#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 433
Jaji Ndunguru anawasha kipaza sauti anasema tumesikia hoja za mshtakiwa na Mahakama inatamka kwamba shauri kwa upande wa utetezi limefikia mwisho.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji kwa vile sasa kesi ya pande zote mbili imefungwa tunaomba Mahakama itupangie siku ya kuja kuwasilisha hoja za mwisho.
Sijawasiliana na upande wa mashtaka naomba nipendekeze tarehe yangu ya kuwasilisha hoja za mwisho.
Waheshimiwa Majaji natambua kwamba shauri limepangwa kuisha tarehe 25 September 2026 na mwenendo wa kesi una kurasa zaidi ya 1000, itakuwa kazi kubwa sana lakini naomba mimi kuanzia Jumatano ya tarehe 23 Septemba 2026 nitakuwa tayari kwa ajili ya kufanya final submission.
Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka mnasemaje?
Katuga: Tunaungana na mshtakiwa ila hajasema tufanye kwa maandishi au kwa mdomo.
Kwa tarehe aliyoipendekeza sisi tutajitoa Jumatano hiyo hiyo na sisi tutakuwa tayari kufanya final submission. Waheshimiwa majaji ingawa upande wa utetezi umefunga kesi ila tulikuwa na hamu sana ya kufanya cross kwa mashahidi wa Lissu waliokuwa wamebakia
Watu wanacheka sana, wanamuona Katuga kama kitukoππππ
Jaji Ndunguru: Hiyo amri mbona mahakama bado haijaitoa?
Tunakubaliana kuwa siku ya Jumatano shauri litakuja kwa ajili ya mawasilisho ya mwisho saa tatu kamili asbuhi
Imepigwa High Coooouuuuurrrrtttttt
Majaji wanatoka,
Mhe. Lissu anaangana na Mawakili wake pamoja na Viongozi wa Chama pamoja na watu mbalimbali waliojitokeza Mahakamani.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 18, 2026
Last time tuliishia part 431 so leo tunaendelea na -;
Part 432.
Mhe. Tundu Lissu ameingia Mahakamani watu wana vibe sana wanaimba Mwamba Mwamba huku wakipiga makofi mengi sana.
Majaji wote watatu wameingia na kuketi kwenye viti vyao.
Wakili wa Serikali Ajuaye amesimama na kutambulisha jopo lake na kuwa wako tayari kuendelea.
Mhe. Lissu na yeye anasema niko tayari kuendelea.
Mhe. Lissu amesimama na kusema kwamba nimekutana na Kamishna wa Polisi Ramadhani Kingai ambaye nilikuwa nimependekeza awe shahidi wangu wa leo, nimekutana nae Mahakamani kwenye chumba hiki hiki waheshimiwa majaji, naweza kuthibitisha kwamba ameheshimu wito wa Mahakama amekuja na nimezungumza nae kuhusu yeye kuwa shahidi wa upande wa utetezi na nimezungumza nae kiasi cha kutosha, baada ya kumueleza maeneo ambayo ningependa ayatolee ushahidi ameniambia kwamba yeye hawezi na hayuko tayari kutoa ushahidi kwa upande wangu kwa maneno yake mwenyewe amesema
βYeye yuko upande wa wale wanaoomba na watakaoshangilia nikipatikana na hatiaβ
Kwahiyo amesema hayupo tayari kuja kutoa ushahidi kwa niaba yangu.
Nimemuelewa Waheshimiwa Majaji kama hayuko tayari siwezi kumlazimisha kutoa ushahidi ambao hataki kuutoa.
Waheshimiwa Majaji Kingai ameniambia kitu kingine kuhusiana na mashahidi wengine wawili IGP Camillius Wambura na CDF Jacob Mkunda, amesema vilevile hata wao watakaporejea nchini na kupata wito wa Mahakama msimamo wao utakuwa ni huo huo kwamba na wao hawatakuwa tayari kutoa ushahidi kwa upande wa utetezi kwasababu ile ile kuwa wako upande wa wale wanaoombea na watakaoshangilia nikipatikana na hatia.
Katika Mazingira haya waheshimiwa majaji maana yake ni kwamba sina mashahidi zaidi kwahiyo naomba kufunga ushahidi kwa upande wa utetezi.
Ni hayo tu waheshimiwa majaji.
Naomba Repost yako.
