Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, Tanzania imeshuhudia mageuzi makubwa katika sekta mbalimbali kupitia utekelezaji wa miradi ya kimkakati. Miradi hiyo imejumuisha ile mipya kama ya kukuza sekta ya utalii na miundombinu, pamoja na miradi iliyorithiwa kutoka awamu zilizopita na kuendelezwa kwa kasi mpya.
Sambamba na hayo, Serikali imeendelea kuweka misingi madhubuti ya maendeleo kwa miaka ijayo kupitia dira mpya ya taifa.
Mafanikio haya yanadhihirisha dhamira ya dhati ya Serikali kuijenga Tanzania ya kisasa, nchi inayopaa kiuchumi huku maisha ya Watanzania yakiboreka siku baada ya siku. Hii ndiyo Tanzania tunayojenga.
@SuluhuSamia@ikulumawasliano #DiraYaSamia #KaziNaUtu2025 #KumenogaSioMchezo #KaziNaUtuTunasongaMbele
Rais Samia Suluhu Hassan amenunua tiketi 10,000 kwa ajili ya mashabiki watakaoshiriki ufunguzi wa mashindano ya CHAN 2024 unaofanyika leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa mkoani Dar es Salaam.
Julai 25 kila mwaka ni siku muhimu kwa Taifa letu, Siku ya Mashujaa, ambapo tunaungana kuwakumbuka na kuwashukuru wale wote waliotoa maisha yao kupigania uhuru na kulinda amani na heshima ya nchi yetu. Tunaendelea kuwaombea wapumzike kwa amani.
Tunapowaenzi mashujaa wetu, sote kwa pamoja tuendelee kukumbuka pia wajibu wetu wa kubaki kuwa wazalendo kwa nchi yetu, kulinda uhuru, amani, utulivu na mshikamano waliotuachia wale waliotutangulia, huku tukifanya kazi kwa bidii kwa maendeleo ya Taifa letu.
Don't listen to him. Go to vocational school and learn welding, electrical installation, mechanical work, plumbing, bricklaying, carpentry, painting, tiling, catering, tailoring, hairdressing, vehicle repair, panel beating, spraying, etc. Don't let these people deceive you.
Bodi ya Filamu Tanzania inaendelea kuboresha Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza kwa kuwaongezea weledi wa utayarishaji bora wa filamu kwa wanatasnia kupitia mafunzo kwa njia ya uchambuzi wa Filamu (Film Screening).
Uchumapo zabibu katika shamba lako la mizabibu, usichume mara ya pili, zilizobaki apewe mgeni, yatima na mjane- katika kupata kwako usiwasahau walio kosa
Wapende sana watoto wako maana wakikosa upendo leo, watautafuta kwa maumivu wakiwa watu wazima.
Mtoto asiyeonja upendo nyumbani, hukua akiuomba kila mahali hata pasipofaa. Na wala hatojua kuwa anauomba.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, amesema Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) linakamilisha taratibu za kuufanya muziki wa Singeli kutambulika rasmi kuwa sehemu ya orodha ya urithi wa dunia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimtunuku Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Pili kwa Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Ali Shein kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 26 Aprili, 2025.