๐M/kiti UVCCM UDOM
๐UDOSO PARLIAMENT SPEAKER
๐Minister of health and food UDOSO
๐General secretary Sonph- UDOSO
๐Former minister of education Mati.ilonga
Mwaka 2019/2020, tulikutana na mkulima Iringa Vijijini jina lake David Alexander - aliyekuwa ameanzisha kilimo cha tunda la apple lakini alikwama kutokana na ukosefu wa umeme. Nilimfikishia Waziri wa Nishati changamoto hiyo na gharama za kupeleka umeme zilipunguzwa kutoka milioni 300 hadi milioni 90, kupitia mpango wa REA.
Kwa ushirikiano na viongozi wa mikoa na wilaya, tulimsaidia kupata aina bora za apple na kisha kugharamia usambazaji wa miche. Leo, ameanzisha cluster inayozalisha zaidi ya tani 100 kwa msimu, na kilimo hicho sasa kimeenea Njombe, Dodoma, Kagera, na Mwanza. Ameanzisha pia bidhaa kama juisi ya apple na guide apples.
Haya ni matokeo ya Serikali kuamua kuamini ndoto ya mkulima mmoja na kuwekeza katika ndoto yenye matumaini makubwa. Tunaamini Tanzania inaweza kuwa mzalishaji mkubwa wa apple barani Afrika.
My opening remarks on Day 1 of the 3rd G25 African Coffee Summit that was held in Dar es Salaam 21-22 February 2025.
Africa is determined to move beyond being just a producer and investing in value chain opportunities particularly for Youth.
Tumeanza majaribio ya kuboresha uzalishaji wa pamba katika mikoa ya Tabora, Shinyanga, na Simiyu kwa kuhakikisha vijiji vyote 40 vinapata matrekta, maafisa ugani kupitia BBT, na matumizi ya drones kwa upuliziaji dawa.
Lengo ni kutathmini matokeo kabla ya kupanua mradi kwa mikoa mingine, huku tukifanya majaribio kama haya kwa zao la korosho. Tunajenga vituo vya mechanization, spraying, na huduma za ugani ili kulinganisha uzalishaji wa mkulima anayetumia teknolojia hizi na aliyefanya kilimo cha kawaida mwaka uliopita.
Pia, tunahamasisha Precision Agriculture kwa kuondoa upuliziaji wa mabomba, kupunguza athari za kiafya kwa wakulima, na kupunguza gharama za uzalishaji. Matokeo ya majaribio haya yataongoza utekelezaji wa mpango huu kitaifa.
Video ikionyesha Watu wa Congo ๐จ๐ฉ,
Wakifurahia baada ya kuona msafara wa jeshi la Tanzania,
Ukiingia kuwasaidia dhidi ya Vita inayoendelea huko...
Video kwa Comments ๐
WASSIRA: GARI NI INJINI SIYO BODI.
- Asema Umri wake si hoja wakaulize madaktari muhimbili
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira amewajibu Mwenyekiti CHADEMA Tundu Lissu na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho John Heche waliozungumzia umri wake hivi karibuni.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mkoani Geita leo Januari 29, 2025, Wasira amesema umri wake hauathiri uwezo wake wa kufikiri wala kufanya maamuzi sahihi.
"Mimi nina umri mkubwa lakini akili ni za miaka 55. Heche (John) akitaka akaulize madaktari wa India na Muhimbili, wamesema nina akili safi kabisa. Gari ni injini, siyo bodi," alisema Wasira huku akiwataka wapinzani wake kuzingatia hoja badala ya umri wake.
Wasira ametoa mfano wa @realDonaldTrump, ambaye amechaguliwa kuwa Rais wa Marekani katika uchaguzi wa hivi karibuni, akisema kuwa licha ya umri wake mkubwa, Wamarekani walimchagua kwa sababu ya sera zake na si kwa kuangalia umri wake.
"Heche akitaka ushahidi aende Marekani akawaulize Wamarekani kwanini walimchagua Donald Trump mwenye umri kama wangu na wakamuacha Kamala Harris mwenye miaka 60," alisisitiza Wasira.
====
December 04, 1996, Mwl, J.K Nyerere, aliitupia lawama Serikali ya Zaire (DR Congo) wakati ikiiongozwa na Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa za Banga kwamba ndiyo chanzo cha mgogoro ukanda wa maziwa makuu.
