Kiongozi Mkuu wa kanisa Katoliki Duniani Papa Leo wa 14 yuko katika maandalizi ya safari yake ya kwanza Kimataifa tangu achaguliwe kuliongoza Kanisa Katoliki Ulimwenguni mwezi mei mwaka huu.
Askofu Mkuu na msaidizi wa kiongozi wa juu wa Kanisa Katoliki nchini Lebanon Paul Sayah,amesema kuwa Vatcan bado inashughulikia mpango huo na wanangojea tarehe rasmi ya kutangazwa kwa ziara hiyo ambapo ziara hiyo itakuwa na umuhimu mkubwa kwa papa kwani amekuwa akisisitiza mara kwa mara kuhusu amani Mashariki ya Kati na mshikamano wa kidini.
“Lebanon ni nchi yenye tamaduni na dini mbalimbali na ni mahali pa mazungumzo,ni miongoni mwa maeneo machache ambapo Waislamu na Wakristo wanaishi pamoja kwa kuheshimiana hivyo ujumbe wake kwa ukanda mzima utakuwa wa maana.” Amesema Askofu Sayah.
Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu wapi Papa ataelekea kwa mara ya kwanza nje ya Italia, kwani safari za awali mara nyingi huashiria mwelekeo wa utume wa Papa mpya Kwa mfano, ziara ya kwanza ya Papa Francis mwaka 2013 kwenda kisiwa cha Lampedusa, Italia, iliweka msisitizo wake katika suala la uhamiaji na jamii zilizotengwa.
Katika miongo ya hivi karibuni, safari za kimataifa zimekuwa sehemu kuu ya upapa, zikimsaidia Papa kuungana na Wakatoliki duniani kote kusambaza ujumbe wake na kushiriki katika diplomasia.
#MillardAyoUPDATES
Huyu ndiyo mchezaji ambaye Man United walimkosa kwenye mechi dhidi ya Arsenal. Huyu angekuwepo pale mbele na Mbeumo na Cunha Man United wangepata japo draw. Dirisha la usajili bado lipo wazi, Man United fanyeni maamuzi sahihi.
Umekaa zako unatafakari ela za malejesho mara gafla mtu anakuita kwa sauti mbele za watu “we Lucas mfipa”..was it necessary to call me mfipa,Next time taloga mtu ndio mtajuwa nguvu ya kabila langu😀
ROSE NDAUKA anasema kama hawataki KATIBA MPYA basi wafute mfumo wa vyama vingi tujue moja ila sio kuwa mtu unapiga kura kwa unaemtaka anatangazwa asie shinda hii sio sawa na suala la kupotea watu linamuumiza kwa kuwa wanaopptea ni vijana wamaisha ya kawaida wasio waviongozi...