@Royaltv_plus Jemedari haya ni Mambo ya kijani na Manjano, Tumekwama hapo kwa sababu ya Ushenzi. na Mshenzi ni Mshenzi tu, Nyuma Mwiko ni washenzi. Utapoteza muda tu.
“Nimepigania Haki na Demokrasia kwa sehemu kubwa ya maisha yangu ili kuwe na nchi ya Demokrasia, imekuwa ni ideal kwa nchi yangu, msimamo huo umenigharimu sana, umeniletea madhira mengi sana, msimamo huo kwa siku zilizobaki kwa maisha yangu ni msimamo ambao nitaendelea kuusimamia, na kama ikibidi KUFA nipo tayari KUFA…”-; Mhe. Tundu Lissu
September 28, 2026
REPOST 200
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 337
Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Tanzania Bara Amani Golugwa.
Mhe. Lissu: Umeshuhudia tatizo la wagombea kuenguliwa baada ya kurudisha fomu?
Golugwa: Nafahamu lipo tatizo la wagombea kuenguliwa.
Mhe.Lissu: Haya matatizo yamekuwa yanawakabili wagombea wa vyama vyote au Chadema pekeee?
Golugwa: Yamekuwa yakiwapata wagombea wa Chadema na vyama vingine vya upinzani isipokuwa CCM.
Mhe. Lissu: Je umewahi kumuona mgombea wa CCM alienguliwa?
Golugwa: Hawajawahi kabisa kuenguliwa.
Mhe. Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kuhusu ripoti za Kimataifa ulizosoma?
Golugwa: Ripoti za SADC, Umoja wa Afrika, EU na Taasisi ya Thabu Mbeki na hizi zote zilikuwa za Mwaka 2025.
Mhe. Lissu: Anza na Ripoti ya Umoja wa Afrika kwanza imesema Uchaguzi wa Tanzania hauna viwango na haujakidhi matakwa na miongozo ya chaguzi za kidemokrasia duniani.
Waliona wapiga kura wakipewa kura na wasimamizi na kuziingiza kwenye masanduku ya kura.
Anasimama Ajuaye anasema muda umeisha kwahiyo tuendelee kesho.
Jaji Ndunguru anaahirisha shauri mpaka kesho saa tatu asubuhi.
Naomba Repost yako