#TajiriLaKihaya
TAARIFA YA KUOMBA MSAMAHA KWA WANAHARAKATI
Nimeona ni vyema nitumie nafasi hii kuwaomba radhi wanaharakati wote ambao kwa namna moja au nyingine niliwakwaza kwa kuwaita “WANAHARAKATI UCHWARA.”
Kwanza kabisa, naamini wote tulikuwa na lengo moja: Mwenyekiti Tundu Lissu awe huru na haki itendeke. Kilichotutofautisha haikuwa lengo, bali njia, mbinu na mitazamo yetu katika kulifikia lengo hilo.
Ni kweli tulitofautiana sana. Wengine tuliamini njia fulani ndiyo sahihi, wengine walikuwa na mtazamo tofauti. Lakini leo ninatambua kwamba kutofautiana kimtazamo hakupaswi kutufanya tudharauliane, tuwekeane majina au kupunguza thamani ya mchango wa mwenzetu.
Kiukweli, suala la hukumu ya kifo ni jambo zito, linalotisha na kuogopesha. Linaweza kumfanya mtu afikiri tofauti, achukue tahadhari au aone umuhimu wa kutumia mbinu nyingine. Hilo halipaswi kutafsiriwa moja kwa moja kama udhaifu, usaliti au kukosa uzalendo.
Nimejifunza kwamba si kila anayechagua njia tofauti na yako ni adui yako, na si kila anayekupinga anakutakia mabaya.
Leo, pamoja na tofauti zetu, tunapaswa kukumbuka kuwa mapambano ya haki ni safari ndefu inayohitaji mshikamano, uvumilivu na hekima.
Miaka minne tutavumilia, rufaa itaendelea, na kwa vyovyote itakavyokuwa, tutaendelea kusimamia kile tunachoamini mpaka haki ipatikane.
Tusikate tamaa. Hakuna marefu yasiyo na ncha. Usiku unaweza kuwa mrefu, lakini hauwezi kuzuia alfajiri kuchomoza.
Ninaamini pia kwamba historia haitakumbuka tu nani alikuwa sahihi kwenye mabishano yetu, bali itakumbuka namna tulivyosimama kutetea haki, utu na misingi ya demokrasia.
Kwa hiyo, kwa wanaharakati wote niliowakwaza kwa kauli yangu, naomba radhi kwa dhati. Haikuwa sahihi kutumia lugha iliyoweza kudharau juhudi na mchango wenu.
Tusiruhusu tofauti za mbinu zitugawanye kiasi cha kusahau sababu iliyotukutanisha.
Tunaweza kutofautiana bila kuchukiana, kukosoana bila kudhalilishana na kupingana bila kuwa maadui.
Haki ni kubwa kuliko ubinafsi wetu, na safari ya kuitafuta inahitaji kila mmoja wetu.
Na hii ndio maana Halisi ya
TAJIRI LA KIHAYA NI MMOJA TU✌️
“Kesi yako ya kuiba kwa kutumia silaha imefutwa kwa kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka, ila utahukumiwa kwa kosa dogo la “Uzurulaji”
Nadhani title ya 'Baba wa Taifa' iwe na ukomo (Iendane na generations), with all due respect.
Nyerere awe Baba wa Taifa kuanzia Uhuru hadi 1999.
2000 kuja huku mbele 'Baba wa Taifa' awe TAL (Anapigania uhuru wa vizazi vya sasa na vya baadae, singlehandedly).
Dogo katoka shule, kanikuta nimekaa nje hapa Kabla hata hajashusha begi wala kunisalimia swali lake la kwanza likawa, "Kaka, vipi TAL ameshinda kesi?"
Nimemjibu amehukumiwa miaka 4 jela. Amehuzunika sana, mpaka sasa amekataa kula, anasema hana njaa. 💔