Wanalimwengu wanaweza kukukatia tamaa.
Wanaweza kukusema vibaya, na kukudharau.
Lakini kamwe, USIJIKATIE TAMAA. JINENEE MEMA, JIPENDE, JIKUBALI.
kuwa rafiki wa maisha yako.
Maana, aonavyo mtu nafsini mwake NDIVYO ALIVYO.
Unavyovichukulia poa ni ndoto kwa wengine:
Unachukulia poa afya uliyonayo
Unachukulia poa kazi au kibarua ulichonacho.
Unaona kawaida kuwa na mume/ mke uliyenae.
Unachukulia poa mzazi/wazazi ulionao.
Shukuru, wafuraihe angali wakiwa hai bila kujali madhaifu yao.
Sahau kitu kinaitwa 'starehe ni zangu.'
Figo zikipata shida kwa ulevi familia yako itaweka vitu rehani/kupitisha bakuli kukutibu.
Ukiwa hoi taabani, jamii italazimika kuitunza familia au watoto wako.
Utawapa watu mzigo wa kukuombea
Kwaufupi maisha yetu yanaathiri wengine.
Hasira ilimfanya mtu akampiga boss wake.
Hasira ilimsababishia mtu ulemavu.
Hasira ilimkosesha mtu mke/mume sahihi.
Hasira ilimfukuza mbeba hatma wa mtu.
Nimejifunza hasira hii haitoki kwa Bwana.
Usiringie uzuri wa sura au umbo,
Usiringie Pesa,
Usijivunie gari au nyumba nzuri,
Wala usijivunie mke au mume mzuri,
Maana hivi vyote huaribika, ni suala la muda tu.
Ringia kuwa na mtoa vyote, Yesu.
Kitu nimechelewa kujua ni kuwa, kuna changamoto hazihitaji pesa kutatulika.
Mfano, mtu aliyekosana na Mungu mambo yake yakaharibika, Pesa haiwezi msaidia.
Ni toba na kurudisha mahusiano na Mungu.
Uwe mwanaume mwenye kukabili talaka, kupoteza kazi au biashara
Kushughulikia madeni, na bado ukasema, 'nitaweka kila kitu sawa.'
Mwanaume wa kweli hatafuti huruma. Never
Ngono haitakuridhisha.
Umaarufu hautakuridhisha.
Dawa za kulevya hazitakuridhisha.
Pesa haitakuridhisha.
Pombe haitakuridhisha.
Mafanikio hayatakuridhisha.
Bro, maisha ni tupu bila Mungu.
Ni yeye pekee anayeweza kukuridhisha.