@godbless_lema Tuko ngarenaro hapa ngoja tuone, pia kumbuka Arusha ndio tuliokupa jina na heshma iyo uliyonayo Tena kwa jasho na damu bro na pia ukumbuke Kuna watu wanaishi na ulemavu na vipande vya mabomu kwaajili ya harakati zako,sasa tunaomba usituumize Braza.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 428
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Re- examination, Makam Mwenyekiti Bara John Heche.
Mhe. Lissu: Ulionyeshwa video ukaulizwa kama ni wewe na kama hayo maneno yanaelekea kuwa ni ya kwako na ukasema hukumbuki kutoa hotuba ya aina hiyo.
Heche: Sikumbuki kutoa hotuba hiyo, wametumia akili mnemba kuitengeneza.
Mhe. Lissu: Fafanua Akili Mnemba
Watu kichekoππππ
Heche: Akili Mnemba ndio Artificial Intelligence (AI)
Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu magari manne ya bei mbaya ukasema una magari mawili, fafanua.
Heche: Nilimaanisha nina Prado na Hilux ambazo ndo huwa nazitumia, hiki ndo nilichomaanisha.
Mhe. Lissu: Unakumbuka kuhusu kukamatwa kwako nje ya Mahakama na kuwa unapelekwa Tarime, Uliulizwa ulienda Kenya? Ukasema nilizuliwa, fafanua.
Heche: Nilizuiliwa na immigration kwenye mpaka wa Sirari.
Mhe. Lissu: Unakumbuka uliulizwa na mawakili wa Serikali kuhusu wewe kukutana nao Oysterbay Police na walisema kwamba 70% ya waliokamatwa walikutaja wewe kuwa unahusika na kuratibu wewe hizo vurugu, ukasema hujui , fafanua.
Heche: Nilikuwa ndani tangu tarehe 22 Oktoba 2025 kwa vyovyote vile siwezi kuhusika na yaliyotokea Oktoba 29, 2025.
Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu matibabu yangu hasa kuhusu matibabu nje ya nchi, ulijibu kwamba wakili wa Serikali alikuwa sahihi nusu na sio sahihi nusu, Fafanua
Heche: Kuna mazingira ambayo Mbunge anaweza asifuate utaratibu wa kawaida, mfano mazingira kama ya dharula.
Mhe. Lissu: Uliulizwa ni lazima Mbunge mpaka apate referral kwenda nje ya nchi? Ukasema sio lazima apate refferal
Heche: Mbunge akiwa mahututi sio lazima apewe referral
Wakili wa Serikali: Waheshimiwa Majaji muda umeisha hivi sasa ni saa kumi na moja tunaomba ahirisho hadi kesho saa tatu kamili asubuhi.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji huyu John Heche ndio shahidi wangu wa mwisho kwa ambao ni raia, Kwahiyo kesho tutamaliza sio zaidi ya lisaa kwahiyo naomba kesho mashahidi wengine kesho waje ili niongee nao kujua namna tunavyoenda na ushahidi uliobaki.
Watu kichekoππππππ
Jaji Ndunguru: Shauri linaahirishwa hadi kesho saa tatu kamili asubuhi, shahidi bado hujamaliza kutoa ushahidi wako.
Imepigwa High Cooooouuuuuurrrrrtttt
Majaji wanatoka
Tukutane kesho saa tatu kamili asubuhiβοΈ
Naomba Repost yako.
@MtataProMax Siku mkianza kumsofia Heche ndio tutajua mmeshamaliza biashara kwa sasa bado ndio maana anawayesa sana.pia anagalizo:siku Heche na lissu wakikubaliana na ccm mjue chawa ajira kwishnei
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 419
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche.
Katuga: Waambie Majaji kuwa wewe ulitangazwa katika uchaguzi usio huru na haki lakini haukuukataa.
Heche: Sahihi
Katuga: Ni sheria gani ya uchaguzi au yoyote ya nchi inayokulazimisha wewe ukitangazwa kwenye uchaguzi usiokuwa huru inakulazimisha usiukatae?
Heche: Ni wananchi, sheria siijui
Katuga: Wewe binafsi ukitangazwa kuwa mshindi, uchaguzi unakuwa sio wa haki?
Heche: Sio kweli
Katuga: Kwahiyo uliingia Bungeni kupitia uchaguzi usio huru na haki?
Heche: Sahihi kabisa
Katuga: Ukaserebuka
Heche: Kuna kuserebuka Bungeni?
Watu kichekoππππ
Katuga: Nilikusikia ulisema kuwa kuna Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi baadae akaenda kugombea jimbo la Butiama ?
