa na sheria.
Na sheria zisinyime watu uhuru wa kuzungumza. Isipolinda wote, tutakuwa wafungwa.
Mahakama ilisema yafuatayo kuhusu sheria za aina hii: <<<"Such statutes must be under the doctrine of overbreadth.">»
<<"If the statute is so overbroadly written that it could chill free speech, then it can be struck down because of its chilling effects.">»
Maana ya Overbreadth Doctrine ipo katika kamusi ya Black's Law, toleo la saba.
Kesi ya Freeman Aikael Mbowe ilimalizia kwa maneno haya ukurasa wa 58.
**"The failure to lay a name of lawful authority targeted by utterances prejudiced the first accused, upon which it can evaluate if the words in question were calculated to achieve the act or conduct said to be seditious.
The charge was defective.'
Kwa kifupi, Hati ya Mashitaka inayosema alichochea umma.
Wasafiri, wasio wasafiri, wageni, wenyeji, watoto wachanga - hao wote ni umma.
Huwezi kujitetea kwa hati ya namna hiyo.
Ndiyo maana Mahakama imesema haya maneno yafafanuliwe katika Hati ya Mashitaka.
Yasipofafanuliwa, hayo mashitaka ni batili.
Itaendelea.......
VIDEO:
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Aggrey Mwanri, amekemea vikali vitendo vya rushwa ndani ya chama, akisisitiza kuwa hakuna mwanachama au kiongozi atakayevumiliwa endapo atatumia fedha au njia nyingine zisizo halali katika kuwania nafasi za uongozi.
Mwanri ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wananchi na wanachama wa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya CCM Sanya Juu, Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.
Katika mkutano huo, Mwanri ameonya dhidi ya vitendo vya rushwa vinavyoweza kujitokeza kuelekea uchaguzi wa ndani wa CCM, akieleza kuwa chama hakitakubali mtu kutumia fedha au mbinu nyingine zisizo za kimaadili kujitengenezea mazingira ya ushindi.
Aidha, amesisitiza kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayeanza kuonyesha dalili za kutengeneza safu au makundi kwa lengo la kuathiri mchakato wa uchaguzi wa ndani wa chama.
Katika hatua nyingine, Mwanri amemuagiza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Ndugu Patrick Boiysafi, kuhakikisha anafanya vikao na viongozi na wanachama katika ngazi mbalimbali za chama ili kukemea kwa nguvu zote vitendo vya rushwa na mienendo inayoweza kuhatarisha uchaguzi wa ndani wa chama.
Kauli hiyo inaendana na msimamo wa CCM kuhusu mapambano dhidi ya rushwa katika uchaguzi wa ndani, ambapo nyaraka za chama zinaelekeza kuchukuliwa hatua dhidi ya wanaobainika kujihusisha na utoaji wa rushwa kwa mujibu wa kanuni za chama na sheria za nchi.
Msemo wa msanii wa Bongo Fleva DuduBaya unaotamba kwenye mitandao ya kijamii sasa umeanza kuingia katika mazingira ya shule, huku baadhi ya wanafunzi wakionekana kuutumia katika mawasiliano yao ya kila siku.
Kiongozi na Mbunge mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amemkosoa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, kwa kutangaza hadharani kuwa jezi mpya za Taifa Stars ni mbaya, akisema kauli hiyo inaonesha kuwa Waziri hafuatilii ipasavyo kazi zake za uwaziri na badala yake amefanya suala la jezi kuwa mjadala wa mitaani.
Zitto ameyasema hayo leo Alhamisi, Septemba 24, 2026, kupitia ukurasa wake wa Facebook, wakati akitoa msimamo wake kuhusu mvutano unaoendelea kati ya Wizara, TFF na kampuni ya Sandaland kuhusu jezi mpya za Taifa Stars.
Kauli hiyo imekuja siku moja kabla ya Taifa Stars kuingia uwanjani, huku Waziri Makonda leo akisisitiza kuwa timu hiyo ni mali ya nchi na kwamba suala la jezi linapaswa kupewa uzito.
Zitto amesema yeye binafsi amezungumza na Waziri Makonda kuhusu suala hilo na kumweleza kuwa mjadala huo hauna maana kwa wakati huu, akisema baadhi ya maelezo ya Waziri ni mazuri lakini yanapaswa kujadiliwa mezani kati ya Wizara, TFF na Sandaland badala ya kuendelezwa kwa kelele mitaani.
“Waziri kutangaza kuwa jezi mbaya inaonesha kuwa hakai wizarani na hafuatilii kazi zake za uwaziri. Jezi ambayo tayari Timu ya Taifa inavaa unatangazaje kuwa ni mbaya?” amesema Zitto, akiongeza kuwa wakati Taifa Stars ikiwa na mchezo unaofuata, mjadala unapaswa kuelekezwa zaidi kwenye maandalizi na ushindi wa timu kuliko kuhamishia nguvu kwenye suala la jezi.
Amesema Waziri kulalamika hadharani kuhusu jezi hizo ni dalili ya kushindwa uongozi, akisisitiza kuwa changamoto zinazohusu ubora wa jezi na masuala ya kibiashara zinaweza kutatuliwa kwa Wizara kukaa pamoja na Sandaland. Zitto pia amesema amezungumza na kampuni hiyo na kuishauri ikae na Wizara ili kutafuta suluhisho.
