Flashback - 2024 nilipokua natoa taarifa ya Maendeleo ya Ushirika kwa Naibu Waziri Mkuu - Mhe Dotto Biteko.
Na sasa Benki ya Ushirika @coopbanktz si ndoto, si maneno tena, imekua uhalisia.
Mapinduzi kwenye sekta ya Kilimo na Ushirika yanawezekana na yanaendelea. #Agenda1030
📍Kigamboni, Dar es Salaam
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, Mhe. @JMakamba akisaini Kitabu cha Maombolezo alipofika nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika Dkt. Faustine Ndugulile Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo tarehe 01 Disemba 2024.
Hayati Dkt. @DocFaustine alifariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
Picha kwa Hisani ya @CloudsMediaLive
Mwenyekiti wa Bodi ya @ushirika_tcdc Bw. @amnsekela akiongozana na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege pamoja viongozi wa @CRDBBankPlc wametembelea banda la KDCU Ltd inayoshiriki maonesho ya wakulima…
Waziri wa @ViwandaBiashara Mhe. Dkt. Seleman Jaffo, ametembelea banda la Chama Kikuu cha Ushirika cha KDCU Ltd katika maonesho ya nane nane, ambapo amepongeza amepongeza jitihada za chama katika uzalishaji, uongezaji thamani na utafutaji wa masoko shindani ya zao la kahawa.
📍Tabora
VYAMA VYA USHIRIKA VIJIJINI OMBENI l UWAKALA WA KUSAMBAZA MBOLEA - SILINDE
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. @DavidSilinde (Mb), amevitaka Vyama vya Ushirika vijijini kuendelea kuomba uwakala wa kusambaza mbolea katika maeneo yao ili kuweza kuwafikia wakulima kwa wakati.
Amesema wakati wa ufunguzi wa Siku ya Ushirika Duniani (SUD) katika viwanja vya Nanenane vilivyopo Ipuli, Mkoani Tabora tarehe 1 Julai 2024 ambapo amemwakilisha Waziri wa Kilimo. Mhe. @HusseinBashe (Mb).
“Msimu wa 2021/2022 - 2023/2024 Vyama vya Ushirika vilitumika katika usambazaji wa pembejeo mbalimbali ili kuweza kuwafikia wakulima wake kwa urahisi zaidi, ambapo jumla ya shilingi 1,172,239,240,501 zilitumika kuagiza pembejeo. Hivyo, naelekeza Vyama vya Ushirika hususan vilivyopo vijijini viendelee kuomba uwakala wa usambazaji wa pembejeo katika maeneo ya wakulima kwa wakati,” amesema Naibu Waziri Silinde.
Aidha, taasisi za kifedha zimepongezwa kwa kuendelea kusaidia Sekta ya Kilimo kimtaji na kuwapatia wakulima mikopo ya jumla ya shilingi trilioni 33.159. Kati ya hiyo, shilingi trilioni 3.317 ilitolewa kwenye Sekta ya Kilimo, sawa na asilimia 10 ya mikopo yote.
Ameipongeza pia Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Wadau wake katika kuhamasisha na kuchangia mtaji katika Benki ya Taifa ya Ushirika tarajiwa kupitia wekezaji kutoka kwa Vyama vya Ushirika na wadau, ili iweze kufikia mtaji unaotakiwa na kuwa Benki kamili ya Taifa ya Ushirika.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara Kilimo na Mifugo, Mhe. Deo Mwanyika (Mb) amesema kuwa Kamati hiyo inafanyia kazi suala la kuboresha sheria za ushirika na sera ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu yake vizuri.
Viongozi mbalimbali wamehudhuria Siku ya Ushirika Duniani wakiwemo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bw. Deusdedith Kitwale; Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Hussein Omar; na Mrajis Mkuu wa Vyama vya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege.
Kauli mbiu ya maadhimisho ni "Ushirika Hujenga Kesho iliyo Bora kwa Wote", ambapo maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 6 Julai 2024.
📸: W/Kilimo
@WizaraKilimo@ushirika_tcdc@amnsekela@dailynewstz
Salaam Ndugu Zangu.
#BajetiYaWakulima IMEPITA ✅
Awali ya wote nichukue fursa hii kuwashukuru Viongozi wenzangu na Menejimenti na Taasisi mbali mbali za Wizara ya Kilimo kwa kufanikisha kwa uweledi na umahiri mkubwa uwasilishaji wa hoja ya Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Maonyesho ya ‘From Farm To Lab’ yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge Dodoma.
Niwashukuru wadau wote walioitikia wito wa kuhudhuria na kuwa na sisi kwenye Bajeti hii ya Kihistoria ya Wizara ya Kilimo.
