Kwa makosa ya ukweli. Yule Mwaipopo aliyeunda kundi la kijeshi kinyume cha katiba na sheria hatujaona hatua yeyote dhidi yake! Yupo juu ya sheria? Kwanini hajakamatwa? Ndugu Rais @SuluhuSamia iponye nchi yetu. Turudishe 2021-2023. Hatua ya kwanza ni Tundu Lissu kuwa huru
NIMEULIZWA HIVI:
“Madeleka, kama Tanzania INAHESHIMU HAKI ZA BINADAMU, mbona watu WANATEKWA, KUTESWA, KUULIWA na KUPOTEZWA?”.
NIMEJIBU HIVI:👇
“Inategemea na TAFSIRI. Labda hiyo ndiyo HAKI MPYA YA BINADAMU Tanzania”.
Sawa kwa CHADEMA nachanga hakuna shida mkubwa Ila Kwakuwa namba Yako ya Mpesa ninayo , nayo naweka kakitu ! Unafanya kazi kubwa ! Sitaiweka hadharani bila Ruhusa Yako
Keep it up @HecheJohn
NDUGU ZANGU TUWACHANGIE CHADEMA NEEDS 300M
Kuelekea Baraza kuu la kihistoria..
Nimesikia sauti yenu, Asanteni sana Watanzania kwa upendo mkubwa.
Ushindi wetu uko karibu sana..
Msiogope, tutashinda.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godless Lema amesema suala la uchawa limekuwa utamaduni wa Watanzania ambao unaua ukweli na kuliangamiza taifa.
Lema ameeleza hayo leo Julai 11, 2026 katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, ambapo ameeleza zaidi kwamba hakuna taifa linaloweza kujengwa kwa sifa za kupangwa na kuabudiwa kwa viongozi.
Katika ukurasa wake Lema ameandika "Kama kuna utamaduni hatari unaokita mizizi Tanzania leo basi ni uchawa, ni janga kubwa kuliko saratani kwa ustawi wa taifa, unaua ukweli, unahalalisha uongo, unazika uwajibikaji na kuwafanya wanaosema ukweli waonekane maadui. Hakuna taifa linaloweza kujengwa kwa sifa za kupangwa na kuabudiwa kwa viongozi. Taifa hujengwa kwa ukweli, uwajibikaji na ujasiri wa kukosoa pale panapokuwa na makosa. Uchawa si maendeleo, ni adui wa maendeleo na kikwazo cha haki".
Mchungaji Peter Simon Msigwa amesema dalili za taifa kuanza kuyumba hazianzi kwa kuanguka kwa ghafla, bali hujitokeza pale taasisi zake muhimu zinapoanza kupoteza uwezo wa kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba na sheria.
Amesema hali hiyo husababisha sheria kubaki kwenye maandishi huku zikikosa nguvu ya kutawala, na taasisi kama Bunge, Mahakama na Jeshi la Polisi kupungua uwezo wa kusimamia haki na uwajibikaji.
Katika makala yake yenye kichwa "Kabla Taifa Halijaanguka", Msigwa amesema hatari kubwa si kuwepo kwa taasisi kwa jina, bali kupoteza kusudi la kuanzishwa kwake, akitolea mfano wa mawazo ya mwanafalsafa wa Kifaransa Montesquieu, aliyeeleza kuwa uhuru wa wananchi hulindwa pale mamlaka yanapowekewa mipaka kupitia taasisi huru zinazoweza kuwajibisha kila mmoja bila upendeleo.
Msigwa amesema historia inaonesha kuwa mataifa mengi yaliyoanguka hayakuanguka kwa ghafla, bali baada ya wananchi kuanza kuzoea vitendo visivyo vya kawaida kama dhuluma, rushwa, ukimya mbele ya uovu na kukandamizwa kwa haki. Amesema hali hiyo hujenga mazingira ya kukusanya madaraka sehemu moja na kudhoofisha misingi ya demokrasia.
Akitolea mifano ya Afrika, Msigwa ametaja Ghana, Zambia na Malawi kuwa mataifa yaliyoonesha umuhimu wa taasisi imara katika kulinda utawala wa sheria na kuhakikisha mabadiliko ya uongozi yanafanyika kwa njia za kikatiba na uchaguzi wa amani, licha ya changamoto zinazoweza kujitokeza.
Aidha, amesisitiza kuwa wananchi wana wajibu wa kushiriki katika uchaguzi, kufuatilia utendaji wa viongozi, kukataa rushwa, kuuliza maswali kwa amani na kutetea haki za wengine bila kujali tofauti za kisiasa. Amesema demokrasia haijengwi siku ya uchaguzi pekee, bali kupitia ushiriki na uwajibikaji wa kila siku.
Msigwa pia ametoa wito kwa viongozi wa dini, waandishi wa habari, wanasheria, wasomi na viongozi wa umma kutekeleza wajibu wao kwa uadilifu ili kulinda misingi ya taifa, akisema uzalendo wa kweli unapimwa kwa kulinda Katiba, utawala wa sheria, taasisi huru na haki za wananchi, akihitimisha kwa kusisitiza kuwa historia itawahukumu wananchi kwa namna walivyolinda misingi ya taifa pale ilipoanza kuyumba.
Kweli, sikio la kufa halisikii dawa! Dunia nzima inakunyooshea kidole, lakini wewe umeukaza shingo na kuziba masikio. Unadhani madaraka ni ya milele? La hasha. Madaraka ni ya muda tuu (transitory power) yanapita. Lakini haki haifi, wala haizikwi. Siku yake ikifika, haki yetu tutaipata, bila shaka! A luta continua! ✊🏾