Kuhusu uwezekano wa kutumia kampuni kubwa kama Nike, Zitto amesema hilo halina tatizo iwapo taratibu za kibiashara zitafuatwa, akitoa mfano kwamba endapo Nike ingekuwa na nia ya kuuza jezi za Taifa Stars, ingeweza kununua haki za kibiashara kutoka Sandaland badala ya kuondoa mkataba wa kampuni hiyo ya Kitanzania.
Zitto amesema hatua hiyo ingeweza kumwezesha Mtanzania mwenye mkataba kuendelea kunufaika huku kampuni ya kimataifa kama Nike ikiingia kwenye biashara kwa utaratibu wa kisheria. Sandaland kwa upande wake imekuwa ikisisitiza kuwa ina mkataba halali na TFF wa kutengeneza na kusambaza jezi za Taifa Stars na tayari imetangaza nia ya kuchukua hatua za kisheria kuhusu kauli za Waziri.
Amesisitiza kuwa mkataba wa uzalishaji wa jezi unapaswa kuheshimiwa, huku suala la ubora likichukuliwa kama eneo la kuboresha kupitia mazungumzo, si sababu ya kuendeleza mvutano hadharani.
Zitto amemalizia kwa kuwataka Waziri Makonda na Sandaland kuacha mjadala huo wa hadharani na kukaa pamoja kutafuta jawabu, akimtaka Waziri “kuweka mawe mfukoni” na kuelekeza nguvu kwenye maandalizi ya Taifa Stars, huku Sandaland akiitaka kuachana na hatua za mahakamani na kutafuta suluhu kupitia mazungumzo.
Serikali ya Tanzania imelipa Dola za Marekani milioni 32 (sawa na takriban Shilingi bilioni 74 za Kitanzania) ili kuipatia nchi uhalali wa kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mwaka 2027.
Hatua hiyo imebainishwa leo, Septemba 24, 2026, na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya michezo na usimamizi wa nembo za taifa.
Waziri Makonda ameeleza kuwa mbali na kitita hicho cha Dola milioni 32 cha uenyeji, Serikali pia ipo katika mazungumzo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ili kulipa Dola za Marekani milioni 12 (takriban Shilingi bilioni 30) kwa ajili ya kupata haki za matangazo ya televisheni (broadcast rights) ya mashindano hayo.
Amefafanua kuwa fedha hizo si za ujenzi wa viwanja au miundombinu ya barabara, bali ni uwekezaji wa kimkakati wa kuitangaza Tanzania duniani, kukuza utalii, na kutengeneza fursa za ajira kwa vijana
"Tumelipa sisi taifa kuwa wenyeji wa AFCON milioni 32... Sawa na bilioni takriban 74. Hii ni pesa ya kuwa tu mwenyeji. Lakini pia tunazungumza na CAF tunatakiwa tulipe dola milioni 12 ya kupata haki za matangazo. Hizi fedha sio za kujenga uwanja, sio za kununua maji, sio za kufanya kujenga barabara. Kama nchi tumelipa ili tupate uhalali wa kuhosti haya mashindano. Namba mbili tupate uhalali wa kuitangaza taifa letu kupitia mashindano ili watakaokuja waje wakiona Tanzania ni sehemu sahihi ya kuwekeza, vijana wengi wapate ajira”, ameeleza Makonda.
Waziri Makonda amesisitiza kuwa kutokana na Serikali kuwekeza mabilioni hayo ya fedha, jezi ya Timu ya Taifa (Taifa Stars) ni vazi kuu linalotambulisha nchi na nembo inayopaswa kuongezewa thamani kubwa ya kimasoko badala ya kuchukuliwa kwa wepesi au kutangazwa bila uratibu rasmi.
Wakati akina Dotto Magari, Mwijaku na akina Mr Pimbi wakiwa Wana Pinga harakati za Dudu Baya kupinga Ush*ga, lakini makampuni yame endelea kumshika Mkono Dudu Baya Kwa Kumpa pesa na baadhi ya vitu.
Leo kampuni ya kuuza vitu vya ndani wame mpa ofa Dudu Baya ya kuchagua vitu ambavyo anahitaji kwenye maduka yao.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo amesema kuwa Dudu Baya anahitaji sapoti Kwa sababu vita anayo Pigana nayo siyo rahisi
Ikumbukwe pia Jana, kampuni nyingine ilimpa ofa kama hii hii na kumzawadia simu mpya l.
Super Star #ChrisBrown amefunguka kuchukia tasnia ya muziki na watu maarufu wenye upendo feki na kutothamini kipaji chake.
Kupitia insta story yake #ChrisBrown ameeleza mengi juu ya kazi yake hiyo ya muziki na tasnia kwa ujumla. 👇
"Mimi si rafiki yenu, si swahiba wenu, siwapendi, sitaki ridhaa yenu, upendo wenu wa kinafiki. Nachukia tasnia ya muziki na sitaki kushiriki upuuzi wenu"
"Kama hakuna faida kwa watoto wangu sikuhitaji, Hamtaweza tena kuwa karibu nami kiunyenyekevu, ajenda zenu na hisia zenu".
"Siwapendi hata mmoja wenu nyie watu maarufu. Mimi ni bora zaidi yenu bila ubishi mimi ni mfalme. Hakuna msanii hata mmoja duniani anayeweza kunifikia n mnajua hilo. Nimechoka kuwa mtu mwema nitakuwa yule muovu" ✍Chris Brown
Upi mtazamo wako juu ya hichi alichokiandika Chris Brown?
#EastAfricaTV #TogetherTunawakilisha ✍ @Shneida_Infos