Pamoja na Vipaumbele vyetu 6 tunajivunia kuwa #BajetiYaWakulima imejikita kwenye mabadiliko yatakayoleta tija kwenye
1)Korosho
2)Sukari
3)Tumbaku na
4) Kahawa reforms
Shukrani za dhati ziende kwa Waheshimiwa Wabunge wenzagu kwa kuwa na imani na Wizara na kazi zake kwa mara nyingine, tunashukuru mapendekezo na ushauri wote tuliopokea na tunaahidi kufanyia kazi kwenye utekelezaji. Tunawasihi msichoke kutufikishia mawazo yenu pale mnapoona tunaweza kuboresha utekelezaji wa bajeti hii na mipango yake.
Kwa nafasi ya kipekee Nimshukuru Dkt @SuluhuSamia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwekeza kwenye Sekta Ya Kilimo. Hii imani uliyotupa, hakika hatutokuangusha.
Tunaahidi kusimamia utekelezaji kwa umahiri na uzalendo ili kuleta tija kwenye maendeleo ya Taifa hili na kufanikisha maono mapana ya Maendeleo na Mapinduzi kwenye Sekta ya Kilimo.
Taifa Letu, Kesho Yetu.
Kazi Iendelee
Leo nimehudhuria Mkutano Mkuu wa 14 wa Wadau wa zao la Kahawa kujadili namna ya kuboresha na kukuza zao hili la kimkakati nchini.
Mkutano huu umewakutanisha Wakulima, Wazalishaji, viongozi wa vyama vya ushirika pamoja na wamiliki wa viwanda vya uchakataji wa zao la kahawa.
Uzalishaji wa Zao la Kahawa umefikia tani 80,000 ikiwa mavuno bado yanaendelea na upande wa tija imeongezeka toka 0.3 hadi 1 sawa na ongezeko la asilimia 67. Malengo yetu ni kufika tani 300,000 Ifikapo mwaka 2030, hii ni ishara njema ya mikakati tuliojiwekea.
Nimeviagiza vyama vya Ushirika Kukusanya mahitaji ya wanachama wao ili kupatiwa pembejeo za kilimo na kuepusha madeni yanayolimbikizwa kwa wanachama.
Nimemuelekeza Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa kuhakikisha zoezi la kuwachimbia visima wakulima linafanyika haraka ili kuwahakikishia kilimo cha uhakika cha kuendeleza kukuza tija.
Pia serikali inapitia upya mnada wa Kahawa ili kuendelea kumnufaisha mkulima.
Niwashukuru wakulima wa zao la Kahawa, Wadau na Waheshimiwa wabunge wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda biashara kilimo na Mifugo Mhe. Mariam Ditopile kwa kuhudhuria kwao katika mkutano huu. Tumepokea maoni ya kamati na motisha yao kuungana nasi katika mpango wa kuongeza Bajeti ya Kilimo na kuhakikisha Fedha zinafika kwa wakati ili kutekeleza mipango ya Kuboresha kilimo hapa nchini. #Agenda1030
🏆 The Fairtrade Global Awards 2023 officially starts today! Attendees will be able to celebrate and experience the farmers, workers, businesses, and organisations that have worked continuously to show that the future is fair. Stay tuned for a winner announcement and event recap.
🇹🇿🇬🇧
Alisoma Chuo Kikuu cha Hull nchini Uingereza. Akawa Mshauri wa Rais wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, Mtumishi Wizara ya Mambo ya Nje, Msaidizi wa Rais Kikwete, Mbobevu wa Diplomasia na Sheria za Kimataifa, Balozi wa Tanzania nchini China, Vietnam na Mongolia…
📍Karagwe, Kagera
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama Kikuu wakichangia mada wakati wa Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa ELCT-Kayanga hapo jana Aprili 05, 2023.
📍Karagwe, Kagera
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya kusindika kahawa ya @TanicaCafe, Kamanda wa Polisi Mstaafu Alfred Tibaigana akitoa salaam za Kampuni hiyo katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa KDCU Ltd uliofanyika Ukumbi wa ELCT-Karagwe hapo jana Aprili 05, 2023.
📍Karagwe, Kagera
Mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wilaya za Karagwe na Kyerwa - KDCU Ltd ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. @innobash akiwaaga wajumbe wa mkutano huo hapo jana.
📍Karagwe, Kagera
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Wilaya za Karagwe na Kyerwa (KDCU Ltd) Bw. Melitus Biduli akiwasilisha Taarifa yake katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama hicho uliofanyika Ukumbi wa ELCT-Karagwe hapo jana Aprili 05, 2023.