Tusome kwa makini:
👇🏾👇🏾
Tanzanian billionaire Rostam Aziz's takeover of the country's top gas field is blocked by regulator
Tanzania's competition watchdog has blocked Taifa Gas, controlled by tycoon Rostam Aziz, from buying the operator of the country's biggest producing gas field.
Tanzania’s competition regulator has blocked a deal that would have given Tanzanian tycoon Rostam Aziz a large stake in the company that runs the Songo Songo gas field, which produces about half of the country’s natural gas.
The Fair Competition Commission issued a notice on Oct. 5 prohibiting the merger application filed for the transaction, Orca Energy Group Inc., the field’s Canadian-listed operator, said in a statement late on Oct. 9. The commission gave no reasons.
https://t.co/AsSmGi9ujX
Video hii imeniachia mafunzo makubwa matatu. Kwanza, namna nguruwe walivyodanganyika kwa kujikuta wameingia wenyewe, kwa hiyari yao wenyewe, kwenye ‘mfumo.’ Mwanzoni nguruwe waliingia wenyewe kwenye mtego wakila chakula kile kile na kuondoka bila wasiwasi—maana hapakuwa na madhara ya moja kwa moja. Kwa hivyo ilionekana kama mle ndani ya mtego palikuwa na fursa na kwa vile mazingira hayakuwa yanabadilika wala kutisha, nguruwe wakahisi ‘wamejipata’ na ikawa rahisi kwao kujenga mazoea.
Jambo la pili, ni namna mtegaji alivyokuwa hana haraka na matokeo. Unaweza kuona hakutumia nguvu wala mabavu mwanzoni na alilenga zaidi faida ya muda mrefu. Nguruwe, kwa upande wao, walifaidi chakula walichokihitaji, wakala wakashiba, halafu wakaondoka zao bila madhara yoyote. Akili za hawa nguruwe ziliamini mazingira yale ya hatari yalikuwa salama kwa vile hawakupoteza uwezo wa kuingia na kutoka. Fursa inayopatikana kwa muda mfupi na papo kwa papo iliwafumba macho wasikumbuke hatari kubwa iliyojificha.
Kinachoumiza zaidi hapa ni namna akili za nguruwe zilivyorudi ghafla lakini kwa kuchelewa na tayari wakawa hawana cha kufanya tena. Kufumba na kufumbua uhuru wa kuingia na kutoka ulipotea na hapo ndipo nguruwe walipogundua kumbe hawapo salama tena. Ule mlango ulipofungwa kuwazuia kutoka chakula kilibaki pale pale, lakini kilichowastua na kuanza kuleta taharuki ni kupoteza uwezo wa kuondoka. Nguruwe hawakuona tena thamani ya chakula kilichokuwepo mule ndani bali tukio la kupoteza uhuru wao ndio lililowasanua.
Tuna mengi ya kujifunza hapa kuhusu binadamu. Kitu gani hasa huwa kinatuingiza kwenye mapenzi, kwa mfano, na chanzo kikubwa cha migogoro ya mahusiano? Mfumo wa biashara nyingi zinazoendeshwa katika enzi hizi za ubepari na namna gani walaji tunageuzwa kuwa ‘fursa’ zinazokuja kutunasa kwenye uraibu? Umewaza siasa? Umewaza dini? Unafanywa ujisikie salama kwanza ili upoteze uwezo wako wa kuondoka.
Utitiri wa Wagombea Urais 1995 ulimfanya Nyerere atafsiri 'The Republic' ya Plato.
Tazama mapitio ya kitabu cha 'Jamhuri ya Plato Tafsiri ya Julius Nyerere' >https://t.co/2lcXFnqNzj
Again, Paul Merson is correct in everything he said here. The majority of the media aren’t holding back now. Anyone who tries to justify Man City’s cheating or defends it with the ‘they won it on the pitch’ narrative is embarrassing themselves as a pundit.
Your body is a lagging indicator of the food you eat.
Your knowledge is a lagging indicator of the information you consume.
Your happiness is a lagging indicator of the people you care about.
Ukishakuwa na watoto wanaofikiri kukuheshimu ni kukuogopa, watoto wasioweza kuonesha hofu zao mbele yako, wasioweza kukasirika mbele yako, wasioweza kukueleza hisia zao, wasioweza kusema mawazo yao mbele yako, ni suala la muda tu utashangazwa wakishaanza kuamini huna unachoweza kuwafanya.
Usidanganyike na utulivu usioambatana na uhuru. Usidanganyike na nidhamu inayotegemea woga. Usidanganyike na adabu inayoegeshwa kwenye unafiki. Binadamu ukimlazimisha kukuogopa atakushangaza. Familia inaweza kuwa na utulivu wa hatari unaochochea mifarakano mikubwa mbeleni.