Hii ni kauli muhimu sana, imethibitisha yale ambayo tumeyasema kwa miaka yote.
Leo kiongozi wa juu wa ccm ametibitishia Watanzania na Dunia kwamba . Kwa wale waliokua wanafikiri tunasema uongo au tunawazushia.. polisi, usalama wa Taifa na jeshi la wananchi wamsikilize bwana Chacha.
Vyombo vya ulinzi na usalama ni mali ya ccm na hao viongozi wa vyombo hivyo ni wanachama na makada wa ccm.
Maswali muhimu ya kujiuliza, je vyombo vya ccm, polisi, usalama wa Taifa na JWTZ kama alivyosema bwana Chacha vinaweza kutendea haki wapinzani wa ccm?
Je ni halali kwa Watanzania mamilioni kulipa kodi ambazo zinatumika kuhudumia vyombo vya dola ambavyo ni vya ccm?
Chama chetu kitasema kwa undani kuhusu jambo hili na kutoa msimamo kamili, kwasasa tuelewe.
1. No reforms no Election ilikua muhimu sana ili kubadili hali ya vyombo hivi kuwa mali ya chama kimoja katika Nchi ya vyama vingi..
2. Kesi ya Mwenyekiti wetu ni ya uongo amebambikiziwa na vyombo vya ccm kwasababu ya kulinda chama chao dhidi ya ushindani wa kweli kutoka kwake na chama anachokiongoza.
3. Katika mazingira haya aliyoyasema Chacha haitawezekana kwa Mwenyekiti wetu kutendewa haki, kwasababu hivi vyombo vya ccm haviwezi kumtendea haki mwanachadema..
4.Tuhuma za kuua watu, kuteka, kupoteza zinazofanywa na vyombo vya dola ni kwaajili ya kuisaidia ccm kujitangaza washindi kwa njia ambazo sio halali.
5. Wanachama wa ccm hawafiki hata milioni 5 Nchi hii. Watanzania wako milioni 60, kwanini vyombo vya watu milioni tano vilipwe na kuhudumiwa na Watanzania wote kwa maslahi ya watu million 5.
Lazima tupate katiba mpya sasa.
Hitimisho la @TunduALissu mbele ya Mahakama:
“Mimi kwa hakika najua maslahi yangu ni yapi: kutetea ukweli ninaoujua kwa ujasiri na bila hofu… Kifo kinatutabasamia sote; yote ambayo mwanadamu anaweza kufanya ni kukitabasamia pia.”
“History will absolve me”.
Leo tarehe 26 Julai 2026 mimi PETER MADELEKA natangaza rasmi KUACHANA NA SIASA ZA ACT WAZALENDO.Nafanya hivyo ili nipate MUDA WA KUTOSHA kuungana na WAPENDA HAKI wote katika KUPIGANIA HAKI na USTAWI wa nchi yetu.Tanzania yenye HAKI Inawezekana kama kila mtu ATATIMIZA WAJIBU WAKE.
Watanzania walitaka namba ya MAKAMU HECHE ili wamtumie PESA kama kumuunga mkono kipindi hiki kigumu.
MAKAMU HECHE kaamua kuomba watanzania wachangie CHAMA-Chama kina jukumu zito ndani ya huu mwezi mmoja kuitisha BARAZA KUU LA CHAMA.
Baraza kuu la CHAMA linakuja kufanya maamuzi MAZITO juu ya haya mambo mawili.
1. KATIBA MPYA.
2. FREE TUNDU LISSU.
Jumla MILIONI 330 inatakiwa-Kufanikisha hili BARAZA KUU. Weka mchango wako kwenye account rasmi za CHAMA.
Voda (MPESA): 0744446969
JINA: CHADEMA HQ.
Repost 500
Tumeenda Mbali Na Nyumbani Kupamba Ili Nyumbani Irudi Pesa Ama Iirudi Maiti, Ukiona Huna Cha Kutusaidia Basi Usitufanyie Fitna.
Good Morning My Beautiful Friends