Aliyepigwa Risasi na Kukatwa Mguu Oktoba 29 afunguka kwa uchungu mbele ya Tume
Dar es Salaam. Tume ya Rais ya Uchunguzi leo ilikuwa Ilala kusikiliza waathirika wa matukio yaliyotokea Oktoba 29, 2025 na kuendelea.
Moja ya watu waliotoa ushuhuda mbele ya Tume ni kijana George Chipeta ambaye ni fundi magari aliyepigwa risasi mguuni akiwa kwenye pikipiki alipokuwa kwenye shughuli zake.
Mkutano huu ni mwendelezo wa ziara ya Tume kuzungumza na wadau mbalimbali nchini ikiwemo waathirika wa matukio ya Oktoba 29, 2025.