@FamWorld2025 Hata wewe subiri uzae mtoto wa kiume, afu uone mtoto wako wa kiume anatapeliwa na wadada wa mjini, uzuri we ni mwanamke, always Son is favorite to mom, na mama ni mwanamke na anajua mwanamke yupi tapeli na wife material βοΈ,
Julai 25 kila mwaka ni siku muhimu kwa Taifa letu, Siku ya Mashujaa, ambapo tunaungana kuwakumbuka na kuwashukuru wale wote waliotoa maisha yao kupigania uhuru na kulinda amani na heshima ya nchi yetu. Tunaendelea kuwaombea wapumzike kwa amani.
Tunapowaenzi mashujaa wetu, sote kwa pamoja tuendelee kukumbuka pia wajibu wetu wa kubaki kuwa wazalendo kwa nchi yetu, kulinda uhuru, amani, utulivu na mshikamano waliotuachia wale waliotutangulia, huku tukifanya kazi kwa bidii kwa maendeleo ya Taifa letu.