Leo Balozi @JSimbachawene amemtembelea na Mhe. @kipmurkomen Waziri wa Uchukuzi wa Kenya katika ofisi yake kwa mazungumzo. Wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uchukuzi ili kuongeza biashara na kutatua changamoto zinazojitokeza na mpango wa kubadilishana uzoefu
Nilipata fursa ya kukutana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. John Simbachawene kwenye makao makuu ya wizara ya barabara na uchukuzi hapa Nairobi asubuhi hii.
Mazungumzo yetu yaliangazia maswala kadhaa wa kadhaa yakiwemo uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi zetu mbili, uchumi na biashara, uwekezaji, na miundombinu kwenye sekta ya uchukuzi.
Niliipongeza Tanzania kwa kuboresha uchukuzi kupitia usafiri wa BRT ambao Kenya pia inapanga kutekeleza kama njia mojawapo ya kudhibiti msongamano wa magari, kuimarisha usafiri na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Vile vile, nilimshukuru H.E. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na watanzania kwa jumla kwa kuwa marafiki wa dhati wa Kenya na wakenya.
Lengo letu kama Afrika Mashariki ni kuendeleza uhusiana mwema, kuboresha biashara kati ya nchi zetu, na kuweka mikakati itakayowezesha usafiri wa haraka na rahisi kutoka nchi moja hadi nyengine.
Ubalozi umewezesha mazungumzo kati ya Mhe @AngelineMabula na Bi. Maimunah Sharrif, Mkurugenzi Mtendaji wa @UNHABITAT, wamejadili kuhusu programu za kuendeleza makazi nchini Tanzania na wamesaini MoU ili kuwa ofisi za @UNHABITAT Tanzania na kupanua wigo wa miradi yake nchini kwetu
Balozi @JSimbachawene amepokea ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Makazi #UNHA2 unaofanyika Nairobi tarehe 5-9 Juni. Ujumbe umeongozwa na Mhe. Dkt. Angeline Mabula, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi @wizara_ya_ardhi@mfa_tanzania
Balozi @JSimbachawene na mwakilishi wa Tanzania katika UNEP ameongoza ujumbe Tanzania ktk mkutano wa pili wa majadiliano ya kuandaa mkataba wa kimataifa wa kukabiliana na taka za plastiki. Pamoja naye ni wataalam wa NEMC, Ofisi ya Makamu wa Rais, TBS na Mkemia Mkuu wa Serikali
Leo tarehe 5.5.2023 Balozi wa Tanzania nchini Seychelle mwenye makazi Nairobi Dkt John Simbachawene amekutana na Waziri wa Afya wa Seychelles, Mhe Peggy Vidot na kufanya naye mazungumzo yaliyolenga kuboresha mahusiano kati Tanzania na Seychelles kwenye sekta ya Afya
Mhe. Balozi @JSimbachawene akisalimiana na baadhi ya Diaspora wa Tanzania waliopo Kenya katika maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano, Diaspora hao ni pamoja na wafanyabiashara, wanafunzi, wafanyakazi wa UN, wafanyakazi wa sekta binafsi na Jumuiya ya Wanawake wa Tanzania Kenya ULWA
Ubalozi umepokea ujumbe wa Maafisa kutoka Chuo cha Ulinzi Tanzania (NDC) waliopo kwenye ziara ya kimafunzo nchini Kenya inayoitwa "Immediate Strategic Neighbourhood Field Practical Training". Maafisa hao wanatoka kwenye nchi mbalimbali wakiongozwa na Brig. Jen. BT Rutambuka
Balozi @JSimbachawene alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Madini, Blue Economy na Maritime wa Kenya, Mhe Salim Mvurya katika ofisi ya Wizara,Nairobi. Viongozi hao walijadiliana kuhusu kuboresha mahusiano katika maeneo ya madini na maritime kati ya Tanzania na Kenya.
Balozi Simbachawene pamoja na Konseli Mkuu wa Tanzania aliyepo Mombasa, Mhe. Athuman Haji wamefanya mazungumzo na Bw. Andrew Sisau wa @PMAESAHQ na kuwakaribisha kuwekeza kwenye meli za kitalii - cruise ship kwa ajili ya utalii katika fukwe za Tanzania na Afrika Mashariki
Balozi Dkt John Simbachawene amekutana na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma ambaye yupo nchini Kenya akihudhuria Mkutano 3rd Symposium on Greening Judiciaries in Africa unaofanyika Nairobi, tarehe 3 - 5 Aprili. Majaji kutoka nchi 25 za Afrika wameshiriki mkutano huo.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya na Sudan kusini Balozi John Simbachawene kushoto akimpongeza Bw. Benson Meikoki,Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda cha madawa cha Kairuki Health and Organization Nertwork (KHEN) mara baada ya kuwasilisha mada Katika kongamano la msafara wa kibiashara wa Tanzania uliotembelea nchini Sudan Kusini Katika jiji la Juba ili kuangalia fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji Katika sekta ya Kilimo afya na Elimu.
This morning Amb Dr John Simbachawene led a delegation from @UdsmOfficial including Prof. Rutinwa & Prof Mbamba to visit Juba University and met with the Deputy Vice Chancellor Prof. Robert. Discussions were centred on how @UdsmOfficial & Univ. of Juba can enhance cooperation
Air Tanzania Head of Marketing, Ms. Christina Tungaraza in South Sudan participating in Tanzania South Sudan Business forum organized by Tantrade under the supervision of H.E Dr. John Stephen Simbachawene Ambassador of Kenya & South Sudan.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya ambaye pia anawakilisha nchini Sudani Kusini ameshiriki Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Sudani Kusini lililofanyika tarehe 22-23 Machi 2023 Jijini Juba, Sudani Kusini
Kongamano la Kwanza la Kibishara kati ya Tanzania na Sudani Kusini linaendelea hivi leo katika jiji la Juba. Kongamano limefunguliwa na Mhe. Agog Makur, Naibu Waziri wa Fedha wa Sudani Kusini na kuhudhuriwa na washiriki wapatao 120 kutoka nchi zote mbili