Uadilifu na kujiheshimu ni tunu kubwa sana! Pale mtu mzima unapojitoa ufahamu, ukakosa haya hata kuuza utu wako kwa vipande thelathini vya fedha kama Yuda Iskariote, unakuwa umejidhalilisha na kupoteza hadhi yako. Je, kweli unapata usingizi wa amani?
@MsigwaGerson Wakati mwingine kunyamaza kunasaidia kuponya kuliko ili mnalo Fanya,Mungu wa mbinguni awape hekima mjue wapi pa kusema na wapi pa kunyamaza
Nchi hii tunao wasomi wengi sana wenye nafasi kubwa tu za maamuzi kwenye masuala muhimu lakini wamekutana na mfumo wa “kula kwa urefu wa kamba”. Mtu mwerevu mwenye njaa anapokutana na kundi la wajinga wenye shibe atajiona fala tu. Mabadiliko ya kweli huletwa na MIFUMO yenye tija.
@godbless_lema Napenda sana kwenda na Mwanangu Bagamoyo huwa namuonesha yale majumba ya kifahari ya wakati ule ambayo sasa ni magofu na makazi ya Popo.
Huwa nawasii utu, ubinadamu, wema huwa havizeeki wala kupitwa na wakati.
Kama jamii,We need to redefine "Success" Tafsiri inayouzwa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii ni hatari kwa Taifa. Haijalishi umeua,umeteka,umedhulumu, umeuza utu au umehujumu rasilimali za umma,mradi tu una hela unakua mwamba.
Huu si ushindi, ni kuporomoka kwa maadili.
@madeinmusoma Miaka ya 1990s ni madhehebu Yale tu ya kipentekoste yaliamini unaweza kuokoka ukiwa duniani,mengine yaliamini kuokoka ni baada ya kutoka duniani(kufa).
Na ndio maana mwl mwakasege KKKT mwanzo hawakumuelewa.