Heche: Sahihi
Katuga: Hakuna mtu aliyewahi kufanya kazi Serikalini na baadae akajiunga na chadema?
Heche: Wapo
Katuga: Mtu yeyote aliyekuwa mtumishi wa umma, mfanyakazi wa Serikali nikisema kuwa atakuwa na haki ya kujiunga na Chadema?
Heche: Mtu akiwa mtumishi wa Umma halafu akajiunga na Chadema watamfukuza, ila akimaliza sawa
Katuga: Ni sahihi mtumishi wa umma akistaafu anahaki ya kujiunga na chama chochote?
Heche: Sahihi
Katuga: Ni sheria gani huyo mgombea wa Butiama aliyovunja yeye kujiunga na kugombea CCM?
Heche: Kwa utaratibu wa CCM huwezi kugombea kama hujawa mwanachama kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita kwahiyo alijiunga CCM akiwa Mkurugenzi wa Tume
Katuga: Ni sahihi kuwa msimamo wa Chadema ulimaanisha bila mabadiliko uchaguzi usogezwe mbele?
Heche: Ni sahihi
Katuga: Ulieleza sheria gani inaruhusu uchaguzi kusogezwa mbele?
Heche: Sikueleza
Katuga: Ni sahihi kuwa wewe Lissu na Lema mlienda Kenya kumuona Raila Odinga?
Heche: Ni sahihi
Katuga: Huko Nairobi mlimwambia Raila kuwa mnaenda kuzuia uchaguzi? Tunaenda kukinukisha?
Heche: Tulimueleza matatizo yote ya uchaguzi wa Tanzania
Katuga: Nina wasiwasi kama kweli ulipata division one
Heche: Una haki ya kuwa. pia punguza hasira na wasiwasi japo na mimi nina wasiwasi sana na Degree yako ya Mzumbe
Jaji Ndunguru: naomba twendelee tukimaliza hapa mtaenda kulumbana huko nje
Watu:πππππ
Heche: Waheshimiwa majaji tulizungumza mambo yaleyale ingawa hatukutumia exactly words.
Katuga: Taarifa zinazotolewa na Brenda ni wewe unamuelekeza atoe?
Heche: Ofisi ya Katibu Mkuu
Katuga: Uliulizwa na mshtakiwa kwamba yeye anashtakiwa kwa kuandaa mkutano na kutamka aliyoyatamka, wewe ukasema sio kweli
Heche: Sahihi
Katuga: Kabla hujaja kutoa ushahidi ulisoma hati ya mashtaka?
Heche: Niliisoma
Katuga: Waambie majaji kuna sehem imeandikwa Lissu anashtakiwa kwa kuandaa mkutano?
Heche: Nipe hati ya mashtaka niisome ila nakumbuka ameshtakiwa kwa mambo yaliyotokea kwenye mkutano
Katuga: Jibu swali
Heche: Sijui
Katuga: Ni ushahidi wako ulisema kuwa tuhuma za kualika waandishi wa habari sio sahihi na Sekretarieti ndio ilialika?
Heche: Sahihi
Katuga: Waambie majaji mshtakiwa anashtakiwa kwa kualika waandishi wa habari?
Heche: Sijui
Katuga: Waambie majaji kama Mwenyekiti Lissu alitaka au hakutaka hotuba yake ya 3/4/2025 alitaka iwafikie umma
Heche: Siwezi kujua kama alitaka
Katuga: Ni kweli au sio kweli kuwa 3/4/2025 kuna mambo ya ndani yalifanyika huku waandishi wa habari wakiwa wametolewa?
Heche: Sikumbuki
Katuga: Na ulikuwepo kwenye mkutano?
Heche: Mwanzo mwisho
Katuga: Mr Sikumbuki
Heche: Unataka nijibu majibu yako unayoyataka wewe, huku anacheka.ππ
Katuga: Waambie majaji Lissu alikuwa na uwezo wa kukataa au hakuwa na uwezo wa kukataa kuongea na waandishi?
Heche: Sijui
Katuga: Lissu alikuwa na uwezo wa kukataa au kukubali kuongea na waandishi wa habari?
Heche: Secretariat haina uwezo wa kumlazimisha Mwenyekiti.
Katuga: Unafahamu au hufahamu kama kulikuwa na hotuba rasmi iliyokuwa imeandaliwa?
Heche: Aliyoandaa yeye au?
Part 420 Inaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.