Furaha kwenye maisha inatuonesha uzuri wa maisha ya dunia tunayoishi ila huzuni inatupa funzo kuwa kuna sehemu bado hatupo bora tunatakiwa tuzidi kujifunza.
Furaha ni hali ya akili na moyo inapatikana katika mambo madogo ya kila siku kama vile kucheka na rafiki au kufanikisha malengo makubwa. Kutafuta furaha kunaweza kutufanya tuwe na mtazamo mzuri zaidi na kuishi kwa amani ya ndani.
Kusamehe ni hatua muhimu katika kuachilia mazito ya zamani. Wakati mwingine tunabeba maumivu kwa muda mrefu na kujikuta tukifanya maamuzi mabaya kutokana na hasira kusamehe hutoa njia ya kujiponya na kujikomboa kutoka kwenye hisia mbaya.