Mwl, Julius Nyerere aliilaumu serikali ya Zaire (sasa DR Congo) kwa kusababisha mgogoro katika eneo la Maziwa Makuu kwa kutaka kuwafukuza Wanyarwanda ambao wameishi ndani ya eneo hilo kwa karne nyingi.
Akizungumza New York, USA mjadala ulioandaliwa na International Peace Academy, alisema kabila la Wanyarwanda, liitwalo 'Banyamulenges', waliishi Mashariki mwa Zaire tangu eneo hilo likiwa sehemu ya Rwanda.
"Siku zote wamekuwepo katika eneo hilo kabla ya kugawanywa (na mamlaka ya kikoloni- Ujerumani na Ubelgiji)," Mwl, Nyerere alikuwa akieleza hadhara ya mabalozi wa Umoja wa Mataifa, wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na waandishi wa habari.
"Hakuna serikali yenye haki ya kuwanyima haki yao ya uraia. Banyamulenge, pamoja na kundi jingine la Wanyarwanda ambao waliajiriwa na Wabelgiji kufanya kazi kwao Zaire miongo mingi kadhaa iliyopita, walikuwa Wazaire." alisema na kufafanua Mwl. Nyerere.
"Hawawezi kurudi Rwanda... hawajui mababu zao walitoka wapi, huko Rwanda wanakwenda kuwa wakimbizi tu. Hawana ardhi huko, hao wamezaliwa Zaire." Mwl, J.K. Nyerere alisema na kuongeza: "Zaire ni nchi kubwa, inaweza kuendelea kuwahifadhi kama watu wake."
"Ni sawa na mimi ningewafukuza Maasai wanaoishi Tanzania niwaeleze waende Kenya. Huko siyo kwao. Hawana makazi, ndugu au kipande cha ardhi hata kama wanapakana na kufanana tabia na Maasai wa Kenya."
Sikiliza, unaweza kupata kitu cha kuanzia katika kuelewa mgogoro wa kivita unaoendelea Mashariki ya DR Congo.
Video credits; The Pan African News Agency (PANA).
Kutoka Ujumbe Mpaka Ukatibu wa CCM: Safari ya Kisiasa ya Dk Emmanuel Nchimbi
Makala hii ilichapishwa na The Chanzo siku aliyoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM.
@Jambotv_ Kila la heri class mate wangu, hakika vijana wa MP 2014 TUNAJIVUNIA UWEPO WAKO KATIKA TASINIA YA SIASA ZA UPANDE WA PILI UMEKUWA UKITUWAKILISHA VYEMA
*๐๐VIJANA WA VYUO WAMEWEZA KUPATA SOMO LA ITIKADI NA MKUFUNZI COMRADE MASOUD*
Vijana wa vyuo na vyuo vikuu tawi la UVCCM UDOM-TIBA likiongozwa na *Ndugu Jisinza Jisaba* wameweza Kupata mafunzo ya Itikadi ambapo katibu wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dodoma
*MWENYEKITI MWANYEMBA ATOA PONGEZI TAWI LA UVCVM UDOM TIBA*
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma *Ndugu Abdulhabeeb Mwanyemba* ametoa pongezi kwa uongozi wa Tawi la UVCCM UDOM-TIBA kwa namna ya walivyoweza kuandaa Mkutano Mkuu wa Tawi.
*๐๐VIJANA WA VYUO WAENDELEA KUPATA SOMO LA ITIKADI NA MKUFUNZI COMRADE MASOUD*
Vijana wa vyuo na vyuo vikuu tawi la UVCCM UDOM-TIBA likiongozwa na *Ndugu Jisinza Jisaba* wamendelea Kupata mafunzo ya Itikadi ambapo katibu wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dom.
*UVCCM UDOM TIBA IMESHIRIKI KIKAMILIFU ZOEZI LA UPANDAJI WA MITI*
Tawia la UVCCM UDOM-TIBA likiongoza na mwenyekiti wake *ndugu Jisinza Jisaba* limeshiriki kikamilifu katika upandadaji wa miti. Hii nisambasamba na kuunga mkono juhudi ya kutunza mazingira.